Siri ya soda ya coca cola na funzo kwa maisha

Hio siri haina tija..brand ni brand tu....wanaikuza tu hii stori wanajishtukia wao..dunia hii ya mchina wakiamua kuja na copy ya cocacola hawashindwi basi tu wao wako na machines na technology kwa sasa na sio drinks
 
Hii huwa naona ni fix tu
Sure wanajishtukia wao tu...kumbe hata hakuna mtu mwenye mpango wa kushindana nao..ni brand inayoheshimika tu ila sidhan kama wachina waamue kuja na copy yake wakashindwa basi tu wachina wanawaza mengine hawataki ushindani Kwenye beverages
 
Hivi unajua kuwa viwanda vyote vya Coca-Cola duniani (ikiwemo hapa kwetu Tanzania) havijui fomula halisi ya kinywaji hicho? Hapa ndipo akili kubwa inapopiga pesa duniani kote kupitia mbinu hizi:
Viungo vyote vya siri vinachanganywa na kupikwa Marekani pekee ili kutengeneza kioevu kizito (concentrate). Viwanda vya ndani vinapokea dumu hilo likiwa limefungwa; kazi yao ni kuongeza maji, sukari, na gesi tu. Hawajui kilichomo ndani!

Karatasi yenye fomula ya cocacola imefungiwa kwenye chumba cha teknolojia ya juu chini ya ardhi kule Atlanta. Ni viongozi wawili tu wa kampuni wanaoijua, na ni marufuku kusafiri kwenye ndege moja isije kutokea ajali siri ikapotea.
Walikataa kuisajili serikalini kama hakimiliki (patent). Sababu? Sheria inataka ukiandikisha hakimiliki, baada ya miaka 20 lazima uweke siri wazi ili kila mtu aige. Coca-Cola waligoma ili kuzuia mtu mwingine yeyote kupika kinywaji chao.
👇
Kama Coca-Cola wanalinda siri ya maji na sukari kwa miaka 140 kwa ulinzi mkali hivi, inakuwaje wewe unavujisha siri za familia, mipango yako ya maendeleo, au michongo ya hela kwa kila mtu vijiweni na kwenye magroup ya WhatsApp?

Usivujishe fomula ya maisha yako kabla hata haijaanza kufanya kazi! 😁
siri ya mafanikio ndiyo
 
Mbona kama chai ?

Hao watu wawili ni immortal hawajafa tu tokea Coca-cola ianzishwe miaka hiyo ?

Vipi kama wakifa je , coca-cola itakufa au ?
 
Saa nyingine hutaki kujua siri za watu mara ghafla unakutana na motivation speaker anakuambia siri ambazo matajiri hawataki ujue wakati yeye bado maskini pamoja na kujua hizo siri.
 
Ana akili gani huyo juha zaidi ya kuokoteza madesa?! Halafu mbaya zaidi desa lenyewe kabofoa kuliwasilisha.
Ili Dunia iwe na ladha lazima kuwe na watu kama wewe😁😁😁
 
Unakutana na mtu from nowhere tu anakuelezea hela aliyoipata kwenye shughuli zake siku io na hela anayopataga kila siku!!
 
Back
Top Bottom