Siku Cocacola ilipogundua kwamba haimiliki Coca Cola

Siku Cocacola ilipogundua kwamba haimiliki Coca Cola

CreativeSanta

Member
Joined
Aug 26, 2026
Posts
16
Reaction score
18
Mwaka 1985, kampuni yenye brand inayotambulika kuliko viongozi wengi wa dunia ilifanya jambo lisiloaminika.

Iliua bidhaa yake yenyewe!.

Si kwa sababu ilikuwa imefilisika wala si kwa sababu ilikuwa imepoteza soko, bali kupitia mshindani wake bwana pepsi aliyekua akiwaambia wanywaji wa Coke kwa vitendo kua “Huenda hamna uhakika na mnachokipenda.”

Kwa miaka kadhaa Pepsi ilkua ikisukuma blind taste challenge, kampeni ambayo iliwawekea watu glass mbili zenye vinywaji vyeusi bila kuwaambia walikuwa wakinywa brand gani. Katika vipimo hivyo, Pepsi mara nyingi ilipata matokeo mazuri.

Kwa mara ya kwanza, Coke haikuonekana kama ukweli usiohitaji kuulizwa. Ilionekana kama kitu ambacho kingeweza kupingwa.

Hapo ndipo mambo yalipoanza kubadilika.

Pepsi haikuwa ikijaribu tu kuuza soda. Ilikuwa ikijaribu kuvunja uhusiano kati ya Coca-Cola na uhakika. Kama ungeweza kumfanya mnywaji wa Coke akubali kwamba, bila label angeweza kuchagua Pepsi, basi ulikuwa umeingiza shaka mahali ambapo counter-advertising pekee isingeweza kutatua.

Kujibu tishio hilo, Coca-Cola ikaingia maabara. Vipimo vikafanyika. Formula mpya ikatengenezwa. Blind taste-test ikawa reverse engineered kwa kuwapa watu glass mbili zenye formula mpya ya Coke vs Pepsi. Matokeo yakawa mazuri yakiegemea formula mpya ya Coke, Wakajua wameichapa Pepsi kwa fimbo yake yenyewe iliyoichuma.

Uamuzi huu wakubadilisha formula ulikuwa wa busara kabisa kwenye karatasi.

Aprili 23, 1985, Coke ya zamani ikaondoka. Kilichofuata baada yake hakikufanana na data.

Watu wakaghafirika na kutrhow tantrums kama mtoto agavirikavyo ukimanyang'nya toy yake. Watu hawakukasirishwa tu na ladha. Walikasirishwa na kupoteza kitu walichodhani ni chao.

Simu na barua za malalamiko zikamiminika kuelekea makao makuu, Atlanta. Pressure ikaongezeka. Ndani ya miezi michache, Coca-Cola ikarudisha formula ya zamani kama Coca-Cola Classic, huku ikikiri kufanya makosa yalokua na msukumo wa blind taste-test.

Coca-Cola ilikuwa imepima blindly kile kilichokuwa kwenye chupa, haikuwa imepima kilichokuwa ndani ya mioyo ya watu.

Kwa miaka mingi, Coca-Cola haikuwa imeuza kinywaji pekee. Ilikuwa imeingia kwenye Krismasi, kwenye birthday, kwenye first date, kwenye chakula cha familia kiasi chakufanya kawaida ya maisha ya watu.

Mtu aliposema anataka Coke, wakati mwingine hakuwa akiomba ladha tu, alikuwa akiomba kitu alichokijua.

Lakini Pepsi ilikuwa imegundua upande mmoja wa siri hiyo: mara nyingi binadamu anaweza kupendelea kitu tofauti akipewa chaguo bila historia.

Coca-Cola ikagundua upande mwingine kua tatizo lilikuwa kudhani uamuzi wa sekunde chache mbele ya kikombe ndio uamuzi ule ule ambao mwanadamu hufanya mbele ya kitu ambacho amekijengea kumbukumbu kwa miaka.

Huwezi ku-blindfold memory. Huwezi kuiweka nostalgia kwenye kikombe kidogo cha plastiki.

Huwezi kupima kwa sekunde chache kile ambacho brand imejenga ndani ya mtu kwa miongo kadhaa.


Pepsi kwa upande wake, ilikuwa imegusa ukweli huu bila kuumiliki kikamilifu ikidhani imemaliza na kufika pale ilipopataka nakusahau kwamba, brands kubwa huishi hasa wakati label haijafichwa.

Vita ikaendelea kutoka kwenye ladha kwenda kwenye akili. Coke na Pepsi hawakuwa wanapigania tu koo la mtu.

Walikuwa wanapigania dakika moja kabla ya uamuzi - ile sekunde ambayo mtu anaangalia chupa mbili na tayari ana hisia kuhusu moja kabla hata hajanywa.

Na hapo ndipo maana ya ushindani mzima inabadilika. Kampuni kubwa hazipigani tu kwa bei wala hazipigani tu kwa matangazo.

Zinapigania kumfanya mtu ahisi kwamba bidhaa hiyo imekuwa yake muda mrefu kabla hajafika dukani.

Na kitu kinapokuwa sehemu ya wewe mwenyewe, hata kampuni iliyokitengeneza inaweza kugundua siku moja kwamba HAIKIMILIKI TENA!
_________________________________
 
Mwisho wa siku.

Cocacola = Ngolo Kante

Pepsi = Yusuph Kagoma
 
Back
Top Bottom