Siri ya Pinda kunusurika

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

ALHAMISI, DESEMBA 26, 2013 11:40 NA MWANDISHI WETU



*Katibu Umoja wa Wanawake aadhirika kikaoni
*Wabunge 178 waomba kikao na Kinana



KATIKA hali isiyo ya kawaida, Ijumaa iliyopita Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliponea chupuchupu kung’olewa uenyekiti wa kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kikao hicho (party caucus) kilifanyika baada ya hali ya hewa bungeni kuchafuka baada ya kuwekwa hadharani bungeni ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyosomwa na Mwenyekiti wake James Lembeli.

Ripoti hiyo ilihusu tathmini ya upungufu kadha wa kadha uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, upungufu ulioibua mjadala mzito bungeni, na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.

Mawaziri hao ni Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na David David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi). Hata hivyo habari zilizopatikana zilisema mawaziri hao waling’olewa kwa amri ya Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa za ndani kutoka kwenye kikao hicho zilisema kuwa, Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Nkumba ndiye aliyewasha moto dhidi ya Pinda kwa kumtaka ajiondoe kwenye nafasi ya uenyekiti wa kikao hicho.

“Kwenye kikao chetu hali haikuwa nzuri, Mheshimiwa Nkumba alimtaka Waziri Mkuu ambaye kikanuni ndiye Mwenyekiti wa kikao ajiondoe mwenyewe kwenye uenyekiti kutokana na udhaifu wake kiutendaji.

“Na kweli bwana, baada ya Nkumba kumbana Pinda kweli kweli, tukashangaa kumuona Waziri Mkuu akielekea kutekeleza yale yaliyosemwa na Nkumba, lilikuwa jambo la kustaajabisha sana.

“Lakini kabla hajatekeleza matakwa ya Nkumba na wabunge wengine, akasimama Mbunge wa Mtera Job Lusinde na kumtaka Waziri Mkuu aendelee na uenyekiti wa kikao chetu, kwa sababu kama angetoka kama alivyotaka kufanya, basi ungekuwa mwanzo wa mwisho wake,” kilisema chanzo chetu.

Taarifa zilisema kuwa, baadhi ya wabunge walilumbana kwa kiasi kikubwa huku baadhi yao wakimtetea Waziri Mkuu wakidai mfumo uliopo unamfanya kushindwa kuchukua hatua ikiwamo ya kuwafukuza kazi watendaji waandamizi serikalini, huku wengine wakitaka ang’oke kutokana na udhaifu wake kiutendaji.

Katika kikao hicho, wabunge wa CCM walisimamia hoja ya kuwataka mawaziri waliotajwa kwenye ripoti ya Lembeli wajiuzulu.

Waziri wa kwanza kutangaza kujiuzulu alikuwa ni Kagasheki huku uamuzi wa mawaziri watatu kujiuzulu ukitangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Kagasheki alitangaza kujivua wadhifa huo saa 2:09 usiku alipokuwa akichangia majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo.

Katika maelezo yake Kagasheki alisema: “Mimi ni mtu mzima nimesikia hisia nzito sana kwa waliyoyasema wabunge. Rais Kikwete aliponiteua ilikuwa ni kwa furaha yake, yaliyotokea yametokea lakini hali ya wanyama huko si nzuri”

“Mimi mwenyewe nimewasikia na nachukua fursa hii kuachia ngazi hii ya uwaziri na nitachukua taratibu za kawaida kuijulisha sehemu inayohusika(Rais).

Baada ya Kagasheki kutangaza hatua hiyo, Spika aliwaita mawaziri Dk Nchimbi na Nahodha kuchangia hoja hiyo, hata hivyo hawakuwapo ndipo alipoitwa Dk. Mathayo na kutoa maelezo yake.

Katika maelezo yake Dk. Mathayo alisema kuwa ripoti hiyo haikumtendea haki kwani kamati ya Lembeli haikumwita kumuhoji na kwamba hata ripoti nzima haikueleza yeye kuhusika na kashfa hiyo.

Hata hivyo akihitimisha hoja hiyo Lembeli alisema Dk. Mathayo ameshindwa kusimamia mapendekezo tisa, yakiwamo matatizo ya wafugaji aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete Januari 18, 2006 alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.

Akitoa maelezo ya kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Niliona nimtafute Mkuu wa nchi (Rais Jakaya Kikwete), nilimpa picha yote ya kinachoendelea, alikubali ushauri wa Bunge; amekubali kuchukua uamuzi wa kutengua uteuzi wao(mawaziri).”

Katibu UWT aonja joto ya jiwe:

Taarifa zaidi zimesema kuwa, Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Makilagi, alipata wakati mgumu baada ya kuchukua msimamo tofauti na wabunge wenzake kuhusiana na ripoti ya Lembeli.

Hali hiyo ilikuja baada ya Makilagi kudai kuwa ripoti hiyo pamoja na mambo mengine ina mkono wa vyama vya upinzani na kwamba baadhi ya mambo ‘yalitiwa chumvi’.

Baada ya hoja yake hiyo, baadhi ya wabunge akiwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango walimshambulia kwa maneno makali huku wengine wakimshangaa kwa kukosa huruma dhidi ya wanawake ambao wanatajwa kufanyiwa unyama katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

“Mheshimiwa Makilagi yeye alionekana kuegemea upande wa Serikali, kwa wenzake walimchachafya vibaya sana, ilifikia wakati mpaka Mheshimiwa Henry Shekifu naye akazungumza kwa ukali kabisa.

“Na katika kuonyesha msisitizo ilibidi hata picha za waathirika ambazo hazikuonyeshwa bungeni zionyeshwe, ili Makilagi azione. Kwa kweli wabunge wenzake walimshangaa sana,” alisema mtoa taarifa.

Wabunge wamsubiri Kinana:

Katika hatua nyingine, joto la kuwataka mawaziri mizigo wang’oke kwa hiari au Rais Kikwete awang’oe limechukua sura mpya baada ya wabunge wa CCM kuomba kikao na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.

Taarifa za uhakika ambazo Rai imezipata zimedai kuwa tayari wabunge 178 wa CCM wameshajiorodhesha wakitaka kuonana na kiongozi huyo katika kikao kijacho cha Bunge.

“Lengo letu ni kuhakikisha mawaziri mizigo wanaondoka, na ni Kinana ambaye amewataja na kumtaka Mwenyekiti wetu Rais Kikwete awawajibishe, sasa ikiwa wale ambao wametajwa watakuwa hawajaondoka au kuondolewa hadi kikao kijacho cha Bunge, basi lazima tuonane na Kinana.


“Na tukionana naye hatuendi kunywa chai na soda, tutaonana kutaka majibu, kwa sababu kama watakuwa hawajaondoka, basi tutamlazimisha yeye (Kinana) ajiuzulu,” alisema mmoja wa wabunge machachari wa CCM, ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
 
Huyo makilagi anajikweza sana,hii ni kutokana na namna alivyobebwa kutoka kwenye kuwa mfagiaji wa ofisi ya wilaya ya ccm,kwenda mpaka UWT taifa, hadi kuwa mbunge na hatimae katibu wa wabunge wenzie.yote hii ni kazi ya Nimrod Mkono, hivyo mama yuko radhi kuitetea serikali hata kwa gharama ya damu za wa Tz.
 
Mzee Mwinyi alishasema "kila enzi ina mambo yake" enzi hii walio wengi wana sauti kubwa zaidi kuliko wachache.
 
Huyo makilagi anajikweza sana,hii ni kutokana na namna alivyobebwa kutoka kwenye kuwa mfagiaji wa ofisi ya wilaya ya ccm,kwenda mpaka UWT taifa, hadi kuwa mbunge na hatimae katibu wa wabunge wenzie.yote hii ni kazi ya Nimrod Mkono, hivyo mama yuko radhi kuitetea serikali hata kwa gharama ya damu za wa Tz.

Muache tu hiyo damu itaesabika juu yake na kizazi chake. Mungu si dharimu hata damu za watanzania zimwagike kama kuku.
 
Jamani hawa wabunge wa maccm wana2changanya cndohawa walikuwa wanasema serikali ckivu ya ccm nakumbeza mh.mnyika kwamba serikali ya jmk ni legelege! sasa hiyo mizigo yatoka wapi?
 
Hii oporesheni Tokomeza ilikuwa na maudhui gani hasa hasa!! maana hapa tunapata sura ya ujangiri lakini na uhamiaji haramu. kama mnakumbuka baada ya kikwete kutembelea kagera na sehemu zinginezo huko kanda ya magharibi ndio tukaona utesaji huu! mimi nawashangaa wabunge kutombana rais! kwa mara nyingine wabunge wanashindwa kuwa makini katika maamuzi ya suala hili!!

Rais ndie aliyetangaza hili na ndie mteua mawaziri, mkuu wa majeshi na mkuu wa polisi na sio waziri mkuu. Tulishuhudia issue ya Jairo bungeni jinsi Rais alivyofanya, Tumeshuhudia Richmond Rais alivyokwepeshwa na issue hii, EPA n.k

Ni kwa mara hii wabunge wasikurupike kutoa maamuzi bila kwanza kuondoa kiini cha tatizo.
 
soma comment yako mara mbili mbili kabla ya kupost!

Hii oporesheni Tokomeza ilikuwa na maudhui gani hasa hasa!! maana hapa tunapata sura ya ujangiri lakini na uhamiaji haramu. kama mnakumbuka baada ya kikwete kutembelea kagera na sehemu zinginezo huko kanda ya magharibi ndio tukaona utesaji huu! mimi nawashangaa wabunge kutombana rais! kwa mara nyingine wabunge wanashindwa kuwa makini katika maamuzi ya suala hili!!

Rais ndie aliyetangaza hili na ndie mteua mawaziri, mkuu wa majeshi na mkuu wa polisi na sio waziri mkuu. Tulishuhudia issue ya Jairo bungeni jinsi Rais alivyofanya, Tumeshuhudia Richmond Rais alivyokwepeshwa na issue hii, EPA n.k

Ni kwa mara hii wabunge wasikurupike kutoa maamuzi bila kwanza kuondoa kiini cha tatizo.
 
Hizi zote sinema tu na ni kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa CCM ipo tayari kwa mwaka 2015.

Kama hawa CCM suala la ujangiri limewagusa sana, mbona hatukuona kuvalia njuga ile skendo ya ndege iliyobeba wanyama kule KIA!!!
 
kwani cdm ndio wapangaji wa bei ya umeme?
kichwa maji wewe, unafikiri vyama vya upinzani kazi yake nini? kutusemea na kupaza sauti kukosoa serikali, sasa hv chadema kimekuwa mzgo na kinatukatisha tamaa.
 
hivi kutengu;liwa kwa mawaziri hawa au hata waziri mkuu akijiuzulu kutatatua matazo haya?
Mimi naona hii ni kushusha homa, bado hatuja maliza tatizo!!
 
wizara ni nyingi mno kwa waziri mkuu kusimamia zote kikamilifu, ndo 7bu kuna manaibu waziri, makatibu na watendaj wengine, kiukweli w mkuu ana kaz kubwa mno ndo mana hata yeye yuko tayar kuachia kit. kwa maoni yangu mm kabla hajafikiriwa kutoka, waanze watendaji wizaran, ila the best solution apo baadae ni kuurekebisha mfumo mzima; wizara zipunguzwe
 
waachane na pinda wa watu wakabe huyo mr vasco da gamma. au bado hajarudi ughaibuni kuzunguka dunia?
 
Back
Top Bottom