madogo, sijakusoma ndugu yangu hapo.Tamthilia imetengenezwa vizuri, inaeleweka kwa ufasaha, ina flow kwa mpango mzuri, na inatia hamasa kuiagalia. Labda kwa wale wanaoona tatizo la kuiangalia na watoto je haina age-restriction? Kuna weza wekwa alama ya PG-parental guidance kama kuna mahala panahitaji, kama mnataka kujitofautisha na hao mnao waita bongowood- ambao naona wanatoa burudani kwa viwango vyao ndio maana ni "maarufu sana" kwa watanzania wengine--tukiweza tafiti chambua kwanini wanapendwa pengine tutaondoa mtazamo 'hasi' juu yao na kuwakubali 'wao' kama 'wao'.
Na hili la swahiliwood vs bongowood' , bongomovie' ndio kitu gani?
Precisely mkuu,inaonekana ni tamthilia nzuri sana!Sijawahi kupata muda kuitazama tamthilia hii lakini kwa kuona vionjo humu ndani imenipa mzuka niitafute!
Hahahahaaaaaaa!... Ni kweli tulifika sehemu tukazinguana, hata hivyo
wiki hiyo hiyo nikapata kazi nyingine kutoka kwenye taasisi moja ya Canada
ambapo nililazimika kusafiri kwenda kutengeneza documentary ambayo ilinichukua
takriban miezi mitatu.
Kuhusiana na kazi hii ya 'Siri ya Mtungi' panapo majaaliwa nitaandika
makala maalum ikiwa kama somo maalum kwa watengeneza filamu wetu...
Mwalimu, naamini umeichek leo EATV.Sijawahi kupata muda kuitazama tamthilia hii lakini kwa kuona vionjo humu ndani imenipa mzuka niitafute!
TUKUTUKU vipi umepata chance ya kuichek leo kupitia EATV??Precisely mkuu,inaonekana ni tamthilia nzuri sana!
lol, nilijua tu nyie wasanii lazima myumbishane !
Ndio maana sikukuona kwenye EFF, that May 11-15! Ndio ulikuwa upo na hao jamaa au tulipoteana tu ukumbini??
Poa, nasubiri mambo matamu kutoka pande hizo za hao jamaa "wapya".
Unajua, mara nyingi tukikubaliana jambo basi lifanyike on time na kwa kufuata misingi.
Lakini zikishaanza longolongo mara nyingi mimi huamua kujitoa na kufanya shughuli zingine.
Huo ndiyo msimamo wangu..
TUKUTUKU vipi umepata chance ya kuichek leo kupitia EATV??
Sijui tatizo lipo wapi ila inaonekana watu wengi sana hawanataarifa za hii kitu, pamoja na jitihada zote za jamaa kujitangaza....
Sijui tatizo lipo wapi kwenye upokeaji wa taarifa!!
TUKUTUKU vipi umepata chance ya kuichek leo kupitia EATV??
Sijui tatizo lipo wapi ila inaonekana watu wengi sana hawanataarifa za hii kitu, pamoja na jitihada zote za jamaa kujitangaza....
Sijui tatizo lipo wapi kwenye upokeaji wa taarifa!!
Raia Fulani, nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Hata wachangiajisehemu yoyote akishagusa mzungu mara nyingi huwa sion ufanisi wa mwafrika. Kwenye hiyo tamthilia ni wazungu wanaongoza. Wabantu wanachezeshwa. Fungu linatoka vyanzo vya kuaminika. Ingekuwa ni zao la kampuni ya nyumbani tungeweza kusema habari nyingine. Kwa kifupi ni nzuri kwa kuwa imegharamiwa
Mkuu nimeicheki makala. umechimba sana. naona hapa kwenye siri ya mtungi wanayaendeleza yale ya CFU. Japo sijaiangalia sana, ni wazi kuwa mapenzi ndani ya hii tamthiliya yamejaa uthubutu uliokaribia kupitiliza kiasi kwamba kwa mwafrika kumwomba penzi binti au mwanamke wa kiafrika ni jambo rahisi tu. Siku zote mzungu amependa kuwa juu kwa kila jambo hata nje ya mipaka yake kwa kisingizio cha 'kufanya utafiti' juu ya jambo husikaRaia Fulani, nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Hata wachangiaji
na wafuatiliaji wa kazi hii nawashauri kuwa wasiangalie ubora tu wa picha,
waangalie mambo mengi ambayo kuhusiana na tamaduni zetu, utagundua
kuwa kwa kuwa kazi imeandaliwa na wazungu basi mambo mengi yanakosa
uhalisia wa Kiafrika bali yanakuwa yanabeba uzungu mwingi, japo Waafrika
wamehusishwa katika utengenezaji huu, hii ni kutokana na kutoshiriki kikamilifu
katika ngazi ya maamuzi; mfano aina ya mapenzi yaliyomo humo, mtazamo wa
wapenzi nk. Nimewahi kuandika makala kuhusiana na mtazamo wa Wazungu
kwa Waafrika (ambayo unaweza kuisoma kwa ku-click hapo kwenye title) jinsi
ambavyo wazungu wamekuwa wakituchukulia Waafrika. Anyway, sitaki kuiongelea
sana kazi hii 'Siri ya Mtungi', wadau waifuatilie huenda wataburudika zaidi...
sehemu yoyote akishagusa mzungu mara nyingi huwa sion ufanisi wa mwafrika. Kwenye hiyo tamthilia ni wazungu wanaongoza. Wabantu wanachezeshwa. Fungu linatoka vyanzo vya kuaminika. Ingekuwa ni zao la kampuni ya nyumbani tungeweza kusema habari nyingine. Kwa kifupi ni nzuri kwa kuwa imegharamiwa
Raia Fulani ushaanza uoga wako wa kunihisia vitu ambavyo havipo, mi pia ni raia fulani tu ambaye nina mguso wa kipekee na hizi sanaa.Tatizo ni media inayotumika. Sina hakika kama ndio sababu ya kurushwa itv au inarushwa kote. Halafu yaelekea una taarifa za ndani kuhusu hii tamthiliya. Unahusika?
Niliiangalia kama mara mbili hivi haikunishawishi kabisa . . . sijaangalia tena!
Sijui kwanini toka naanzisha hii sred tu nilijua kuna mtu ataleta hoja za "wazungu" lol....
Naona wadau karibia wote mnamsimamo unaofanana juu ya hichi kitu maana nina kijana wangu mtaani naye ni mdau sana wa tasnia toka mwanzo nimemwambia acheki hii kazi kakazana oohh wazungu wazungu!!
Miaka yote tupo sisi kama sisi "wabantu" na tasnia yetu, na wote tunajua nini tumekuwa tunafanya, Bishop Hiluka kaandika wee kukosoa na kurekebisha lakini wapi, kazi zetu tunazijua wenyewe mpaka sasa.
Kosa hasa la hao "wazungu" ni nini hapo?
Kuwa na uwezo na kugharamia kukamilisha walichoona wao kinafaa kwa kupitia sanaa yetu?
Raia Fulani, nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Hata wachangiaji
na wafuatiliaji wa kazi hii nawashauri kuwa wasiangalie ubora tu wa picha,
waangalie mambo mengi ambayo kuhusiana na tamaduni zetu, utagundua
kuwa kwa kuwa kazi imeandaliwa na wazungu basi mambo mengi yanakosa
uhalisia wa Kiafrika bali yanakuwa yanabeba uzungu mwingi, japo Waafrika
wamehusishwa katika utengenezaji huu, hii ni kutokana na kutoshiriki kikamilifu
katika ngazi ya maamuzi; mfano aina ya mapenzi yaliyomo humo, mtazamo wa
wapenzi nk. Nimewahi kuandika makala kuhusiana na mtazamo wa Wazungu
kwa Waafrika (ambayo unaweza kuisoma kwa ku-click hapo kwenye title) jinsi
ambavyo wazungu wamekuwa wakituchukulia Waafrika. Anyway, sitaki kuiongelea
sana kazi hii 'Siri ya Mtungi', wadau waifuatilie huenda wataburudika zaidi...
Najua una uzoefu katika haya masuala, wala siwezi kubishana na wewe juu ya hivi vitu, nadhani nipo kwenye nafasi ya kujifunza zaidi ili kuielewa tasnia.
Mkuu kumbuka huko juu umeeleza kuwa jamaa mlishindana kwenye masuala fulani fulani kwenye ukamilishaji wa hii kazi, so huoni kuwa ni rahisi sana mtu kusema kuwa upo biased kwa sababu hiyo???
Mkuu, hili suala la wazungu na waafrika ni suala/jambo ambalo lipo sana
hata kama hatutakubali, sitaki kuingia kwenye mjadala huo lakini kuna
mambo yanayohusiana na hili yaliyonifanya nijiondoe pale...