Naam sasa kumbe hapa ndio tumegundua ubaya na tatizo la hii tasnia yetu kutokuwa na movies za kutosha zenye themes tofauti na zenye stories zilizokwenda shule.., sababu nyie mnaoandika script zinapwaya.., mkuu umeshaandaa movies ngapi au script ngapi zenye utamaduni na weledi kama wewe unaosema..? nina uhakika ukiandika kama hii watu wataangalia na kuna Gap kubwa kwenye soko la movies kama hizi..
Mkuu, nakubaliana na wewe katika mambo mengi ila pengine tofauti yetu ni lugha
tunazoongea pengine zinatofautiana japo ujumbe unabaki kuwa ni uleule, kwa mfumo
wa soko la filamu Tanzania kama utafuata weledi kwa kiwango kikubwa unaweza
usitengeneze filamu, labda tamthilia kwa kuwa hazihitaji fadhila za wahindi kuzisambaza.
hivyo kwa mfumo huu unatufanya baadhi yetu kutupwa nje ya soko. Nimeshaandika script
kadhaa kwa soko la Bongo na hata kwa soko la nje, ila bahati mbaya sana kwa product
za Bongo (Bongo Movie) nyingi huwa ni tofauti sana na script yenyewe. Hii ni kwa sababu
mwenye kui-transform script into movie ni director ambaye inategemea weledi wake au angle
atakayoitumia katika kuitafsiri script into movie.
Mimi huiangalia sinema kwa mambo makuu matano: Script nzuri, Waigizaji wazuri, Wapigapicha
wazuri, Muongozaji mzuri na Mhariri mzuri. Naamini script ni sawa na msingi imara wa nyumba
unaotokana na ramani nzuri (stori). Kama script haitakuwa mzuri hata filamu haiwezi kuwa nzuri
kabisa, hii inamaanisha kuwa kwa script mbovu hata ukimleta muigizaji mzuri duniani hawezi
kucheza katika kiwango tulichozoea kumuona akicheza.
Waigizaji ni sawa na matofali yanayotumika katika ujenzi wa nyumba, huku wapigapicha
ni kama simenti na maji kwa ajili ya kujengea nyumba. Muongozaji ndiye fundi mjenzi,
anayepaswa kuchanganya vizuri simenti, maji na mchanga ili kupata kile kinachotakiwa.
Bahati nzuri tasnia yetu imebarikiwa kuwa na waigizaji wengi wazuri, wapigapicha wengi
wazuri na hata wahariri wengi wazuri, lakini inakosa waandishi wazuri wa script na waongozaji
wazuri wa filamu. Hii haimaanishi kuwa hakuna kabisa waandishi au waongozaaji wazuri hapa
nchini, wapo wengi tu wenye uzoefu na elimu ya kutosha katika uandishi na uongozaji wa filamu,
tatizo ni mfumo mbovu unaowafanya kutupwa nje ya ulingo wa soko la filamu kwa kuwa
hawathaminiki, hawatumiki wala hawapewi heshima inayostahili.
Script limekuwa tatizo kubwa kwenye filamu zetu, hasa kwa kuwa ni moja ya vipengele muhimu
sana katika uandaaji wa filamu na michezo ya kuigiza inabebwa na dhana ya kuwa script ni hatua
ya mwanzo, ni ramani ya kutuongoza kutoka kwenye wazo (
concept) hadi final edit.
Lakini watazamaji walio wengi hukimbilia kumlaumu mwandishi wa script pindi filamu inapokuwa
mbaya, ikisababishwa na kutoelewa nani hasa mwenye jukumu la kuhakikisha filamu inakuwa nzuri.
Hapa ndipo script inapokuwa chanzo cha mahusiano mazuri au mabaya (
a love-hate relationship)
kati ya mwandishi na timu ya uzalishaji, hasa muongozaji wa filamu.
Uhusiano mbaya huja pale muongozaji wa filamu anapoamua kubadili baadhi ya matukio ndani ya script,
wakati mwingine hubadili sehemu kubwa ya script bila hata kumshirikisha mwandishi na hivyo kuvuruga
mtiririko mzima wa stori. Kitendo hiki kinaweza kusababisha kuzalishwa filamu yenye hadithi tofauti
kabisa na iliyoandikwa mwanzo ingawa jina la mwandishi litabaki lilelile. Haya yamekuwa yakitokea sana,
binafsi yamenikuta na nimeshawahi kushuhudia yakitokea hata kwa waandishi na waongozaji wakubwa
duniani.
Filamu ni zao la muongozaji na wala si la mtayarishaji, mwandishi au muigizaji kama ambavyo wengine
wanadhani. Muongozaji wa filamu anapaswa kuwa mbunifu na kiungo muhimu kati yake na timu ya
uzalishaji. Muongozaji anawajibika katika kutafsiri script iliyoandikwa kwenye karatasi na kuihamishia
katika picha halisi na sauti kwenye skrini – na anapaswa kuiona taswira halisi na kutafsiri mtindo na
muundo wa filamu hiyo, na hivyo kufanya kazi zote mbili kama kiongozi wa timu na msimulizi kwa
kutoa picha halisi.
Tatizo kubwa lililopo kwenye tasnia ya filamu hapa Tanzania ni kwa waongozaji wetu wa filamu
kudhani kuwa kazi ya uongozaji wa filamu ni kujua: "
standby... action... cut!" na kusahau kuwa
muongozaji ndiye anayepaswa kumtengeneza mhusika kwa kutegemea muongozo unasemaje.
Kama muigizaji atashindwa kuvaa uhalisia, hilo sio kosa lake ni kosa la muongozaji na hutafsiri
uwezo wa muongozaji ulipokomea.
Sasa nikirudi kwenye swali lako la msingi: kutokana na mfumo wa soko la sasa, ukweli sina
hata movie moja niliyowahi kuandaa lakini kuna movie nyingi ambazo niliandika script au
kufanya kazi kama consultant, sound expert au director. Sasa sijui unahitaji kuziona filamu
zilizotokana na script nilizoandika au unahitaji kuziona script nilizoandika?...