Siri Ya Mtungi.

Siri Ya Mtungi.

kwa mfumo
wa soko la filamu Tanzania kama utafuata weledi kwa kiwango kikubwa unaweza
usitengeneze filamu
, labda tamthilia kwa kuwa hazihitaji fadhila za wahindi kuzisambaza.
hivyo kwa mfumo huu unatufanya baadhi yetu kutupwa nje ya soko. Nimeshaandika script
kadhaa kwa soko la Bongo na hata kwa soko la nje,
Mkuu umenikumbusha hili tatizo lilishamkumba Tyler Perry (ambae studios zilikuwa zinataka kubalisha movies zake na zilimwambia movies zake ni tofauti na wenyewe walivyotaka..) ila jamaa hakukata tamaa wala hakubadilisha mfumo wake bali alianzisha studio yake na kutoa movies zake mwenyewe.. (kwahiyo labda swali lije kwenye ugumu wa kusambaza movie mwenyewe na ku-promote mwenyewe bila kutegemea wasambazaji) nina uhakika ugumu utakuwa mwanzo tu ila ukishajenga jina watu watakufuata.., pia word of mouth na trailers za hapa na pale zinaweza zikakusaidia kwenye promo..; labda swali gumu zaidi hivi low budget movie kwa Tanzania na kwa kutumia unknown actors inaweza ikagharimu kiasi gani hadi mtu ushindwe kutoa kitu bila kushirikisha mdosi ?

ila bahati mbaya sana kwa product
za Bongo (Bongo Movie) nyingi huwa ni tofauti sana na script yenyewe. Hii ni kwa sababu
mwenye kui-transform script into movie ni director ambaye inategemea weledi wake au angle
atakayoitumia katika kuitafsiri script into movie.
Ni kweli hili ni tatizo ila nadhani cha maana ni mtu ukikosa Director anayekubaliana na wewe kwanini usivae kofia ya Director pia, na kupunguza gharama kwanini usitumie unknown actors ambao ni bei nafuu au uchukue watu wanaochipukia na kuingia mkataba wa kuwalipa baada ya mzigo kuingia sokoni na wewe kupata faida ?

Kama script haitakuwa mzuri hata filamu haiwezi kuwa nzuri
kabisa, hii inamaanisha kuwa kwa script mbovu hata ukimleta muigizaji mzuri duniani hawezi
kucheza katika kiwango tulichozoea kumuona akicheza
.
Ni kweli usemayo ila niliona interview moja ya Samuel Jackson akasema yeye huwa anaangalia script na anakwenda kuifanyia kazi na kurudi na kushauriana na mtunzi/director kuhusu hiyo script husasan kwenye Dialogue yeye mwenye hupenda kuweka maneno yake na kuboresha kwahio nadhani cha muhimu nadhani ni kwa director; script writer na actor wote kufanya kazi pamoja mwanzo mpaka mwisho kwa kukubaliana sio kila mtu kufanya kazi kivyake.
Sasa nikirudi kwenye swali lako la msingi: kutokana na mfumo wa soko la sasa, ukweli sina
hata movie moja niliyowahi kuandaa lakini kuna movie nyingi ambazo niliandika script au
kufanya kazi kama consultant, sound expert au director. Sasa sijui unahitaji kuziona filamu
zilizotokana na script nilizoandika au unahitaji kuziona script nilizoandika?...
Hapana mkuu mimi hapa kama mtazamaji wa movies ninahuzunika kwa ukosekanaji wa movies bora wakati kuna stories nyingi sana zinazoweza kutumiwa hapa nchini.., na sababu umeshafanya kazi kama Director, na umeshaandika Script nakushauri utoe kazi yako ambayo utadirect mwenyewe sababu hapo utapata kitu ambacho kitakuwa bora na kama wewe unavyokitaka..., mwanzo mgumu naukishajenga jina zaidi hata usambazaji utakuwa rahisi tu..., by the way siku ukitoa kitu ni PM nitakwenda dukani kununua na kukuunga mkono.., pili tumieni pia vitu kama Youtube kujipromote wakuu huwezi kujua huenda kazi yako akaiona jamaa ambae akakupa kazi zaidi..,
 
Mkuu umenikumbusha hili tatizo lilishamkumba Tyler Perry (ambae studios zilikuwa zinataka kubalisha movies zake na zilimwambia movies zake ni tofauti na wenyewe walivyotaka..) ila jamaa hakukata tamaa wala hakubadilisha mfumo wake bali alianzisha studio yake na kutoa movies zake mwenyewe.. (kwahiyo labda swali lije kwenye ugumu wa kusambaza movie mwenyewe na ku-promote mwenyewe bila kutegemea wasambazaji) nina uhakika ugumu utakuwa mwanzo tu ila ukishajenga jina watu watakufuata.., pia word of mouth na trailers za hapa na pale zinaweza zikakusaidia kwenye promo..; labda swali gumu zaidi hivi low budget movie kwa Tanzania na kwa kutumia unknown actors inaweza ikagharimu kiasi gani hadi mtu ushindwe kutoa kitu bila kushirikisha mdosi ?

Kuna kipindi fulani walikuja wataalam wa filamu watatu, wawili kutoka Hollywood
na mmoja kutoka Australia kwa ajili ya kufanya reasearch katika film industry ya
Bongo, hii ilikuwa ni project maalum hasa kuangalia kama inaweza kufanya kazi
baada ya Kenya kuprove failure kwenye commercial films. Bahati nzuri walikuwa
na taarifa zangu, nikatafutwa na kujiunga nao. Tulisafiri zaidi ya mikoa nane na miji
yote mikubwa yenye pilikapilika ya Tanzania.

Hivyo nikaamua kuitumia nafasi hiyo pia kufanya utafiti na kuandika ripoti yangu
ambayo ilijumuisha kuanzia script hadi distribution. Siku ukiihitaji naweza kukupatia
ripoti ya utafiti wangu niliyoipa jina la "The Perspective of the Film and
Television Industry in Tanzania" ambayo nimeshaifanyia presentation kwenye
maeneo mbalimbali, hii ndiyo iliyokuja kuzaa wazo la Swahiliwood baada ya
Taasisi ya Media for Development International-Tanzania (MFDI-Tanzania)
chini ya John Riber kuamua kuifanyia kazi. Hawa MFDI ndiyo watengenezaji
wa filamu ya Chuo na hii tamthilia ya 'Siri ya Mtungi' tunayoijadili hapa.

Katika utafiti wangu huo ambao baadaye niliamua kujiingiza kwenye biashara
ya usambazaji na kusambaza filamu mbili za "Naomi 1" na "Naomi 2" kwa kushirikiana
na kampuni ya Studio KVS, hii ilikuwa ni kufanya utafiti kwa vitendo. Mambo
niliyogundua ni kwamba ili uweze kupata mafanikio unahitaji kuwa na mtaji mkubwa
kwani wauzaji wa rejareja walioko mikoani watakuuzia kazi yako vizuri kama utakuwa
unatoa kazi mara kwa mara (ikiwezekana kila wiki), kinyume na hapo huwa wanauza
lakini wanakuwa wasumbufu kulipa hadi wasikie unatoa nyingine...

Ni kweli usemayo ila niliona interview moja ya Samuel Jackson akasema yeye huwa anaangalia script na anakwenda kuifanyia kazi na kurudi na kushauriana na mtunzi/director kuhusu hiyo script husasan kwenye Dialogue yeye mwenye hupenda kuweka maneno yake na kuboresha kwahio nadhani cha muhimu nadhani ni kwa director; script writer na actor wote kufanya kazi pamoja mwanzo mpaka mwisho kwa kukubaliana sio kila mtu kufanya kazi kivyake.
Sipingani sana na wewe ingawa wakati nasomea masuala ya uandishi wa script
(creative writing) tulifundishwa kuwa: Script nzuri inaweza kutoa filamu mbovu
lakini script mbovu kamwe haiwezi kutoa filamu nzuri. Naamini unaweza kupata
product nzuri kutokana na script mbovu endapo mtashirikiana (hasa kama ni kundi
la watu wenye weledi) kuiboma na kuiboresha vizuri. Hii itatokana na muongozaji
endapo hatakuwa overall incharge (maana wengine huwa hawataki kushauriwa)...
 
Kwanza niwatake radhi wanajamvi kwa kupotea kwangu na kuwaachia mjadala, mniwie radhi sana sidhani kama mmetafsiri kuwa nilikula kona!

Nimekuwa na matatizo makubwa sana ya kiafya ila Mungu ananipigania, nawashukuru wote ambao mmetoa michango yenu na sana wale wanaofuatilia tamthiliya hii na kuunga mkono vipaji vya watz wenzetu ambavyo soko la kijinga limekuwa limevificha sijui kwa maslahi ya nani!!

Mkuu, labda tutafute focus maana tumekuwa tukiongelea vitu vingi mno,
ungependa tujikite kwenye kuangalia nini? ...

Mkuu wangu Bishop Hiluka, sihitaji tufocus kwenye kukosoa hii kazi japo nakiri kuwa kuna mapungufu fulani kama ulivyotolea mfano kuwa hata kazi makini kiasi gani lazima itakuwa na mapungufu hata kama ni 0.005% ka 100%.

Ninachotamani kusikia ni kama hapa chini ulivyosema na kueleza.

Mwisho, labda niweke wazi, binafsi waliotengeneza hii kazi ni rafiki zangu,
nimeshafanya nao kazi, pia nilikuwa na mkataba nao wa script ambao umekwisha
December 31, 2012, na sasa niko huru lakini kuna kazi nyingine tumekubaliana kufanya
baadaye mwaka huu kama Mungu akipenda na kama tutafikia makukubaliano. Haya
ninayoyachangia humu huwa nawaeleza hata wao wenyewe physically, bila unafiki wala
kuongopeana na wao huwa wananipa ufafanuzi, na mwisho wa siku tunamaliza mjadala...

Hayo maneno hapo juu yameusuuza mtima wangu na kububujika kwa furaha isiyo kifani kuwa sisi watz ni tunaweza sana, na aje mwingine aseme miradi yake aliyoshiriki wapi amefikia kikwazo ni nini halafu tupeane mawazo.

Hoja hapa ni kuwa positive katika kazi kubwa tulizo na uwezo wa kuzifanya sisi kama sisi pamoja na kushirikiana na dunia nyingine hata kama ni Mzungu au Kaburu......

Mheshimiwa Raia Fulani kuna kipindi alikuwa na mipango ya kuzama kwenye tasnia, basi na yeye aseme amefanya nini amefikia wapi alikutana na nini na mambo mengine kama hayo....

Hizi mbwembwe za kutaka kukosoa kila kitu na kutafutiza vimakosa kwenye kazi ambazo ni dhahiri kuwa watu wameonyesha umakini, matokeo yake ni kuyumbisha mashabiki na vijana wanaotaka kujifunza sanaa ya filamu.

Nafarijika kwa hatua unazopitia Mkuu Bishop Hiluka, na nashukuru mara nyingi nafuatilia harakati zako pale unapotushirikisha, ndio maana hadi leo sijasahau ule mjadala wetu wa Swahiliwood na leo tunaona matunda yake kama ulivyoahidi.
Na hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa naamini miongoni mwa watu wenye mawazo makubwa!
 
Last edited by a moderator:
Sujui ni kwenye runinga yangu tu, naona picha zake hazipo clear. Ila ni miongoni mwa kazi nzuri za wabongo. Kuna dosari za hapa na pale, kama wakati ule Cheche alipokuwa anapigana na jamaa mmoja mle studio inaonesha kabisa kwamba wanaigiza kupigana. Angalia jinsi wanavyorusha ngumi (mikono) yao.
 
Kwanza niwatake radhi wanajamvi kwa kupotea kwangu na kuwaachia mjadala, mniwie radhi sana sidhani kama mmetafsiri kuwa nilikula kona!

Nimekuwa na matatizo makubwa sana ya kiafya ila Mungu ananipigania, nawashukuru wote ambao mmetoa michango yenu na sana wale wanaofuatilia tamthiliya hii na kuunga mkono vipaji vya watz wenzetu ambavyo soko la kijinga limekuwa limevificha sijui kwa maslahi ya nani!!

Mkuu wangu Bishop Hiluka, sihitaji tufocus kwenye kukosoa hii kazi japo nakiri kuwa kuna mapungufu fulani kama ulivyotolea mfano kuwa hata kazi makini kiasi gani lazima itakuwa na mapungufu hata kama ni 0.005% ka 100%.

Ninachotamani kusikia ni kama hapa chini ulivyosema na kueleza.

Hayo maneno hapo juu yameusuuza mtima wangu na kububujika kwa furaha isiyo kifani kuwa sisi watz ni tunaweza sana, na aje mwingine aseme miradi yake aliyoshiriki wapi amefikia kikwazo ni nini halafu tupeane mawazo.

Hoja hapa ni kuwa positive katika kazi kubwa tulizo na uwezo wa kuzifanya sisi kama sisi pamoja na kushirikiana na dunia nyingine hata kama ni Mzungu au Kaburu......

Mheshimiwa Raia Fulani kuna kipindi alikuwa na mipango ya kuzama kwenye tasnia, basi na yeye aseme amefanya nini amefikia wapi alikutana na nini na mambo mengine kama hayo....

Hizi mbwembwe za kutaka kukosoa kila kitu na kutafutiza vimakosa kwenye kazi ambazo ni dhahiri kuwa watu wameonyesha umakini, matokeo yake ni kuyumbisha mashabiki na vijana wanaotaka kujifunza sanaa ya filamu.

Nafarijika kwa hatua unazopitia Mkuu Bishop Hiluka, na nashukuru mara nyingi nafuatilia harakati zako pale unapotushirikisha, ndio maana hadi leo sijasahau ule mjadala wetu wa Swahiliwood na leo tunaona matunda yake kama ulivyoahidi.
Na hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa naamini miongoni mwa watu wenye mawazo makubwa!
Mkuu na wewe umefikia wapi kwenye michakato yako? Mimi nimesitisha kwanza ule mpango nikisubiri baadhi ya mambo kuwa sawa. Hii haimaanishi kuwa siruhusiwi kukosoa kazi za sanaa
 
Naam this is what am talking about.., sasa kwa kuweka hii kitu online (kwa episodes za mwanzo au kuchombeza mmefanya jambo la maana ili ambao hawajaona waone ni nini mnaongelea) ngoja niiangalie kwanza taleta comments baadae

Siri ya Mtungi Sehemu ya 1 (with English Subtitles) - YouTube

Poa sana mkuu, na tena shukrani!

Nasubiri mrejesho wako Mkuu wangu, japo kwenye page ya kwanza ya threda hii kuna mdau aliweka video ya highlight za vipande kadhaa.

Chukua mda wako ujiridhishe kiongozi, nasubiri mani yako tena tuendeleze mjadala chanya juu ya tasnia yetu kwa mifano halisi.
 
Mkuu na wewe umefikia wapi kwenye michakato yako? Mimi nimesitisha kwanza ule mpango nikisubiri baadhi ya mambo kuwa sawa. Hii haimaanishi kuwa siruhusiwi kukosoa kazi za sanaa

Raia, mi sina mchakato wowte kwa sasa japo kwa baadae nafikiria ku-team up na Hiluka (japo sijafanya mawasiliano naye yoyote kwa sasa zaidi ya kwenye mijadala ya hapa jamvini) na au wadau wengine makini ili nije na mfumo wa usambazaji kwa kazi zote za sanaa, kwanzia Music na Filmu na kazi zingine za sanaa zitakazo kuwa zinasambazika kupitia mfumo huo!
 
Ni poa kutuletea miendelezo ya siri ya mtungi,maana sometime kazi za kioffisi zikizidi mtu hupati hata fursa kidogo ya kuangalia,shukran kwako
 
Raia, mi sina mchakato wowte kwa sasa japo kwa baadae nafikiria ku-team up na Hiluka (japo sijafanya mawasiliano naye yoyote kwa sasa zaidi ya kwenye mijadala ya hapa jamvini) na au wadau wengine makini ili nije na mfumo wa usambazaji kwa kazi zote za sanaa, kwanzia Music na Filmu na kazi zingine za sanaa zitakazo kuwa zinasambazika kupitia mfumo huo!

Ni vyema ndugu. Usambazaji si kazi rahisi lakini. Sijui utatumia mfumo gani. Pia kwenye filamu yuko mwekezaji mmoja anaitwa Wigan. Sijui kama umewahi kumsikia au kusikia mikakati yake
 
jouneGwalu, hili nalo unalijibuje? Hebu cheki na hii link hapa

Mbona hicho cha kwenye hiyo sred kimesemwa hata kwenye hii sred yetu bro??
Au ulitaka kunionyesha nini kwenye hiyo sred?

Kwa uzoefu wangu finyu wa tamthiliya zenye viwango barani afrika, bado sijaona tatizo la "picha chafu" kwenye "Siri ya Mtungi"......

Hivyo hiyo sred inawakilisha kundi fulani la wanafiki tu katika jamii yetu ambalo nahofia linaweza kuwa kubwa na kwa kiasi fulani ndio limefanya tasnia yetu kuwa hivi ilivyo na bado wanalalamika ila makwao wamejaza maCD ya wakina Hemed wakinyonyana ndimi na wakina Wolper......

Unafiki!
 
Duh! Teh teh teh!...
 
Bahati mbaya nimekumbwa na gharika la digitali. Kisimbuzi ninacho lakini, ila ndio hivyo sijaweza ona tv. Panaweza kuwa na tofauti kati ya filamu na tamthiliya maana filam huwekewa madaraja. Tamthiliya ikirushwa imerushwa. Lakini hata ukitazama tamthiliya za wenzetu hakuna popote penye ukakasi
 
Published on 17 Jan 2013"Siri ya Mtungi" ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha, inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa Studio ya Kupiga Picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili wenye afya na huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu.

Siri ya Mtungi's cast of colourful characters, related by blood or marriage, or simply by love, make up a community that is inspired by love, brought down by fear, superstition and betrayal, lifted by comedy and joy, and strengthened by the intimate bonds of family and friendship.

Siri ya Mtungi Sehemu ya 1 (Episode 1 with English Subtitles)

Source: swahiliwood ya youtube
 
Last edited by a moderator:
Siri ya Mtungi Sehemu ya 2 (Episode 2 with English Subtitles)

Source: swahiliwood ya youtube
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom