Siri ya Marekani kuingilia uchaguzi mkuu Tanzania

Nawasilisha kama nilivyokuta Mahali mwandishi yuko hapo chini.
Hivi karibuni Marekani kupitia kikao cha 116 cha Bunge la Congress ilipitisha Azimio la kuitaka Tanzania kufanya uchaguzi huru na haki.

Azimio hili lilibeba kichwa cha habari kinachosomeka kama ifuatavyo:

"Urging the Government of Tanzania and all parties to respect human, civil, and political rights and ensure free and fair elections in October 2020,and recognizing the importance of multi-party democracy in Tanzania."

Ukitazama kichwa cha habari cha azimio lile utaona limetaja serikali ya Tanzania na vyama vyote vya siasa nchini, lakini ajabu kilichoelezwa ndani kinailenga serikali ya Tanzania peke yake. Hapa ndipo sisi watanzania tunapaswa kujiuliza maswali, kuna siri gani imejificha?

SIRI NI HII

Ukweli ni kwamba Marekani inaumizwa sana na jinsi serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ilivyoweza kuyabana makampuni makubwa ya uwekezaji ( Multinational Companies kwa kifupi MNCs) mfano kampuni ya Barrick Gold Mine ambayo kwa miaka mingi yaliifanya Tanzania kama mahali pa kuchota rasilimali bure bure. Hili linawauma mno.

Kuna watu wanaweza kusema Barrick ni ya wacanada, wakatazame wanahisa (shareholders) wa Barrick ni kina nani? Fidelity Management and Research Group (FMR) ni mwanahisa mmojawapo wa Barrick. FMR inatoka Boston. Vanguard Group inatoka Pennsylvania. Haya ni baadhi ya makampuni yenye hisa Barrick.

Suala la demokrasia ni kichaka ambacho Marekani imekuwa ikitumia kuficha mipango yake. Kwa nini nasema ni kichaka? Ili kuelewa hili ijue demokrasia halisi ya Marekani kutokea Djibouti.

Nani anaifahamu Djibouti?

Djibouti inaongozwa na Rais anaitwa Ismail Omar Guelleh tangu mwaka 1999 wakati huo Rais Magufuli hata hajawa Waziri kamili wa Ujenzi. Rais Guelleh maarufu kama IOG anaongoza Djibouti mpaka leo hii kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Mwaka 2010 Bunge la Djibouti liliondoa ukomo wa kumruhusu Rais Guelleh kugombea kwa mara ya 3 baada ya kumaliza awamu zake mbili za miaka mitano mitano kwa mujibu wa Katiba ya Djibouti mbele ya macho ya Wamarekani hali iliyozua maandamano na watu kupigwa.

Hapa tunapaswa kujiuliza, "Kama Marekani inapigania Demokrasia, kwa nini waliacha Katiba ya Djibouti ikachezewa?"

Djibouti ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo demokrasia haina nafasi kabisa lakini Marekani imekaa kimya miaka yote. Tumeshawahi kujiuliza ni kwa nini?

Kama hatujui jibu basi tutazame website ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani www.state.gov kwenye kipengele cha "US-Relations with Djibouti" tutakuta maelezo haya "The Djiboutian government is supportive of US interests."

Kwamba, "Nchi ya Djibouti inaunga mkono maslahi ya Marekani" au kwa lugha nyingine "Djibouti inalinda maslahi ya Marekani." Ni maslahi gani hayo? Kujua maslahi gani hayo msome DG Jamieson hapa chini.

Akiwa Kapteni wa Jeshi la Afrika Kusini katika kamandi ya Majini (SAND) DG Jamieson aliandika andiko la kiutafiti mwaka 2009 akitathmini uwepo wa kamandi kubwa ya kijeshi ya Marekani Afrika (AFRICOM) pale nchini Djibouti.

Andiko hili lilikwenda kwa jina la "AFRICOM: A threat or opportunity for African security?" yaani "AFRICOM: ni kitisho au fursa kwa usalama wa Afrika." Wasomi wetu, vijana wa kitanzania mnaweza kulisoma ili muwaelimishe na wengine pia.

Katika hitimisho lake Kapteni Jamieson alibaini mambo makuu mawili, mosi Marekani imeweka base ile ya kijeshi ya AFRICOM kwa lengo la kuongeza ushawishi Afrika na pili kulinda maslahi ya makampuni ya mafuta ya kimarekani ambayo yanachimba mafuta arabuni na kandokando mwa bahari (Offshore) na si kitu kingine. Hivyo kwa kifupi kwa mujibu wa Jamieson AFRICOM haiisaidii Afrika katika usalama hata kidogo.

Hivyo kwa Marekani ni sahihi kwa nchi ya Djibouti kutokuwa na demokrasia kwa sababu tu inalinda maslahi ya makampuni ya Marekani.

Kimsingi "maslahi ya makampuni ya Marekani" ndiyo sababu inayofanya Marekani iipende Djibouti na kuisifia huku ikiichukia Tanzania ya sasa. Huu ndiyo ukweli.

Kuthibitisha hili rejea Azimio lililopitishwa na Bunge la Congress kuna paragraph inasomeka hivi:

Whereas some United States companies operating in Tanzania have reported harassment, corruption, and lack of respect for contracts and business operations, which threatens future United States business investment and trade partnerships;

Azimio linadai kuwa baadhi ya makampuni ya Marekani yaliyopo Tanzania yameripoti kubughudhiwa, rushwa, kutoheshimiwa kwa mikataba na uendeshaji biashara hali ambayo inatishia uwekezaji wa makampuni ya Marekani Tanzania.

Tujiulize, kudaiwa kodi ambayo ni haki yetu watanzania ni kubughudhiwa?

Au kuzuiwa kwa mchanga wenye madini yaani makinikia kwa faida ya watanzania ni kutoheshimu mikataba?

Au huku kuibuka kwa Laizer kuwa bilionea ni rushwa?

Waseme kweli!

Ukweli ni kuwa Marekani wanaumizwa sana na hizi Bilioni 700 zinazolipwa na Barrick baada ya kubanwa kimkataba. Tena inawauma zaidi kwa sababu walileta wataalamu wa majadiliano (negotiations) 40 na wakashindwa, hii inauma zaidi. Huu ndiyo ukweli mchungu ambao Marekani unawakera sana, hawataki tu kusema kweli na kamwe hawatosema hadharani.

Ukitaka kuona wameumizwa na hizi bilioni 700 zinazolipwa rejea makubaliano ya azimio lile la Congress limeeleza ifuatavyo:

(3) urges the Government of Tanzania to foster a robust, market-led business environment conducive to continued United States trade and investment in Tanzania, including respect for the legal and contractual rights of United States companies operating in Tanzania;

Kwamba, "Tanzania iiwekee Marekani mazingira mazuri ya kufanya biashara Tanzania."

Ni mazingira gani mazuri wanayotaka Marekani ikiwa Tanzania tayari inatekeleza mpango kazi wa kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ( Blueprint) ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kupitia mikataba, na kuweka mfumo bora wa masoko tangu mwaka 2015.

Tuulizane kwa pamoja "Ni mazingira gani mazuri wanayomaanisha Marekani?"

Au mazingira ya kunufaika wao Marekani peke yao tu halafu sisi Tanzania hatunufaiki kisha baadae watuletee madawati waandike "Kutoka kwa watu wa Marekani" ilihali ni hela yetu iliyopatikana kiujanjaujanja?

Na hili napenda lieleweke wazi kuwa ni hela yetu kwa sababu ardhi yetu ndiyo inatumika kuwanufaisha raia wa Marekani.

Kuthibitisha hili kuwa ni hela zetu, Slaughter (2009) alipata kuandika "How US multinational companies strengthen the US economy" kwa Kiswahili "Ni namna gani makampuni makubwa ya Marekani yanaimarisha uchumi wa Marekani."

Katika kitabu hiki Slaughter anasema:

U.S. multinational companies are, first and foremost, American companies. As a group, U.S. multinationals perform large shares of America’s productivity-enhancing activities that lead to high average compensation for American workers.

Kwa kifupi alichoeleza Slaughter ni kuwa wafanyakazi wa Marekani wanafidiwa na hela inayopatikana kutoka katika makampuni makubwa mfano wa Barrick, je si hela yetu hiyo?

Sasa hii ndiyo sababu halisi ya kuingilia uchaguzi wa mwaka huu. Marekani imeona Tanzania imefumbua macho kutoka usingizini hivyo inajaribu kutumia kichaka cha Demokrasia ili kuhakikisha anapatikana mtu atakaelinda maslahi ya Marekani kama alivyo Guelleh pale Djibouti ili wafanyakazi wa Marekani waendelee kunufaika na madini ya watanzania.

Nasema ni demokrasia kwao ni kichaka cha kuficha mipango yao kwa sababu hata tafiti zinaonesha wazi.

Rejea utafiti uliofanywa juu ya mfumo linganifu wa Marekani uliochapishwa na Taasisi ya Kifalme ya Masuala ya Kimataifa ya London kama nilivyonukuu hapa chini:

A study of the inter-American system published by the Royal Institute of International Affairs in London concluded that, while the US pays lip service to democracy, the real commitment is to “private, capitalist enterprise.” When the rights of investors are threatened, democracy has to go; if these rights are safeguarded, killers and torturers will do just fine.

Tafsiri pana hapa ni kwamba; "Wakati Marekani inahubiri demokrasia, mkazo halisi upo kwenye makampuni yao ya kibepari. Pindi wanapoona kile wanachoita 'haki' za wawekezaji wao zikiwa hatarini basi demokrasia haina budi iondoke katika nchi hiyo, na ikiwa 'haki' hizo zitalindwa basi kiongozi anaweza kukaa madarakani atakavyo na wala hawatojali suala la kutokuwepo kwa demokrasia."

"Tujiulize ni haki zipi za makampuni ya Marekani zimebanwa kiasi kwamba wajidhihirishe waziwazi kuunga mkono mgombea fulani kwa sababu tu ameonesha kuyahakikishia makampuni ya Marekani kunufaika na rasilimali zetu?"
Tujiulize kwa makini?

Au tujiulize ni makampuni gani ya sekta binafsi ambayo yanabanwa Tanzania ikiwa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini TPSF imeipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa ushirikiano?

Nawashauri watanzania wenzangu tuwe makini sana tusije tukajikuta tunaingizwa walipo Libya hivi sasa kwa sababu za ulafi wa baadhi yetu.

*Watu watumie wasaa huu kujiuliza, ikiwa Marekani inasapoti demokrasia Tanzania kwa nini hivi sasa imeacha Libya wakiuana ikiwa walidai hakukuwa na demokrasia? Lengo lao ni lipi?

Muhnu wa hano:

Zihnu Ditalitali.
Tunakwenda na Tundu Lissu no matter what.

Reelecting CCM and Magufuli in 2020 is akin to insanity..... ie doing the same thing over and over again for 6 decades expecting different results. No bloody way..... it's time for CCM and Magufuli to be dumped OUT!!
 
Marekani inachotaka ni uvunjifu wa haki za binadamu ukome, kubambikizia wengine kesi za kipumbavu kwasababu za kisiasa
Uvunjifu mkubwa wa sheria na mambo mengine ya Hovyohovyo kutoka kwa jiwe!
Acheni kusingizia Marekani ili muendeleze ujinga wenu
Wewe ni liability kwa familia, hivi kwenda kumuua yule kamanda wa Iran walikuwa wanatekeleza haki za binadamu? Kuwaambia Misri walipue Bwawa la kuzalisha umeme la Ethiopia hizo ndo haki za binadamu?
 
Mwaka huu lazima mtatema ndoano pumbavu nyie! Mmezoea kuvuruga chaguzi zote ila awamu hii hamna pakutokea
Bora mzungu kuliko ccm
 
Hakuna wa kumlinganisha na Magufuli sasa, huyo tundu mwambieni Siku tatu zijazo tutakua tumeshamziba.

Hivi mtu anakaa ulaya zaidi ya miaka miwili, hatujui alikua anapata wapi pesa ya kula, kulala mahotelin, kunywa mvinyo, kusafiri nchi kama USA, UK, Germany n.k kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ili kuchafua nchi ya Tanzania.
Halafu wiki moja kabla uchaguzi kuanza unarudi ukidai kutaka kuongoza nchi hiyo hiyo yenye watu zaidi ya milioni 60.

Ni kichaa pekee ndio atamuamini na kumpigia kura huyo tundu.

Halafu wewe tundu, chuki zako binafsi kwa Mh Raisi Magufuli usitake kuwauzia watanzania wote hizo chuki.
Watanzania wanampenda Magufuli
 
Hivi tupo tayari kughafiriana na USA na magharibi yote kisa hatutaki kufuata misingi ya haki, usawa kwa wote na utawala bora? Nani alisema hatuwezi kulinda madini na mali asili zetu huku tukiwa na demokrasia na utawala safi.

Kuweka sawa haya mambo wala haitucost chochote na ni tija na hazina kwa taifa zima tusitafute mchawi nani na visingizo lukuki wakati tunajivuruga wenyewe. Kabla ya kutazama kibanzi kwenye jicho la USA, tutazame boriti kwenye jicho la TZ ya sasa.

Wazungu yes ni wahuni, wachina ndio kabisa wahuni kupindukia. Tunapaswa kuwa wajanja we play diplomacy, soft power, hard power etc depending na situation ndo tutasurvive hii dunia sio kushupaza shingo kifala fala tutavunjwa.
Umeongea point nzito mpka mwili wngu umesisimika
 
Mimi simpendi ******** na nitakua kichaa wa kwanza kumpigia TUNDU LISU
Hakuna wa kumlinganisha na Magufuli sasa, huyo tundu mwambieni Siku tatu zijazo tutakua tumeshamziba.

Hivi mtu anakaa ulaya zaidi ya miaka miwili, hatujui alikua anapata wapi pesa ya kula, kulala mahotelin, kunywa mvinyo, kusafiri nchi kama USA, UK, Germany n.k kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ili kuchafua nchi ya Tanzania.
Halafu wiki moja kabla uchaguzi kuanza unarudi ukidai kutaka kuongoza nchi hiyo hiyo yenye watu zaidi ya milioni 60.

Ni kichaa pekee ndio atamuamini na kumpigia kura huyo tundu.

Halafu wewe tundu, chuki zako binafsi kwa Mh Raisi Magufuli usitake kuwauzia watanzania wote hizo chuki.
Watanzania wanampenda Magufuli
 
Nawasilisha kama nilivyokuta Mahali mwandishi yuko hapo chini.
Hivi karibuni Marekani kupitia kikao cha 116 cha Bunge la Congress ilipitisha Azimio la kuitaka Tanzania kufanya uchaguzi huru na haki.

Azimio hili lilibeba kichwa cha habari kinachosomeka kama ifuatavyo:

"Urging the Government of Tanzania and all parties to respect human, civil, and political rights and ensure free and fair elections in October 2020,and recognizing the importance of multi-party democracy in Tanzania."

Ukitazama kichwa cha habari cha azimio lile utaona limetaja serikali ya Tanzania na vyama vyote vya siasa nchini, lakini ajabu kilichoelezwa ndani kinailenga serikali ya Tanzania peke yake. Hapa ndipo sisi watanzania tunapaswa kujiuliza maswali, kuna siri gani imejificha?

SIRI NI HII

Ukweli ni kwamba Marekani inaumizwa sana na jinsi serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ilivyoweza kuyabana makampuni makubwa ya uwekezaji ( Multinational Companies kwa kifupi MNCs) mfano kampuni ya Barrick Gold Mine ambayo kwa miaka mingi yaliifanya Tanzania kama mahali pa kuchota rasilimali bure bure. Hili linawauma mno.

Kuna watu wanaweza kusema Barrick ni ya wacanada, wakatazame wanahisa (shareholders) wa Barrick ni kina nani? Fidelity Management and Research Group (FMR) ni mwanahisa mmojawapo wa Barrick. FMR inatoka Boston. Vanguard Group inatoka Pennsylvania. Haya ni baadhi ya makampuni yenye hisa Barrick.

Suala la demokrasia ni kichaka ambacho Marekani imekuwa ikitumia kuficha mipango yake. Kwa nini nasema ni kichaka? Ili kuelewa hili ijue demokrasia halisi ya Marekani kutokea Djibouti.

Nani anaifahamu Djibouti?

Djibouti inaongozwa na Rais anaitwa Ismail Omar Guelleh tangu mwaka 1999 wakati huo Rais Magufuli hata hajawa Waziri kamili wa Ujenzi. Rais Guelleh maarufu kama IOG anaongoza Djibouti mpaka leo hii kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Mwaka 2010 Bunge la Djibouti liliondoa ukomo wa kumruhusu Rais Guelleh kugombea kwa mara ya 3 baada ya kumaliza awamu zake mbili za miaka mitano mitano kwa mujibu wa Katiba ya Djibouti mbele ya macho ya Wamarekani hali iliyozua maandamano na watu kupigwa.

Hapa tunapaswa kujiuliza, "Kama Marekani inapigania Demokrasia, kwa nini waliacha Katiba ya Djibouti ikachezewa?"

Djibouti ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo demokrasia haina nafasi kabisa lakini Marekani imekaa kimya miaka yote. Tumeshawahi kujiuliza ni kwa nini?

Kama hatujui jibu basi tutazame website ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani www.state.gov kwenye kipengele cha "US-Relations with Djibouti" tutakuta maelezo haya "The Djiboutian government is supportive of US interests."

Kwamba, "Nchi ya Djibouti inaunga mkono maslahi ya Marekani" au kwa lugha nyingine "Djibouti inalinda maslahi ya Marekani." Ni maslahi gani hayo? Kujua maslahi gani hayo msome DG Jamieson hapa chini.

Akiwa Kapteni wa Jeshi la Afrika Kusini katika kamandi ya Majini (SAND) DG Jamieson aliandika andiko la kiutafiti mwaka 2009 akitathmini uwepo wa kamandi kubwa ya kijeshi ya Marekani Afrika (AFRICOM) pale nchini Djibouti.

Andiko hili lilikwenda kwa jina la "AFRICOM: A threat or opportunity for African security?" yaani "AFRICOM: ni kitisho au fursa kwa usalama wa Afrika." Wasomi wetu, vijana wa kitanzania mnaweza kulisoma ili muwaelimishe na wengine pia.

Katika hitimisho lake Kapteni Jamieson alibaini mambo makuu mawili, mosi Marekani imeweka base ile ya kijeshi ya AFRICOM kwa lengo la kuongeza ushawishi Afrika na pili kulinda maslahi ya makampuni ya mafuta ya kimarekani ambayo yanachimba mafuta arabuni na kandokando mwa bahari (Offshore) na si kitu kingine. Hivyo kwa kifupi kwa mujibu wa Jamieson AFRICOM haiisaidii Afrika katika usalama hata kidogo.

Hivyo kwa Marekani ni sahihi kwa nchi ya Djibouti kutokuwa na demokrasia kwa sababu tu inalinda maslahi ya makampuni ya Marekani.

Kimsingi "maslahi ya makampuni ya Marekani" ndiyo sababu inayofanya Marekani iipende Djibouti na kuisifia huku ikiichukia Tanzania ya sasa. Huu ndiyo ukweli.

Kuthibitisha hili rejea Azimio lililopitishwa na Bunge la Congress kuna paragraph inasomeka hivi:

Whereas some United States companies operating in Tanzania have reported harassment, corruption, and lack of respect for contracts and business operations, which threatens future United States business investment and trade partnerships;

Azimio linadai kuwa baadhi ya makampuni ya Marekani yaliyopo Tanzania yameripoti kubughudhiwa, rushwa, kutoheshimiwa kwa mikataba na uendeshaji biashara hali ambayo inatishia uwekezaji wa makampuni ya Marekani Tanzania.

Tujiulize, kudaiwa kodi ambayo ni haki yetu watanzania ni kubughudhiwa?

Au kuzuiwa kwa mchanga wenye madini yaani makinikia kwa faida ya watanzania ni kutoheshimu mikataba?

Au huku kuibuka kwa Laizer kuwa bilionea ni rushwa?

Waseme kweli!

Ukweli ni kuwa Marekani wanaumizwa sana na hizi Bilioni 700 zinazolipwa na Barrick baada ya kubanwa kimkataba. Tena inawauma zaidi kwa sababu walileta wataalamu wa majadiliano (negotiations) 40 na wakashindwa, hii inauma zaidi. Huu ndiyo ukweli mchungu ambao Marekani unawakera sana, hawataki tu kusema kweli na kamwe hawatosema hadharani.

Ukitaka kuona wameumizwa na hizi bilioni 700 zinazolipwa rejea makubaliano ya azimio lile la Congress limeeleza ifuatavyo:

(3) urges the Government of Tanzania to foster a robust, market-led business environment conducive to continued United States trade and investment in Tanzania, including respect for the legal and contractual rights of United States companies operating in Tanzania;

Kwamba, "Tanzania iiwekee Marekani mazingira mazuri ya kufanya biashara Tanzania."

Ni mazingira gani mazuri wanayotaka Marekani ikiwa Tanzania tayari inatekeleza mpango kazi wa kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ( Blueprint) ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kupitia mikataba, na kuweka mfumo bora wa masoko tangu mwaka 2015.

Tuulizane kwa pamoja "Ni mazingira gani mazuri wanayomaanisha Marekani?"

Au mazingira ya kunufaika wao Marekani peke yao tu halafu sisi Tanzania hatunufaiki kisha baadae watuletee madawati waandike "Kutoka kwa watu wa Marekani" ilihali ni hela yetu iliyopatikana kiujanjaujanja?

Na hili napenda lieleweke wazi kuwa ni hela yetu kwa sababu ardhi yetu ndiyo inatumika kuwanufaisha raia wa Marekani.

Kuthibitisha hili kuwa ni hela zetu, Slaughter (2009) alipata kuandika "How US multinational companies strengthen the US economy" kwa Kiswahili "Ni namna gani makampuni makubwa ya Marekani yanaimarisha uchumi wa Marekani."

Katika kitabu hiki Slaughter anasema:

U.S. multinational companies are, first and foremost, American companies. As a group, U.S. multinationals perform large shares of America’s productivity-enhancing activities that lead to high average compensation for American workers.

Kwa kifupi alichoeleza Slaughter ni kuwa wafanyakazi wa Marekani wanafidiwa na hela inayopatikana kutoka katika makampuni makubwa mfano wa Barrick, je si hela yetu hiyo?

Sasa hii ndiyo sababu halisi ya kuingilia uchaguzi wa mwaka huu. Marekani imeona Tanzania imefumbua macho kutoka usingizini hivyo inajaribu kutumia kichaka cha Demokrasia ili kuhakikisha anapatikana mtu atakaelinda maslahi ya Marekani kama alivyo Guelleh pale Djibouti ili wafanyakazi wa Marekani waendelee kunufaika na madini ya watanzania.

Nasema ni demokrasia kwao ni kichaka cha kuficha mipango yao kwa sababu hata tafiti zinaonesha wazi.

Rejea utafiti uliofanywa juu ya mfumo linganifu wa Marekani uliochapishwa na Taasisi ya Kifalme ya Masuala ya Kimataifa ya London kama nilivyonukuu hapa chini:

A study of the inter-American system published by the Royal Institute of International Affairs in London concluded that, while the US pays lip service to democracy, the real commitment is to “private, capitalist enterprise.” When the rights of investors are threatened, democracy has to go; if these rights are safeguarded, killers and torturers will do just fine.

Tafsiri pana hapa ni kwamba; "Wakati Marekani inahubiri demokrasia, mkazo halisi upo kwenye makampuni yao ya kibepari. Pindi wanapoona kile wanachoita 'haki' za wawekezaji wao zikiwa hatarini basi demokrasia haina budi iondoke katika nchi hiyo, na ikiwa 'haki' hizo zitalindwa basi kiongozi anaweza kukaa madarakani atakavyo na wala hawatojali suala la kutokuwepo kwa demokrasia."

"Tujiulize ni haki zipi za makampuni ya Marekani zimebanwa kiasi kwamba wajidhihirishe waziwazi kuunga mkono mgombea fulani kwa sababu tu ameonesha kuyahakikishia makampuni ya Marekani kunufaika na rasilimali zetu?"
Tujiulize kwa makini?

Au tujiulize ni makampuni gani ya sekta binafsi ambayo yanabanwa Tanzania ikiwa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini TPSF imeipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa ushirikiano?

Nawashauri watanzania wenzangu tuwe makini sana tusije tukajikuta tunaingizwa walipo Libya hivi sasa kwa sababu za ulafi wa baadhi yetu.

*Watu watumie wasaa huu kujiuliza, ikiwa Marekani inasapoti demokrasia Tanzania kwa nini hivi sasa imeacha Libya wakiuana ikiwa walidai hakukuwa na demokrasia? Lengo lao ni lipi?

Muhnu wa hano:

Zihnu Ditalitali.
Paragraph yako ya mwisho imenifungua sana akili na imefanya niwaze mambo mengi sana.
Asante
 
Mtu yeyote anayesaidia kuiondosha CCM madarakani huyo mtu ni mwema sana.
 
Tunataka mabadiliko tu, hatutaki ujinga sisi Uhuru ,haki ndo jawabu ya hayo matakataka uliyoleta hapa.
 
Watu hamkos visingizio ila ukweli adui wa mwafrika ni mwafrika mwenyewe. Sku zote watawala wa afrika wamekua na udikiteta na ukaid kwa raia wao ndo maana inapotokea upenyo wa mataifa ya magharibi wanaingia kirais kwani ni raia wenyewe wanakua wamechoka. Mfano tu kama unafuatiria kampain nyomi looote la watu wanaomfata Tundu lissu sidhani kama wanaubiriwa na us hapana ni watu wenyewe wanachoka hivo wanataka mabadiliko kwavile watawala hawapo tiyar kuachia madaraka mambo ndo hayo wazee wa kaz watakuja kuondoa takataka. Ninasema mwaka huu muandike waraka wa vitisho namna ipi, ntuambie vita sijui nini tutapiga kura kwa lissu liwalo na liwe tumechoka tumechoka tumechoka.
 
Mtoa mada umeandika mambo ya maana ambayo wenye akili timamu wote tunayaelewa

Cha ajabu utawaona wanaowaza kwa kutumia WOWOWO watakavyokushambulia

Narudia tena jina linalowastahili ni WATU WANAOWAZA KWA KUTUMIA WOWOWO

Sasa wakiitwa watu wenye akili utaenda na wewe?
 
Wengine hizo kelele za wamarekani ndo zinatupa mzuka wa kulazimika kusafiri kwenda kumchinja jamaa yao kesho.
 
Back
Top Bottom