Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

too low!!!!
 
Haya sasa!!!!!!!!!!!!

Mambo ndiyo hivyo tena!!!!

Karibu kunapambazukaaaaaaaa!!!!!!
 
Tatizo lako unaogopa kivuli nimeshakwambia. unafiki wako unakufanya uishi kwa presha kijana umaarufu wako mtandaoni usije ukivimba kichwa.Wish 2015 ifike mapema ndo kitaeleweka,Unafiki wako unamwisho wait and u will see very soon.
Mwisho mimi sio mwanasiasa na wala kamwe sifikirii kua mwanasia so pole sana kwa kuishi kwa hisia.
 
nadhani hamjamuelewa zitto,yeye kajibu juu ya huyo mwandishi anayedai eti kijana Ben alitaka kumpa sumu ktk hicho kikao na hotel husika,amekana kuwa hajawahi kuwa na hicho kikao na hamfahamu bwana Ben.inakuwaje tuzidi kulazimisha jambo ambalo halikutendeka,hakukuwa na kikao kati ya zitto na ben ktk hotel tajwa,sasa hiyo simu angepewaje?
tatizo ni hao vijana wengine ambao yawezekana ndio walikuwa ktk hicho kikao sasa photoshop inatengenezwa ili ionekane kuwa zitto alikuwa na kikao na Ben na Ben alitaka kumpa sumu zitto.
 

Mwali haya mambo ni sort of complicated. Take note: nimesema "Inawezekana wanamkubali genuinely" kuwa kuna possibility... While hapo hapo other words kuna nafasi pana ya kufikiria kuwa hata otherwise ni sawa.
 

Kijana mwanasiasa uliyebuma, nakumbuka nilivyokuona kwenye TV ukilia kwa sauti hi hi hi hi nirudishe hi hi hi nisamehe Mtela Mwampamba kaokoka leo bado wewe ,na wewe utakuja kukana kiapo chako cha kutumika kama condom na Zitto,kiboko yako MBatia
 

Kaka sijui kama unajui implication ya ulichoandika hapaa, kama ni kweli mnampango wa kublack mail Zito jueni mambo mawili
1. Is criminal offense so ur liable to face lawsuits
2. Since u have expose the plan here damage is already done and whatever u will do no serious damage expected. Vipi kaka una video nyingine ya zito akipanga mauaji ya Denis Msaky au una nini kipya!!!???

Jamani jamaniii jamaniii jamaniiii wanasiasa wachumia tumbo wanaoendesha siasa za kuchafuanaa na jana la kizazi hiki na kijachoooo!!!!

Hao kimaa unaowazungumzia wako kwenye shamba la jiranii tenaa mbali kabisaaa sasaa lenye mahindi ya kutosha wanataka wavukeashamba matatu waje shamba la CDM kama sio uharibifuu ni niniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MY BROTHER ZITO LEARN FROM UR OWN MISTAKE THIS GUYS WAMETANGAZA VITAA NA IF I WONDER WHY DO U ENTERTAIN THEM ON THE FIRST PLACEE..... MAANA NI WATUU WAPUUZI AMBAO HAWAELEWIKI NINI WANACHOFANYAAAA.. AU ULIWAAHIDI UTAHAMA NAO KWENDA CCM??!!!!

HALAFU NYIE VIJANA BADO WADOGO MNA MAISHA MAREFU YA KUJENGA CARRIER ZENU KWENYE SIASA MNAFANYA SIASA AMBAZO I BET U WILL LAST IN GAME FOR A YEAR. U R NOT STRATEGIC..... BROTHER....
NARUDIA TENAAAA.. NASIKITISHWA SANAAAA NA SIASA ZA VIJANA WACHUMIA TUMBOOOOO
 

Kushughulika nao kivipi? Au ndio mnataka mkawangoe kucha ili mje mseme Magaidi?
 
hahahaaaa, wapi papaa Bensaanane na mamaa Josephine ? majuzi mlikuwa biiize kumsemgenya kamanda wa ukweli akiwa mafunzoni JKT. Haya sasa kiboko yenu amerudi kama mna ubavu jitokezeni hahahaa

UNAFIKI mbaya sana w, umekuja kupima upepo au sio, Utawakamata wengine lakin sio sisi ambao tumezaliwa, tumekua, na kuishi jeshini, Tuna roho butu, Tumekomaa tafakari na ujasiri kabla hata ya umri wetu, Sipati tabu na wanafiki kama ninyi kwani nina somo tosha juu yenu.

Go 2 hell.........!
 
Last edited by a moderator:
Ni wewe wasema

Mama Josephine,

Kama wewe ndiye mke wa Dr. Slaa, nakushauri usiwe una-comment humu, especially kwa masuala yanayomhusu mzee au CDM. Ndiyo, ni haki yako lakini at times nafikiri unafanya kazi ya Daktari inakuwa ngumu sana. You will do more to support the cause by watching from a distance than trying to defend your husband in this forum. I am just saying. I maybe wrong.
 

Mtela Mwampamba katoa ya moyoni mimi nimesema kila siku Zitto ni mnafiki na nilimuomba Mungu siku ifike kama ya leo
nimeokota hii kwenye mtandao na mods musitoe kama Zitto alivyoleta uzi acheni na ya MTela tuyafahamu
NINAVYOMFAHAMU ZITTO ZUBER KABWE - KILIO CHA USALITI (Sehemu ya Tatu)
Nianze na Nukuu ya Kauli ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Chama Makini (CCM) Ndugu Nape Moses Nnauye, Kama ifuatavyo:-
..."..UKIWA MNAFIKI UJANANI, UZEENI UTAKUWA MCHAWI..."

Ninayo nyongeza ya maneno yangu binafsi katika nukuu hiyo, niseme kuwa "Tayari wapo watu wameshakuwa na kukithiri katika Uchawi UJANANI, ni shaka yangu ninapojiuliza UZEENI watakuwa "NANI"
Jina Langu ni MTELA ALLAM MWAMPAMBA mwanachama mchanga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ninayesoma na kujifunza Ilani, Sera, Miongozo, Kanuni na Taratibu za Chama Changu, Ninajifunza katika maandiko ya Chama na najifunza kwa Viongozi wangu kutoka katika Kauli zao, Maelekezo yao na Utashi wao katika Utendaji wao makini unaokisaidia Chama katika kukabiliana na Changamoto mbalimbali kinazokumbana nazo. Najifunza misingi ya kuimarisha na Kukijenga Chama Changu hiki kwa kujitoa kwa dhati ya Moyo wangu na Michango ya Fikra zangu huru.
KABLA ya kuwa mwanachama wa CCM, niliwahi kuwa mwanachama na kiongozi ndani ya Chadema, nikishirikiana kwa karibu zaidi katika Ujenzi wa Chama hiko katika hatua mbalimbali kama nilivyowahi kubainisha katika baadhi ya maandiko yangu.

Kwa anayenifahamu na kuifahamu Chadema na Viongozi wake atakubaliana na ukweli kuwa MIMI, MTELA MWAMPAMBA nilikuwa karibu zaidi na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe.
Masaa machache yaliyopita katika Forum maarufu ya mitandao ya kijamii hapa nchini, Jamiiforums maarufu kama JF, Mhe. Zitto kwa ID yake ambayo ni verified ameandika Thread yenye kichwa cha habari: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/424280-siri-ya-kuuwawa-zitto-uwongo.html


ambapo katika taarifa hiyo ameigawanya sehemu nne:-
i) Ameanza na Ukanusho katika sehemu ya kwanza, akikana kumtambua BEN SAANANE.
ii) Sehemu ya pili ameelezea IMANI yake kubwa kwa DR SLAA, na kudai kuwa SLAA hana sababu ya kumdhuru yeye.
iii) SEHEMU YA TATU akatoa USHAURI na ANGALIZO kwa wale WALIOHAMA chama hiko ( akiwanasibisha na yanayoendelea Chadema Hivi sasa) kuacha kujihusisha ama kukiongelea Chama hiko.
iv) Sehemu ya nne ametoa ushauri kwa Viongozi wenzake wa Chadema kuwa na mshikamano ndani ya Chama hiko.

Nikiwa ni Mwanachama wa CCM, nimeapa kwa Imani ya Chama Changu kuwa NITASEMA KWELI DAIMA NA FITINA KWANGU MWIKO. Kiapo hiki ni ndani ya Chama Changu, Serikali yangu na mbele ya Jamii yangu.

Kwa kuwa LENGO langu si KUFITINISHA wala KUJIHUSISHA NA CHAMA CHAKE, Nitabainisha (kwa Ufupi) namna ninavyomfahamu ZITTO ZUBER KABWE, tena ikibidi nitabainisha kinagaubaga na wazi wazi (kama italazimu kufanya Hivyo) kiasi Umma ubaini ni nani ZITTO ZUBER KABWE ndani ya Chama mjenzi, nguzo, mhimili ama mhujumu chama. Nafanya hivyo kwa lengo la kutetea maslahi ya Kitaifa, maana watu hawa wanabeba nembo na sura ya Utaifa, na ni ubaya ulioje watu wasio na DHATI ya kiutawala kuaminiwa katika Utawala.

Na kwa bahati mbaya katika taarifa hiyo nimetajwa tena kwa jina langu kamili, hivyo jukumu la kunyoosha maelezo ya ZITTO ni la msingi na lenye msukumo Binafsi (Si chama Changu kwa namna yeyote)

Ni kwa msukumo huo ninajikuta ninao wajibu wa kuwabainishia UMMA juu ya mambo hayo manne ambayo ZITTO ameyasema.(Kwa maana sitaeleza lini na wapi nimekutana na ZITTO.,sitaeleza tunafahamiana kiasi gani na tuliwahi kupanga lipi na wapi, sitasema tulifanikiwa mangapi na kushindwa mangapi, sitaeleza "sura halisi" ya ZITTO ninayoifahamu mimi kuliko mtu yeyote mwingine katika Chadema (ILA NASISITIZA KUWA NITAFANYA HIVYO TU PALE ITAKAPOBIDI)

Kwanza, nimeipitia kwa Umakini Mkubwa Taarifa hiyo ya ZITTO na kushuhudia UNAFIKI MKUBWA, UPOTOSHAJI NA UONGO ULIOKITHIRI KATIKA BAADHI YA VIPENGELE NA KUJIKOMBA KUSIKO NA HATA CHEMBE YA AIBU WALA SONI kwa mwandishi wa Taarifa ile.

i) SEHEMU HII YA KWANZA:
Nakubaliana kabisa na Zitto kuwa hakukuwa na kikao ambacho kilitukutanisha Sisi Wanne pamoja, pale LUNCH TIME,hayo ni ya mwandishi mwenyewe, maana Mimi si chanzo chake. Lakini hiyo hainamaanishi kwamba sisi hatukuwa tukikutana na kujadili Mambo juu ya Chama Chetu na Maisha kwa Ujumla wake.

Nimesema sitalieleza hili kwa Undani lakini ukweli uko wazi kuwa taarifa ya SUMU ni ya kweli, na tulikutana na ZITTO nyumbani kwa Kaka yake wa kuzaliwa anayeitwa SALUM OSIBISA pale mkabala na ADA ESTATE Kinondoni, baada ya tukio hilo la SUMU na mjadala wetu uliishia kwa maazimio ya kutokwenda polisi ama kwenye vyombo vya dola kwani kufanya hivyo kungekiharibia CHAMA, lakini kwa hofu ya kushitakiwa na kutaka kujilinda (Defensive Mechanism) BEN alimtuma

EXAUD MAMUYA kuja na habari Hapa JF kuwa ZITTO anakihujumu Chama, habari ambayo ZITTO aliikanusha kwa maneno Makali, ambayo hata leo yameendelea kunukuliwa katika maandiko na comments mbalimbali kuwa ametokea kigoma na ikitokea kifo chake kimehusiana na mtu basi mtu huyo kwao hakutobaki kitu.

Zitto anatambua ni barua ngapi alizoziandika kwa kamati kuu ya Chadema kumshitaki BEN SAANANE na kutaka Kamati kuu imtake BEN athibitishe uongo anaousema juu ya Zitto mitandaoni.

ZITTO na viongozi wengine wanajua nini kimesemwa kuhusiana na Sakata letu ndani ya Kamati Kuu iliyopita na Jinsi hoja hiyo ilivyosababisha Kikao hiko kutahamaki pindi mwenyekiti alipoizima, lakini anafahamu kuwa Kikao Cha Kamati Kuu ijayo kitamjadili yeye (ZITTO) na SHIBUDA na BEN ni miongoni mwa watu watakao toa Ushuhuda wa aliyoyatenda ZITTO katika CHADEMA na anayoyasema yeye BEN katika mitandao ya Kijamii.
Kama pamoja na yote ambayo yaliyopita na yanayoendelea CHADEMA hadi hivi sasa bado yupo anayeamini maneno ya ZITTO kuwa hamfahamu BEN SAANANE na kuwa anaweza kupishana nae njiani bila kumtambua na aendelee kuamini hivyo lakini nasema hiyo ni too much of exaggeration on his expressions.


ii) SEHEMU YA PILI:
Nimesema kuwa sitaki kuizungumzia Chadema kiundani, and that fact holds some basic arguments ambazo nataka kuzitoa, ila wakati mwingine hata machache katika maneno yenye ukweli na uhalisia watu hujifunza kwayo na huwaongezea utambuzi, nitasema hata machache tu, katika mgogoro mkubwa unaokitingisha Chama hicho hivi sasa, SEHEMU HII YA PILI ambayo ZITTO ameileza kipropaganda zaidi na Unafiki mkubwa ambao unalenga kujikomba kusiko na Chembe ya haya, aibu wala soni.

Sikuwa nimeamini mapema niliposoma kipengele hiki "Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo." Kwa maana yote yanayoendelea Chadema yanatokana na Mvutano na Kadhia ya CHUKI na VISASI baina ya Makatibu wawili wa Chama hiko, hata kuondoka kwangu na wengine ni kafara ya jambo hilo. Kuna mambo si sahihi kuyaeleza kiundani na hadharani kwasababu tuliambizana na kupanga kwa Usiri na Kuaminiana, hatujafikia hatua hiyo ya kuuvunja hata Uamini tuliopeana kwa Viapo ila kama tutaendelea na maneno ya namna hii na UZANDIKI, ipo siku tutayasema. Kwa kuanzia, Leo nitaweka hapa moja ya Nukuu ya meseji za JOSEPHINE MUSHUMBUSI ya tarehe 22-07-2012 (nikiwa bado mwanachadema) kubainisha Gogoro lililopo baina ya ZITTO na SLAA&MBOWE kama ifuatavyo.

"..nimekusoma uko kigoma kukusanya kadi za chadema, eti zito anapingwa kuwa Rais. Mbona mnatumia nguvu nyingi sana na mikakati iliyovunda! Zito akitaka Urais amuombe Mungu aingie kwenye mioyo ya watanzania siyo Uganga wa Kienyeji, hata wewe ukitaka uenyekiti wa Bavicha behave well. Hakuna Uganga wala uchawi utasimama leo na kesho, mungu anaona mioyo yenu. Hila hazina nafasi jamani kama ulivyo mkakati wenu jaribuni CHAUMA otherwise, si mungu nnayemjua. Naandika haya kuwatambulisha tu upuuzi wote mnaopanga naufahamu. Msijione wajanja saaaana. NA ROHO WANGU MT kama mwalimu wangu ataendelea kunifunulia..''

Meseji hii ilikuja tukiwa Kigoma na ZITO kwenye Uzinduzi wa Leka Dutigite, ninazo zenye maneno makali zaidi na hata kauli za Slaa, lakini hii inatoa highlight kiasi.



iii) SEHEMU YA TATU:
Nikiwa miongoni wa waliohama Chadema napokea Ushauri wako wa kuacha kuizungumzia CHADEMA, lakini ingependeza pia ikiwa nanyi mtaacha kuwazungumzia wale waliohama.
Kimsingi Ushauri wako huu nimeanza kuufanyia kazi kwenye post hii, wa kuacha kuongelea Mengi kuhusu Chadema na Viongozi wake pia.
L
akini naomba nikushauri kutokana na maneno yako uliyoyaandika leo katika kipengele hiki cha tatu kuwa tusitumie jina lako kufanikisha malengo yetu kisiasa,ni maneno yanayoudhi na kutoka katika misingi ya kulindana. Ni wazi kuwa tumehojiwa katika vikao kadhaa ndani ya Chadema na kote hakuna ambako tulitaja jina lako wala kukuhusisha na chochote kuhusu sisi. Usijiachie sana katika mazungumzo yako, wakati mwingine neno huweza kuzaa yale usiyoyatarajia.

Karata yako ya mwisho inayo-determine maisha yako kama mwanachadema iko mikononi mwetu, Please brother, Don't mess with your last poker chip, u will lose the game.
Kauli yangu Moja ya Ushuhuda inamaliza Uhai wako ndani ya Chadema., I know you are smart brother, don't get crossed., straighten your words..!
Kuwa makini, THIS IS SERIOUS…!
iv) SEHEMU YA NNE.


Katika kipengele hiki, nipongeze kwa dhati ushauri huu wa kuwataka viongozi wa Chadema kuacha Fitna, Majungu, Uongo na Uzandiki. Ningependa kuona kuwa kunakuwa na Upinzani Imara hapa nchini ili Chama Changu Cha CCM kiimarike zaidi,lakini si upinzani wa kupinga kila jambo, upinzani wa mkumbo na uongozi wa ki-imla, si upinzani wa kutohoji na kutoruhusu mawazo na mitizamo huru,si upinzani wa kuchochea vurugu, vitendo vya uvunjifu wa amani na kudhuru watu, si upinzani wa kutukana Viongozi wa Chama Tawala na Serikali, Si Upinzani wa kutamani KUONA NCHI HAITAWALIKI…!
T
unataka upinzani makini unaosimamiwa na watu walio makini na kwa mtazamo wangu (ambao ninao tangu awali na haujabadilika) Wewe ZITTO unao uwezo, maadili na nidhamu ya kuweza kusimamia Upinzani huo. (nayasema haya kwa kuwa nawajua viongozi wenu)


Mwisho kabisa katika signature yako ya JF umetumia nukuu ya Mwalimu Nyerere kwenye kitabu chake cha TUJISAHIHISHE cha mwaka 1962 mwaka mmoja baada ya Uhuru, kuwa UKWELI haupendi kupuuzwa puuzwa, soma tena kitabu hicho upate hazina ya mawazo ya kiutawala na uondokane na UNAFSI kwa tafsir ya Mwalimu Nyerere ya neon hilo katika kitabu hicho.
 
Ahsante kwa kujitokeza na kwa kuwa mkweli. Its true kwamba WEWE NI JEMBE LA UKWELI. Pole kwa yale mazoezi ya KAMBINI-NAELEWA UTAKUWA UMECHOKA SANA BUT UKAONA SI VYEMA KUENDELEA KKULALIA GODOLO ULILOLIMISI, UKAJIKAZA NA KUJA JAMVINI KUUANIKA UKWELI DHIDI YA WANAFIKI WANAOTAKA CHADEMA IFE.
CHADEMA HAIFI KWA UNAFIKI WENU MNAOLALA NJAA HUKU MKITUMIWA KUISHABIKIA CCM BILA KUJUA KWAMBA MNALALA NJAA.
MTAKUFA MASKINI NA LI-CCM LENU LILILOJICHOKEA.
 

Hasikii huyo tumemwambia na kumwambia nadhani tunahitaji kumjua vizuri kuna tatizo anaona nini kukaa na kusoma tuu
 
Funguka kijana mwisho wa siku mtajitaja tu taratibu hahahaha mwelekeo sawia.
 
Zitto, we kamanda na kichwa. nimekukubali songa mbele kamanda. Umewapa ushauri wa bure kama hawatautumia hasara ni yao hao vijana wadogo kiumri na kisiasa. Pia Clous FM - Kibanda na Gerad mlikuwa mnaheshimiwa na jamii sasa Clous FM ilikuwa redio ya watu lakini kwa mwelekeo huu nadhani mmiliki inabidi aangalie upya sera ya kampuni yake na weledi wa wafanyakazi hawa.
 
Yani imefikia hatua nikiona kile kipindi cha maisha ni nyumba tbc1, nazima tv au nabadili channel, sababu ya mtangazaji Kibonde.

Siku hizi kuna rafiki yetu Mashauri kwahy mkuu wewe angalia tu
 

Kaka Mtenda mabaya hutendwa the Zitto era has gone for ever ,hili linabebwa na mitandao yote watu tumeprint kama copy 200 kuzisambaza wamjue head wa masalia ,no more the great Zitto, kila kitu peupe Mtela Mwampamba kamvua nguo na kumuweka barabarani ameconfirm yale tulikuwa tunasema pole Zitto ulidhani kuwachanja chale za matakoni wangenyamaza kwisha dhambi za zitto ni nyingi Arusha kawafanya watu wanapigwa nyanya mpaka leo kwa kuwasaliti udiwani wakati yeye alikuwa anawakazania wasikubali ushauri
 
kama utarudi kusoma waraka wa kwanza wa juliana kuhusu hili sakata la kuwekeana sumu,utakuta kwamba siku wakiwa hapo hotelini wanakunywa zito hakuwepo,na huyo ben alikua akitaka sana wakutane na zito ,ila haikuwezekana.Na wakati mwapamba akikiokota kile kipakiti na kukimbia nacho na huyo ben inadaiwa akamfuata hadi kwake.utaona kuwa maandiko ya mwanzo yanatofautiana na kilichoandikwa na mtanzania.

Huu ndio wakati wa kujua kama habari hii ni ya ukweli ama vipi.
Hawa watu,ben,juliana,mwapamba inatakiwa wahojiwe na vyombo vya usalama haraka ili kuondoa hiki kiwingu.
 
Naomba tutofautiane, mi naamini kama Zitto ataendelea kuwa karibuna wenzake na kuendelea kukitetea chama chake dhidi ya propaganda za nje mtela na shonza hawana nguvu ya kumtingisha, hawa watu credibility yao imeshuka sana na soon chochote watakachokuwa wanaongea kitachukuliwa kama waropokaji tu na vijana walioshindwa siasa na wanatafuta mtu wa kuanguka nae.

shonza na mtela wamejimaliza wenyewe kwa sababu spidi waliyokwenda nayo ilikuwa kali mno na ndo maana hata ukifuatilia kwenye mitandao yote asilimia 90 ya
wachangiaji wapo kinyume nao.
 
Last edited by a moderator:
Kauli kama hizi zisizo na kupulizia upepo kidonda ndio tunazitaka... Hongera kwa maelezo yako na ombi langu kwenu CDM na wanasiasa vijana achane siasa za kizamani za fitina na kuchafuana ni siasa za magumashi na watoto wa vijiweni wanaoganga njaa.. Take politics as proffessional na mtuonyeshe tofauti..
Hivi hakuna maadili ya kuwa mwanasiasa au kiongozi maana hawa wanasiasa wengi vijana wanafuata upuuzi ule ule uliofanywa na wachwara na vilaza wa siasa, sioni tofauti... wa siasa za maji taka..

Waone kama akina Nape na Kaka yake Mgulu na Hao vyanzo vya habari Mwampamba, Lukosi, Shoziii.. aibuuu wako kwenye chama kikubwa barani afrika na chenye historia na misingi ya maana but the way they talk, their action, hawaitendei haki CCM. U should learn from senior CCM leader and ur own our brother Zitto, simsifii ila kwa hili na kusimamia anachokiamini amewacha mbali sanaa.

Hawa watu tusipowambia ukweli tutakuja kupata viongozi wanazi na vilaza sanaa baadaye maana system yetu ilivyo usishangae siku moja ukasikia kati ya hawa wachumia tumbo wamepewa uongozi serikali.. Na ndio maana vijana vilaza wachumia tumbo wanaingia kwenye vyama vya upinzani ili wapate umaarufu utakao wasidia kuhongwa nafasi za uchumia tumbo CCM... hAWA SIO WANASIASA NI VIBARAKA.. WASHAONA DILI MJINI AJIRA NGUMU NA WANATAKA WASUKUME VOGUE NA MAGARI MAZURI MAZURIII..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…