Nani atatungoza sasa? manake wote waliobaki mara utasikia wanamiliki makasino, mara utasikia wameasi kanisa na kukaa na vimada. JK kaza mwendo achana na hawa walevi na wazinzi
Mkuu Mamaisara, Dah??.. Hapa ndipo naposhindwa kuelewa yaani tuko radhi kuendelea na maisha ya tabu, mfumo mzima usioeleweka,
-
Elimu duni-aliyemaliza darasa la saba asiyejua kuandika wala kusoma(sijui walew alio acha shule, kufeli, kurudia),
majengo bila waalimu, wanafunzi wa elimu ya juu kuhangaikia mikopo kwa gharama, lakini hata kucheleweshewa
kama desturi.
-Huduma za
Afya mbovu -Vifaa vya kutendea kazi, madawa, vitanda, wataalamu wachache.
-
Kilimo cha jembe la mkono,
-Wana
Usalama (Polisi, n.k) kuhatarisha Usalama wa walewale wanaowalinda'
-
Hali ya Ndani ya Nchi ikiwa haina amani. lakini nje ya nchi tujlikane ni kisiwa cha "amani"
-
Viwanda vilivyokufa, badala ya kufufuliwa na wananchi kuajiriwa hata kama ni kwa ujira mdogo kwa kuanzia,
-
Madini ingawa Tanzanite hupatikana nchini tu, duniani kote, bado tunakuwa ni nchi ya nne katika uuzaji wake, achilia
mbali madini mengi kwenda nje.
-
Biashara-Wananchi wasio na uwezo mkubwa, kunyanyaswa, Ushuru mkubwa.
-
Utalii-Wanyama kutoroshwa kwenda nje nasisi kufumbia macho, Nchi yenye kuwepo katika maajabu ya dunia lakini
kushindwa kuendeleza na kutangaza hata hili.
-
Usafirishaji,Bandari-rushwa iliyojaa kila kona?
-
Nishati-Kuwepo kwa Mabwawa, maporomoko, ma-Ziwa, Gesi, Makaa ya mawe, Vyura wa Kihansi, Upepo n.k lakini bado Nchi kukosa umeme, na wanao upata yaani chini ya asilimia asilimia(40%) ni kwa mashaka..lini miaka mitatu
mfululizo uliwahi kupata umeme wa uhakika?
-
Miundombinu-Barabara zisizo fikika muda wote, isipokuwa wakati wa kampeni wakihitaji kura.
-
Ajira na Kazi:Vijana lukuki wanaomaliza elimu yao ya juu na kukosa kazi, kwa vigezo vya kutokuwa na uzoefu na hivyo
wazee kubaki makazini hata kamamuda wa kustaafu umeshazidi, huongezewa mkataba, badala ya kuwaajiri
vijana ili moja wapate huo uzoefu, pili kuanza kulipa deni la mkopo alilokopeshwa nahivyokupunguza mzigo
kwa serikali, na kusaidia katika kusomesha vijana wengine, na mwisho vijana ndio population kubwa nchini,
projection ya miaka 15-20 ijayosijui kama wazee walio makazini watakuwa bado wako kazini-Hivyo Taifa
kuwana Watumishi wengi wasio na uzoefu-AMBAO WANGEUPATA SASA!
-
Utawala bora-Usiotaka kujali wale walio waweka madarakani, wenye kuachia wizi, ubadhirifu unaothibitika kila leo na
kuwaacha kuwa viongozi.
Mkuu,haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kubadilika, ila uko radhi KUENDELEA na haya Simply bse ya WOGA wa kutaka kujaribu kitu kipya, ..kusema kwamba wana makasino, ukasisi n.k..
Believe me Mkuu, this is the reason why there are no heroes in the world because at the end of the day people envy them, wait for them to screw up..!!
Kwangu mimi kiongozi haijalishi ana mapungufu gani as long as anaweza kujaribu kufikisha watu mahali fulani, my point is (kuna mapungufu yanayobebeka..mfano mzuri ni wa hayo uliyoyataja.)