Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,451
- 16,337
Siku moja baada ya kifo cha mfanyabiashara wa madini, Marwa Masese (45) na mwanaye, John Marwa (28), dada wa marehemu, Grace Marwa amesimulia mkasa huo akidai kuwa mdogo wake alisaini mkataba wa Sh 2 bilioni na alikuwa anasubiri fedha iingie benki.
Marehemu hao, wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wanadaiwa kuuawa na marafiki zao mkoani Ruvuma walikokwenda kwa shughuli za kibiashara.
Akisimulia mkasa huo kando mwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO), Grace alidai kuwa kaka yake alikuwa ametoka kununua dhahabu Mbeya, kwenye gari alikuwa na mali nyingine nyingi na fedha taslimu.
Alidai kuwa baada ya kuuawa, watuhumiwa walitoroka.
Grace alisema wameitambua miili ya ndugu zao na wameona walivyoumizwa lakini wanasubiri uchunguzi wa daktari.
Alisema wakikabidhiwa miili hiyo wataamua kama watapata nafasi ya ndege waisafirishe kesho kwenda Dar es Salaam na wakikosa watasafirisha kwa magari.
Grace alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwa familia kwa sababu marehemu ni mdogo wake anayemfuata, alikuwa msaada mkubwa kwake na juzi walikuwa waende India kwenye matibabu yeye na mwanaye na walishakata tiketi za ndege kwa ajili ya safari hiyo.
“Nimeumizwa sana na hili tukio, ni baya na linaumiza sana, sina cha kusema ila nawashukuru Jeshi la Polisi, wametusaidia na wameonyesha uaminifu mkubwa,” alisema Grace.
“Kabla ya kuuawa, aliniambia ameshasaini mkataba wa Sh 2 bilioni na alikuwa anasubiri pesa zake ziingie benki na tayari alishanunua hisa.
“Nimeumia kumpoteza mdogo wangu na mwanaye, najua wameuawa kikatili ila Mungu atawalipia,” alisema Grace.
Mwanamke huyo alisema kabla ya Marwa kukumbwa na mkasa huo, alikuwa akiwasiliana naye kila siku, lakini baadaye alipompigia simu, haikupatikana.
Alisema anawashukuru polisi kwa kuwapatia mkufu wa dhahabu wa marehemu wenye thamani ya Sh3 milioni waliouokota ndani ya gari lake.
(Imeandikwa na Joyce Joliga).
Mwananchi.