Sipo hapa kuitetea CHADEMA - Baregu

Sipo hapa kuitetea CHADEMA - Baregu

mkigoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
1,180
Reaction score
309
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, ame s ema baada ya kuteuliwa kwenye nafasi ya ujumbe wa tume hiyo, alikula kiapo cha kutetea masilahi ya Watanzania si ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Prof. Baregu aliyasema hayo juzi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia jijini Mbeya wakati akifungua Baraza la Katiba jijini humo na kuongeza kuwa, huo ndio mwanzo wa mgogoro uliokuwepo kati yake na viongozi wa CHADEMA.

"Wote mliofika katika baraza hili, mmeheshimiwa sana na Watanzania wenzenu waliowatuma mbebe mawazo yao ili yawekwe kwenye Katiba Mpya ambayo itadumu zaidi yamiaka 100...nawaomba msitetee masilahi ya vyama vyenu bali ya Taifa," alisema Prof. Baregu.

Aliongeza kuwa, mbali ya kuwa mjumbe katika tume hiyo pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA ambapo wakati fulani kulikuwa na sintofahamu kati yake na viongozi wake.

Alisema CHADEMA walimtaka afike kwenye Kamati Kuu lakini aliwagomea kwa sababu alitambua alichokuwa akikifanya, kilikuwa kwa manufaa ya Watanzania si chama chake.
p"Mimi sikuapa kuitetea CHADEMA hata kama ni kada wake bali niliapa kuitetea Tanzania na wananachi wake, vyama vya siasa vinaweza kufa lakini Tanzania haiwezi, itaendelea kuwepo milele hivyo lazima tuheshimu hilo," alisema.

Prof. Baregu alisema kwa kutambua umuhimu wa vyama vya siasa kupewa nafasi na tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba, ilitoa nafasi kwa vyama hivyo kuunda Mabaraza ya Katiba, kukusanya maoni yao na kuyapeleta kwenye tume.Alisema fursa hiyo ndiyo inayoweza kutumiwa na vyama hivyo kutetea masilahi ya vyama si kwenye mabaraza ya wananchi.

"Vyama vya siasa vina nafasi yao ya kuunda Mabaraza ya Katiba na kujadili kwa mfumo ambao wataona unafaa, haya mabaraza tuwaachie wawakilishi wa wananchi ambao ndio ninyi.

"Hata katika tume, kuna wakati tulikuwa tukitofautiana mawazo lakini tunafikia muafaka kwa mfano, mimi ni muumini wa Serikali moja lakini nimewaletea rasimu yenye Serikali tatu," alisema.

Maelezo hayo ya Prof. Baregu, yaliwafanya wajumbe waliotoka CCM katika mabaraza hayo, kumpongeza kwa busara zake za kutanguliza uzalendo na masilahi ya Taifa. CHADEMA kilitangaza kujitoa katika mchakato wa mabadiliko ya katiba na kudai mchakato huo umetekwa na CCM na kudai wajumbe wa tume hiyo hawana weledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.

Kutokana na hali hiyo, chama hicho kilidai hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba Mpya hivyo kilimtaka Prof. Baregu ajitoke kwenye tume ili chama kianzishe kampeni nchi nzima ya kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo.
 
Goooood.
Na wadau wengine kwenye tume fuateni huo mtazamo.
 
kuna watakao kuja kumponda. Subiri tuone
 
natamani na wajumbe wengine wafatw nyayo ingawa mleta mada umeleta kinafiki..
 
Yuko sahihi,na ni mfano mzuri kwa wana CCM wengine kuacha kutetea chama hasa kipindi hiki cha kutengeneza katiba mpya,mimi naamini Prof anatoa somo zuri sana kwenye vyama vyetu hivi kuwa mwananchi kwanza na chama baadae,kama CDM nao wana mambo yao ambayo hayamsaidii mwananchi hakuna haja ya kuyaendeleza wala kuyatetea kwenye katiba mpya.
 
Source majira?

Prof mwesiga Baregu ameigomea kamati kuu ya chadema na kuiambia kwamba hayupo kwenye tume kwa ajili ya kutetea maslahi ya Chadema bali ya Watnzania. Soma majira.
 
Ngoja waje akina Baba V na wenzie uone comments za buku8 sasa.
 
Last edited by a moderator:
Prof mwesiga Baregu ameigomea kamati kuu ya chadema na kuiambia kwamba hayupo kwenye tume kwa ajili ya kutetea maslahi ya Chadema bali ya Watnzania. Soma majira.
ameigomea kufanya nini?
 
Good News Mwesigwa kua wa mfano katiba ni ya vyama vyote ni ya watanzania wote tuweke mzani sawa kwa wote na wengine igeni warioba haupo kwa ajili ya ccm tengenezeni katiba itakayo fatwa na vyama vyote tunahitaji katiba ya namna hii. Nape upo hapo acheni kuwa presurise wana tume wafanye kazi yao. Serikali tatu ndia maoni ya wanainchi kwa mujibu wa tume kubalini.
 
Hawa ndo watu makini wanaojua wajibu wao kwa watanzania ni fundisho kwa vyama vyote watu wao wajue kuwa hawako katika sehemu za kuwatumikia watanzania kwa minajili ya vyama vyao ama watu waliowateua.
 
Prof yupo sahihi. Na sio vizuri kuitetea CDM. Ameteuliwa kuandaa katiba ya JMT na sio ya CDM. Wajumbe wengine nao ingekua vizuri kama wangejitambua kama prof!!
 
ni mfano wa kuigwa, sioni tatzo kwenye hlo
 
Baada ya kuona CCM wameuteka nyara mchakato wa katiba mzee Butiku alisema kuwa angejuwa kuwa CCM wataingilia mchakato wa katiba asingekubali kuwemo kwenye tume ya katiba.Baregu na Butiku wamedhihirisha kuwa wako kwa ajili ya kufanya kile ambacho wametumwa na wananchi na hawako kwa ajili ya kufuata matakwa ya vyama.
 
Prof mwesiga Baregu ameigomea kamati kuu ya chadema na kuiambia kwamba hayupo kwenye tume kwa ajili ya kutetea maslahi ya Chadema bali ya Watnzania. Soma majira.

Kwa wale ambao hawatasoma gazeti hii ndiyo habari kamili ya Prof. Baregu:
Amesema CHADEMA walimtaka afike kwenye Kamati kuu lakini aliwagomea kwa sababu alitambua alichokuwa akikifanya, kilikuwa kwa manufaa ya watanzania si chama chake. "Mimi skuapa kuitetea CHADEMA hata kama ni kada wake bali niliapa kuitetea Tanzania na wananchi wake, vyama vya siasa vinaweza kufa lakini Tanzania haiwezi , itaendelea kuwepo milele hivyo lazima tuheshimu hilo." alisema Prof Baregu. Baregu aliongeza kuwa yeye ni muumini wa serikali moja.
 
Back
Top Bottom