Sipo hapa kuitetea CHADEMA - Baregu

Sipo hapa kuitetea CHADEMA - Baregu

He is a free man to believe on what he thinks right to him.
 
kitu kitakacho wamaliza chadema ni kukosa uzalendo ktk ambition zao.hili ni neno la pili kumsikia beregu akienda agaist waziwazi na chadema especialy dr slaa.
tutasikia mengi.na yawezekana hata ziara za chadema kwa ajili ya mabaraza hakubaliani nayo kwa sababu yamekaa kishabiki wa chama na wala si kiutaifa.
mkuu hivi kati ya ccm na chadema nani amekosa uzalendo?
 
Binafsi nampongeza kwa kuwa mzalendo, tunaomba na wajumbe kutoka vyama vingine waje watoe msimamo wao wa wazi!
 
umesoma gazeti la majira lakini?

Nimelisoma!!

Amesema CDM walimtaka afike kwenye kamati akakataa. Lakini hakusema walimuitia nini .................... Mbona Salim anahudhuria vikao vya chama kama kawaida?? Au kuna sheria inayomkataza mjumbe wa Tume ya katiba kuhudhuria vikao vya chama chake?? Maana Salim ambaye ni makamu kwenye tume amechaguliwa kwenye Kamati kuu ya CCM akiwa tayari ni mjumbe wa timu. Sasa akihudhuria vikao vya CCM ina maana anafanya hivyo kwa vile yupo pale kuitetea CCM??
 
Prof. Baregu ni mtu makini. Umakini wake unatokana na kuishi na watu makini. Umakini wa Viongozi wa CHADEMA ndiyo uliosababisha akawa kada wa CHADEMA. Uzalendo wa Prof. Baregu ni uzalendo wa Taifa na unatokana na CHADEMA. Ndiyo maana hata baada ya kutofautiana hawakugombana kwa sababu CHADEMA ni chama MAKINI. Wanachama wa CHADEMA hutofautiana kimtazamo na kimawazo lakini huwa na maamuzi ya PAMOJA. Tofauti bila ugomvi hujenga kuliko kauli za NDIYOOOOOOO walizozoea wenzetu. Asante sana. Ni mtazamo tu.
 
Baregu ni jembe, hawezi kugeuzwa geuzwa na baadhi ya wanasiasa wenye husda na amani ya nchii
 
yuko sahihi, cha msingi wote walioteuliwa wafanye hii kazi kwa weledi tu, wajiepushe na misukumo toka pande zozote hata kama na wao ni sehemu ya jamii fulani; ndo hasa tunachokitegemea kwa wote waliomo ndani ya hiyo tume bila kujali makundi wanayoyakilisha ama watakayoyawakilisha!

kuwa upande wa chama aimaanisha wote mtakuwa mnafikilia kitu kimoja lazma kuwe na mawazo tofauti ndo maana hayo tunayaona yakitokea big up prof
 
prof ana mawazo ya kisomi zaidi na cku zote kama umfahamu waeza kuona kama yupo against nao laa sha!!! ila ana mtazamo unaotofautiana na cdm ndo hicho tu!!!
 
Nadhani viongozi wa CHADEMA walijaribu kutingisha kiberiti wakakuta kimejaa njiti.

Tanzania imebakiwa na wanasiasa wachache sana wanaofanya kazi kulingana na Sheria, kanuni, miiko na misingi ya kazi zao.

Prof. Baregu alionyesha kama ni mmoja wa wanasiasa hao.

Aliyasema hayo kwa sababu watu wamepelekwa kwenye mabaraza hayo kusimamia mawazo ya 'Chama' hata kama hawakubaliani nayo. Ulikuwa wakati mwafaka kuwaonyesha msimamo aliokuwa nao. Kwa furaha wanapompongeza kwa msimamo huo na natumai pia iliwasaidia wao kujitambua...
 
Huyu mzee ni mtanzania wa kweli na mfano wa kuigwa katika siasa zetu za bongo. Ana msimamo wa kipekee kama kamanda Zitto. Pigeni kazi waheshimiwa tuijenge tanzania yetu.
 
Last edited by a moderator:
Aliyasema hayo kwa sababu watu wamepelekwa kwenye mabaraza hayo kusimamia mawazo ya 'Chama' hata kama hawakubaliani nayo. Ulikuwa wakati mwafaka kuwaonyesha msimamo aliokuwa nao. Kwa furaha wanapompongeza kwa msimamo huo na natumai pia iliwasaidia wao kujitambua...
Yes. Huo ndiyo ulikuwa ujumbe wake kwa wajumbe wa baraza la katiba na kikubwa zaidi, alitaka wamuone kama yuko kama wao na wafanye maamuzi kwa misingi na mitazamo ya kitaifa kama yeye alivyofanya wakati wa kuandika rasimu ya katiba pamoja na kwamba wanatofautiana kiitikadi na kimtazo na baadhi ya wajumbe wengine wa tume ya Jaji Warioba.
 
[🙂kama kauli hii ni kweli na sio kuwatega wenzake ili wajiachie baas itakuwa heli kwa utaifa kwanza.

Prof. Baregu aliyasema hayo juzi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia jijini Mbeya wakati akifungua Baraza la Katiba jijini humo na kuongeza kuwa, huo ndio mwanzo wa mgogoro uliokuwepo kati yake na viongozi wa CHADEMA.

"Wote mliofika katika baraza hili, mmeheshimiwa sana na Watanzania wenzenu waliowatuma mbebe mawazo yao ili yawekwe kwenye Katiba Mpya ambayo itadumu zaidi yamiaka 100...nawaomba msitetee masilahi ya vyama vyenu bali ya Taifa," alisema Prof. Baregu.

Aliongeza kuwa, mbali ya kuwa mjumbe katika tume hiyo pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA ambapo wakati fulani kulikuwa na sintofahamu kati yake na viongozi wake.

Alisema CHADEMA walimtaka afike kwenye Kamati Kuu lakini aliwagomea kwa sababu alitambua alichokuwa akikifanya, kilikuwa kwa manufaa ya Watanzania si chama chake.
p"Mimi sikuapa kuitetea CHADEMA hata kama ni kada wake bali niliapa kuitetea Tanzania na wananachi wake, vyama vya siasa vinaweza kufa lakini Tanzania haiwezi, itaendelea kuwepo milele hivyo lazima tuheshimu hilo," alisema.

Prof. Baregu alisema kwa kutambua umuhimu wa vyama vya siasa kupewa nafasi na tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba, ilitoa nafasi kwa vyama hivyo kuunda Mabaraza ya Katiba, kukusanya maoni yao na kuyapeleta kwenye tume.Alisema fursa hiyo ndiyo inayoweza kutumiwa na vyama hivyo kutetea masilahi ya vyama si kwenye mabaraza ya wananchi.

"Vyama vya siasa vina nafasi yao ya kuunda Mabaraza ya Katiba na kujadili kwa mfumo ambao wataona unafaa, haya mabaraza tuwaachie wawakilishi wa wananchi ambao ndio ninyi.

"Hata katika tume, kuna wakati tulikuwa tukitofautiana mawazo lakini tunafikia muafaka kwa mfano, mimi ni muumini wa Serikali moja lakini nimewaletea rasimu yenye Serikali tatu," alisema.

Maelezo hayo ya Prof. Baregu, yaliwafanya wajumbe waliotoka CCM katika mabaraza hayo, kumpongeza kwa busara zake za kutanguliza uzalendo na masilahi ya Taifa. CHADEMA kilitangaza kujitoa katika mchakato wa mabadiliko ya katiba na kudai mchakato huo umetekwa na CCM na kudai wajumbe wa tume hiyo hawana weledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.

Kutokana na hali hiyo, chama hicho kilidai hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba Mpya hivyo kilimtaka Prof. Baregu ajitoke kwenye tume ili chama kianzishe kampeni nchi nzima ya kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo.[/QUOTE]
 
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, ame s ema baada ya kuteuliwa kwenye nafasi ya ujumbe wa tume hiyo, alikula kiapo cha kutetea masilahi ya Watanzania si ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Prof. Baregu aliyasema hayo juzi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia jijini Mbeya wakati akifungua Baraza la Katiba jijini humo na kuongeza kuwa, huo ndio mwanzo wa mgogoro uliokuwepo kati yake na viongozi wa CHADEMA.

"Wote mliofika katika baraza hili, mmeheshimiwa sana na Watanzania wenzenu waliowatuma mbebe mawazo yao ili yawekwe kwenye Katiba Mpya ambayo itadumu zaidi yamiaka 100...nawaomba msitetee masilahi ya vyama vyenu bali ya Taifa," alisema Prof. Baregu.

Aliongeza kuwa, mbali ya kuwa mjumbe katika tume hiyo pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA ambapo wakati fulani kulikuwa na sintofahamu kati yake na viongozi wake.

Alisema CHADEMA walimtaka afike kwenye Kamati Kuu lakini aliwagomea kwa sababu alitambua alichokuwa akikifanya, kilikuwa kwa manufaa ya Watanzania si chama chake.
p"Mimi sikuapa kuitetea CHADEMA hata kama ni kada wake bali niliapa kuitetea Tanzania na wananachi wake, vyama vya siasa vinaweza kufa lakini Tanzania haiwezi, itaendelea kuwepo milele hivyo lazima tuheshimu hilo," alisema.

Prof. Baregu alisema kwa kutambua umuhimu wa vyama vya siasa kupewa nafasi na tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba, ilitoa nafasi kwa vyama hivyo kuunda Mabaraza ya Katiba, kukusanya maoni yao na kuyapeleta kwenye tume.Alisema fursa hiyo ndiyo inayoweza kutumiwa na vyama hivyo kutetea masilahi ya vyama si kwenye mabaraza ya wananchi.

"Vyama vya siasa vina nafasi yao ya kuunda Mabaraza ya Katiba na kujadili kwa mfumo ambao wataona unafaa, haya mabaraza tuwaachie wawakilishi wa wananchi ambao ndio ninyi.

"Hata katika tume, kuna wakati tulikuwa tukitofautiana mawazo lakini tunafikia muafaka kwa mfano, mimi ni muumini wa Serikali moja lakini nimewaletea rasimu yenye Serikali tatu," alisema.

Maelezo hayo ya Prof. Baregu, yaliwafanya wajumbe waliotoka CCM katika mabaraza hayo, kumpongeza kwa busara zake za kutanguliza uzalendo na masilahi ya Taifa. CHADEMA kilitangaza kujitoa katika mchakato wa mabadiliko ya katiba na kudai mchakato huo umetekwa na CCM na kudai wajumbe wa tume hiyo hawana weledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.

Kutokana na hali hiyo, chama hicho kilidai hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba Mpya hivyo kilimtaka Prof. Baregu ajitoke kwenye tume ili chama kianzishe kampeni nchi nzima ya kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo.
Prof. Baregu, akiwa mjumbe wa CC hakupaswa kuijibu Chadema kupitia vyombo vya habari, na hata kama Chadema walimuita kwenye CC, hawakukosea kumuita walimuita mjumbe wa chombo husika

Kutokukubali wito na kuja kutangaza dhumuni la kuitiwa ni unafki, maana ya Demokrasia ni uhuru wa kujieleza alishindwa nini kwenda kujieleza na kutoa maoni yake mbele ya wajumbe wa CC??

Sasa tangu alipoitwa na kukataa na kwenda kinyume na kanuni za ki uongozi Chadema imepungukiwa nini?? Sana sana mengi ambayo Chadema inayapigania ndiyo yale yale yaliyorudishwa kwenye rasimu ya tume

Na zaidi yameleta mkanganyiko huko CCM

Prof. Baregu ikitokea kesho kikafanyika kikao kingine cha CC na usipewe taarifa kama inavyotokea kwa Shibuda kutopewa taarifa za M4C, utalalamika??

Utakuja kusema Chadema kuna ubaguzi, si ndiyo?? Naamini Chadema kuna ubaguzi, ila ni ubaguzi wa busara, huwezi kushirikishwa jambo kama huna busara za kutosha

Samahani mzee wangu

CHADEMA FOR NATION
 
sawa msimamo mzuri ningependa wajumbe wote wawe hivyo ili tupate katiba bora ili tuifukuze ccm madarakani.
 
tangu mwanzo nilimuona Baregu anatetea tumbo lake tu.Cdm walikuwa na msimamo unaoeleweka.yeye yuko pale kwa ajili ya cdm na alitakiwa kupeleka msimamo wa chama na si wake binafsi.ndiyo maana wajumbe wametoka ktk taasisi tofauti ili kuwasilisha misimamo na matakwa yao.kutoka moyoni sijawahi kumuamini Baregu tangu nimfahamu
 
Mkuu. Tatizo kuna watu wanaangalia mambo kiushabiki sana bila mantiki, Chadema kuna mambo ya msingi sana tunayaunga mkono kwenye rasimu ya katiba ambayo mwenyekiti wake ni Warioba. haimaanishi kuwa kwa kuwa tunayaunga mkono basi tunamuunga mkono Warioba kwenye kila kitu na hiyo haimaanishi kuwa kwa kuwa kuna mambo tunayaunga mkono kutoka kwa Warioba basi tunaunga mkono ccm kwa kuwa Warioba ni kada wa ccm. Kinyume chake kwa Baregu.

Hayo ni mawazo yako mgando endelea kumezeshwa hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom