Sipo hapa kuitetea CHADEMA - Baregu

Sipo hapa kuitetea CHADEMA - Baregu

Prof mwesiga Baregu ameigomea kamati kuu ya chadema na kuiambia kwamba hayupo kwenye tume kwa ajili ya kutetea maslahi ya Chadema bali ya Watnzania. Soma majira.

Hapa ndipo tunaweza kutofautisha kati ya Mwanasiasa msomi na yule asiye na shule. Hongera mzee Baregu
 
kwa kweli kitendo anachokionyesha prof ni cha kizalendo. husifuate hao wanafiki. hongela sana prof
 
Kuna jambo la kujifunza kwenye habari hii:
1. CHADEMA kumbe wanatetea maslahi yao binafsi, na tunaposema maslahi yao tuna maana ya viongozi wa CHADEMA kwa sababu wangekuwa wanatetea na wafuaasi wao wote, basi Baregu angeitikia witowa kuitwa kwenye Kamati kuu kwa vile naye ni mmoja wa wale ambao angenufaika na wito huo, lakini kwa kutambua kuwa kuitwa kwake kulikuwa ni kwa ajili ya wachache akaona mbali;
2. Kwa nini Baregu anasema yeye ni muumini wa serikali moja wakati CHAMA chake kimezunguka nchi zima kutafuta maoni juu ya rasimu ya katiba mpya, bali kuhubiri serikali tatu? Yawezekana kabisa mikakati hii serikali tatu ndani ya CDM ilianza hata kabla ya kuundwa kwa kamati ya Katiba lakini mzee wa watu akaa nalo moyoni kwa vile hakuwa na pa kulisemea. Ni dhahiri kabisa kauli ya BAREGU inalenga kuimarisha muungano wakati harakati za CDM kutumia nguvu nyingi sana kunadi serikali tatu inalenga kuuvunja muungano jambo ambalo linadhihirishwa na kauli mbalimbali za makada wa CDM mfano LISSU alivyosema juzi kuwa CUF ni chma cha WAZANZIBARI.
 
Yap, na watu kama hawa wanawafungua macho wale wanakuwa waumini wa vyama vya siasa bila kujua malengo mabaya ya viongozi wa vyama hivyo dhidi ya Taifa.
 
kuna watakao kuja kumponda. Subiri tuone

Mkuu kama watu wanamuunga mkono KAGAME unategemea waache kumponda Prof. Baregu japo ameonesha uzalendo mkubwa na kumwaumbua hawa Ma-liberary
 
Kwa iyo lile lory la maoni halina kazi tena duu baregu noma
 
Mtu akifanya jambo jema hapana budi kupongezwa, safi sana Baregu na hongereni sana CCM kwa kumpongeza Kada CDM kwa hilo kwani ninyi ni wakomavu wa demokrasia.
 
Kama hujaelewa kalale boya wewe...

Sasa haya ni majibu gani kwa mtu anayetaka kujua? Hili jukwaa lina baadhi ya watu ambao ni extemely hopeless.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Japo sijasoma hilo gazeti naunga mkono kichwa cha habari.

Mimi ni mwanaCdm halisi inatakiwa kuweka Utaifa mbele hivyo hata wajumbe wa ccm na cuf waige mfano wa Prof. Baregu.

U-ccm.........NO,NO,BIG NOOOO
U-CDM.........NO
U-CUF...........NO
U-TLP& OTHERS............NO

U-TAIFA....YEEEEESSSSSSSSS
 
Kwa wale ambao hawatasoma gazeti hii ndiyo habari kamili ya Prof. Baregu:
Amesema CHADEMA walimtaka afike kwenye Kamati kuu lakini aliwagomea kwa sababu alitambua alichokuwa akikifanya, kilikuwa kwa manufaa ya watanzania si chama chake. "Mimi skuapa kuitetea CHADEMA hata kama ni kada wake bali niliapa kuitetea Tanzania na wananchi wake, vyama vya siasa vinaweza kufa lakini Tanzania haiwezi , itaendelea kuwepo milele hivyo lazima tuheshimu hilo." alisema Prof Baregu. Baregu aliongeza kuwa yeye ni muumini wa serikali moja.
Kwani tatizo liko wapi hapa?katiba ni ya watanzania na wala si ya vyama,by the way hii habari ni kiporo majira wamekipasha moto maana bila kuitaja Chadema hawatauza kamwe vijarida vyao!!!
 
>Wana chadema kwa ujumla wanamuunga mkono profesa Baregu kwa msimamo huo... Maslahi ya Taifa kwanza ya chama baadae.... TUKO NYUMA YAKO PROFESA KWA KUWA UMEONYESHA TOFAUTI YA WAJUMBE WA CCM NA WA CHADEMA...
KWENYE HIYO TUME, FANYA KAZI PROFESA..
 
Kuna jambo la kujifunza kwenye habari hii:
1. CHADEMA kumbe wanatetea maslahi yao binafsi, na tunaposema maslahi yao tuna maana ya viongozi wa CHADEMA kwa sababu wangekuwa wanatetea na wafuaasi wao wote, basi Baregu angeitikia witowa kuitwa kwenye Kamati kuu kwa vile naye ni mmoja wa wale ambao angenufaika na wito huo, lakini kwa kutambua kuwa kuitwa kwake kulikuwa ni kwa ajili ya wachache akaona mbali;
2. Kwa nini Baregu anasema yeye ni muumini wa serikali moja wakati CHAMA chake kimezunguka nchi zima kutafuta maoni juu ya rasimu ya katiba mpya, bali kuhubiri serikali tatu? Yawezekana kabisa mikakati hii serikali tatu ndani ya CDM ilianza hata kabla ya kuundwa kwa kamati ya Katiba lakini mzee wa watu akaa nalo moyoni kwa vile hakuwa na pa kulisemea. Ni dhahiri kabisa kauli ya BAREGU inalenga kuimarisha muungano wakati harakati za CDM kutumia nguvu nyingi sana kunadi serikali tatu inalenga kuuvunja muungano jambo ambalo linadhihirishwa na kauli mbalimbali za makada wa CDM mfano LISSU alivyosema juzi kuwa CUF ni chma cha WAZANZIBARI.

Kitu cha kujifunza ni kwamba CHADEMA ni chama ambacho kinathamini maoni ya kila mtu kutokana na haki ya kikatiba ambayo kila mtu amepewa uhuru wa kutoa maoni yake pasipokuingiliwa na mtu yeyote ndiyo maana Baregu hajaingiliwa na chama chake kwa kuwa ni muumini wa serekali 1 na chama chake ni muumini wa serekali 3.Tume ya katiba iliyoteuliwa na wananchi ambayo imepokea maoni ya sekali 1,2 au 3 ndiyo itakayoamuwa.
 
Sasa haya ni majibu gani kwa mtu anayetaka kujua? Hili jukwaa lina baadhi ya watu ambao ni extemely hopeless.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

>Siku hizi hata vichaa wameingia humu mkuu.. Wanaacha kukaa kule facebook wanakimbilia huku kwenye fikra pevu, na wao hawana fikra pevu..
 
Mkuu kama watu wanamuunga mkono KAGAME unategemea waache kumponda Prof. Baregu japo ameonesha uzalendo mkubwa na kumwaumbua hawa Ma-liberary
Makubwa hapa kwenye akili za samaki,hapo kwenye red=cuf!!Kumbe magamba yanajua Baregu yupo kafu?
 
Kitu cha kujifunza ni kwamba CHADEMA ni chama ambacho kinathamini maoni ya kila mtu kutokana na haki ya kikatiba ambayo kila mtu amepewa uhuru wa kutoa maoni yake pasipokuingiliwa na mtu yeyote ndiyo maana Baregu hajaingiliwa na chama chake kwa kuwa ni muumini wa serekali 1 na chama chake ni muumini wa serekali 3.Tume ya katiba iliyoteuliwa na wananchi ambayo imepokea maoni ya sekali 1,2 au 3 ndiyo itakayoamuwa.

>Umejuaje kama Baregu ni muumini wa serikali moja?
 
tunataka watu kama baregu kama ukiona chama chako kinaleta mauzauza kama chadema lazima kupingana nao na ikibidi ni kuwakemea kama shetani.
 
Kitu cha kujifunza ni kwamba CHADEMA ni chama ambacho kinathamini maoni ya kila mtu kutokana na haki ya kikatiba ambayo kila mtu amepewa uhuru wa kutoa maoni yake pasipokuingiliwa na mtu yeyote ndiyo maana Baregu hajaingiliwa na chama chake kwa kuwa ni muumini wa serekali 1 na chama chake ni muumini wa serekali 3.Tume ya katiba iliyoteuliwa na wananchi ambayo imepokea maoni ya sekali 1,2 au 3 ndiyo itakayoamuwa.

Waeleze hao wanaoshindwa kusoma na kuanalise. Kwanza hii kitu kilitokea mwaka jana wakati CDM walipotishia kujito kwenye mchakato na ikajadiliwa sana humu. Mleta thread kachukua kasentence kamoja na kuafanya kama vile DCM wanataka kumshinikiza awe pale kwa manufaa yao.

Hakuna mahali au siku ambayo tumesikia kuwa CDM wanataka hivyo. Hata Warioba aliwahi kuwaonya CCM na hii alijadiliwa hapa.
 
Back
Top Bottom