Sipendi kulala guest;

Sipendi kulala guest;

wana forum, nina week moja sasa hapa jijini dodoma, kuna mafunzo flani hivi yanafanyika hapa milembe hospitali.

changamoto ni sehemu ya kulala wakuu, nimezungukia guest za hapa karibu nimeonyeshwa vyumba vyao ,

mmmmmmh, kweli ni wachafu ! bei zao sasa ndo utachoka elfu 20 per dai.

nikapata nyingine ambayo ni angalu wana jitahidi usafi kwa shilingi elfu 30.

asalaleeeeeee kuingia ndani hakuna maji , huduma mbovu,

daaaaaah. kwa mazingira haya sitaki kulala tena guest.

Ombi; nyie mnao miliki haya ma guest house himizeni wafanyakazi wenu kuwa wasafi hata kwa kiwango cha kokoto.

asante.

MIMI
Pole, kuna lodge na hotel, nenda hizo kisha uje utupe mrejesho kaka.
 
asante sana kaka; ngoja nizitafute hizo ulizo niambia;

nimelala pale Top ***** elfu 30 .bafuni hakuna maji ikanilazimu kuoga maji ya kopo lita moja na nusu.

kidogo niwambie nirudishieni hela zangu si kwa ushenzi huu;
Usijali kaka. Mimi mwenyewe Dom nimeshapata shida sana. Sasa hivi nacall tu nakuta chumba.
20181021_161939.jpg

NB: Jamaa hawauzi chakula. Wanatoa BF tu. Chakula ni hadi utoke au wamtume kijana akuletee. Labda hawajawa na wateja wengi ili kuanzisha restaurant.
 
Hapana mkuu, nie ni mkazi wa dar, ila nipo kwenye civil construction kwa miaka 20 sasa. Dodoma nimejenga MSD Warehouses kule kizota 2012-2013. Tangu hapo nimekuwa nikija dom kwa vipindi tofauti, haswa kunapokuwa na mikutano ya kada yetu kwenye ukumbi wa kikwete.
Karbu next time mi mwenyewe mtt wa kada hapo makao makuu
 
Dodoma hovyo kabisa kwenye Guest House au Lodge Yaani unaonyeshwa room ya 20k au 25k utachoka mwenyewe.Hata breakfast hakuna ni kulala tuu.Maji utaletewa kwenye Ndoo (anachemsha pembeni huko)
Guest ya 20-25 then iwe na Breakfast?
 
nimetembea sehemu nyingi ila Dom kwa lodge ni number moja! sema km Mgeni hujui maeneo unaweza vagaa lodge za ajabu ajabu! sasa maeneo km mirembe usitegemee kupata lodge nzr
 
Wewe unatafuta lodge za bei ndogo unategemea nini?

Wahenga walishanena bure aghali
Lodge aliyofikia ni zile za zamani na nyingi zipo jirani na mjini kati. Lodge hizo ni bei poa hivyo kwa vile vikao vyao vipo hapo Mirembe basi yeye yupo sehemu za Hazina, Soko Kuu au Mji Mpya. Jaribu kwenda nje kidogo ya mji barabara ya kuelekea Dar. Ila kwa huduma nzuri afungue pochi. Ama kweli bure aghali.
 
wana forum, nina week moja sasa hapa jijini dodoma, kuna mafunzo flani hivi yanafanyika hapa milembe hospitali.

changamoto ni sehemu ya kulala wakuu, nimezungukia guest za hapa karibu nimeonyeshwa vyumba vyao ,

mmmmmmh, kweli ni wachafu ! bei zao sasa ndo utachoka elfu 20 per dai.

nikapata nyingine ambayo ni angalu wana jitahidi usafi kwa shilingi elfu 30.

asalaleeeeeee kuingia ndani hakuna maji , huduma mbovu,

daaaaaah. kwa mazingira haya sitaki kulala tena guest.

Ombi; nyie mnao miliki haya ma guest house himizeni wafanyakazi wenu kuwa wasafi hata kwa kiwango cha kokoto.

asante.

MIMI
Kuna mahema madogo unayoweza kubeba mkononi na sleeping, hili ni blangeti lenye zipu, sasa ukiwa navyo hivi viwili hauhitani gesti. Ukifika unapokwenda unatafuta mahali salama kama kituo kikuu cha mabasi, stesheni ya treni au sokoni, unasimamisha hema lako unaingia ndani ya blangeti lako mambo poa.
 
Kuna kitu nimejifunza kwenye uzi huu, wengi huwa tunasafiri tukiwa hatujafanya maandalizi ya kule tunapokwenda, bahati mbaya website ambazo ndio zingekuwa chanzo cha taarifa, zinaishia kutoa offer to treaty ikiwa ni picha, huduma zinazopatikana, location na mara chache bei ya huduma hizo.mimi nafikiri kitu kikubwa kilikuwa ni mawasiliano ili kutengeneza contract katika mfumo wa booking na vitu kama hivyo. Nipendekeze kwa hosts wa website hizi (eg Tripadvisor , Jovago etc kufania kazi maboresho haya.
 
Nkiskia dodoma nakumbuka mbal sana..natoka udsm kufata papuch dom wikend,daaah,.maisha ya chuo matam sana,ndomana nna gpa ndogo *****
Sasa wewe nawe yaani unaacha papuchi UDSM unazifungia safari Dodoma!! Mbona UDSM zipo nyingi sana hapo tena za kuokota bure tu.
 
Acha unafiki, Kwa tanzania hii ukiondoa Mwanza, Dar na Moro sehem yenye guest house nzur na safi ni Dom tena za bei nafuu. Nenda Nkuhungu karibu na four ways Ingia Ulanga vyumba 20k+ bf. Au jirani ipo nyingine wanaita Rhino to mention few.
Usidanganye watu moja ya sehemu zenye guest ghali dodoma mojawapo halafu guest zenyewe chafu hazina ubora
 
Kwa Dodoma mie nilikwenda 2018 nikawakubali sana Suma Lodge. Yaani niliwakubali sana tu. Ila sijui kwa sasa 2020 kama bado wako vizuri vilevile.

Ila kuna mgesti mmoja m-bovu sana uko karibu na Police Central ndo bodaboda alinipeleka usiku usiku huo kama saa sita hivi ndo nimewasili, yaani walinikera maana walichukua hela yangu reception kwanza halafu ndo wakanipeleka chumbani. Godoro jembaba kama chapati yaani chaga unazisikia. Halafu eti maji ya kuogea kwenye ndoo. Tukagombana sana wakagoma kurudisha hela yangu. Nikaondoka usiku huo huo nikaanza kutembea kwa mguu barabarani sijui hata naenda wapi. Ndo nikakutana na bodaboda mwingine nikamwelezea tatizo langu akaniambia ngoja nikupeleke Guest nzuri. Akanipeleka Suma Lodge.

Aisee nilifurahi sana kwa mambo niliyoyakuta Suma Lodge. Bei poa (ilikuwa Tshs. 15,000/- tu, chumba kisafi na maji ya moto ya kwenye shower. Halafu asubuhi unapewa na chai ya watu wawili ya maziwa, mkate mmoja mzima wa silesi, mayai ya kukaanga, na unakaa kwenye kibaraza fulani kizuri unakunywa chai huku unapigwa na upepo.

Kwa nje inaonekana namna hii

Suma Lodge, Geti.jpg

Na hapo ndo kibarazani asubuhi ukiwa unakunywa chai inapendeza sana

View attachment 1537672
 
View attachment 1537669

@KAJOKELAA
 
Lipia tangazo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom