"Sipati mke wa kuoa"Part 1

"Sipati mke wa kuoa"Part 1

Mm namiliki biskel yangu ya laki 2, na naishi kwenye chumba cha kupanga kodi 50k per month na maisha yanaendelea kama kawaida na wala sihofii kuonekana mjinga au boya Fulani!! Binafsi huwa siendeshwi na fikra za watu huwa naishi the way ninavyotaka mm na sio watu wengine wanataka haijalishi nina pesa au sina pesa, mwanamke ambaye atakubali kuwa na mm basi ajiandaye kukabiliana na hali yangu, kuwa na magar au nyumba ni Mwenyezi Mungu ndo apangaye muda ukifika wa kumiliki hizo basi nitamiliki na kama imepangwa kuwa nitamiliki kimoja wapo basi naimani nitamiliki.
Maisha ya kujionyesha wakati mwingine yanacost, unaweza ukanunua gari halafu huna uwezo wa kutunza hilo gari, maana gari linaitaji mafuta ya kutosha, linahitaji service Mara kwa Mara, ?wengine wapo mjini wanatembea na magari lakini ikitokea hitilafu kidogo hawajui waanzie wapi wamalizie wap sometimes unakuta mtu anaweza kuita fundi kwa kitu ambacho ni kidogo sana ambacho kama lahiti angekuwa na elimu kidogo ya gari angeweza kutatua mwenyewe!!

Wengine wenye magari waliojaa mjini ni waendesha magari yaani hawa sio madereva kamili, na hawa ndo wanaongoza kupata na kusababisha ajari, yaani gari halimalizi hata mwezi kutoka kununuliwa lakini unakuta limeshabanjuliwa....

Anyway wanaume wenzangu naelewa kila mtu anamatamanio yake lakini haya matamanio yasiwe chanzo cha kukufanya ww ukose amani, jiamini na ujikubali kwa ulichonacho, kupata mke mwema sio kazi maana ukimtegemea sana muumba wako utapata mke bora na wala asiyekuwa na mawazo madogo kama unavyofikiria wewe, cha msingi nikusali au kuswali sana na kuwa na imani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom