"Sipati mke wa kuoa"Part 1

"Sipati mke wa kuoa"Part 1

brenda18

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
5,687
Reaction score
5,300
For a while nimekuwa nikisikia na kuona wakaka wengi, especially wale ambao wanataka kuoa wakilalamika "nina gari, nina nyumba, kazi nzuri, hela etc. But sipati mke wa kuoa".

Yani hiyo statement huwa inanipa a series of unanswered questions. Najua hiyo type na humu ndani wapo kibao. Siwatukani ila najiuliza tu, hivi mnavyowazaga hivyo huwa mnakuwa kwenye akili zenu timamu au? Tangu lini gari likaoa mke, unataka mke au unataka dereva/abiria?

Una nyumba..so what exactly are you looking for; a tenant, a house keeper or what? Aliyewaambia kwamba kuwa na gari, kazi na nyumba ndo kigezo tosha cha kuoa ni nani?

Hivi hukai hukajiuliza mbona nina hivyo vyote but huu ni mwaka wa 3, 4, 5 natafuta "mke" na Sijapata? Kuna tatizo gani? Ungekuwa umekaa kwa kina ukajiuliza hivyo basi naamini akili yako ingekuwa imefunguka hata kidogo.

Apart from nyumba, kazi, gari.. what else can you offer?. Kama hivyo ndo vingekuwa the only vigezo, basi kila mwenye navyo angekuwa ameoa warembo wa kutosha sana tu. Hivyo mnavyoviona ndo vigezo tosha, baadhi yetu tunaviona kama "bonus" tu kwa mwanaume anayejitambua.

Mnatiana tu ujinga humu, Tafuta pesa, utang'oa mademu wa kila aina....kweli yes utang'oa mademu wasiojitambua, sio wanawake wenye akili zao timamu unless una extra things to offer. Kila mtu anapenda pesa/gari, lakini sio kila mtu anashobokea pesa/gari.

Hivi seriously unampata msichana eti kwa sababu una gari, hivi hii century kuna watu still wanashoboka na magari, unless wana matatizo. Gari ambalo unapewa lift mara moja kwa wiki/ mwezi siku zingine zote unashika bomba, ndo limfanye mtu avue tei tei?

Mtu hana cha maana anachoongea ila kujibrag tu, nina hiki, nina kile mweee yani hapo mwenyewe anaona kashamaliza mchezo. So disgusting, ndo maturity ya mtu anayetaka kuoa huyo pyeee. Huna cha maana cha kukudefine apart from gari na nyumba mmmh.

Usipendwe na mtu, basi ushajistukia "au kisa nina gari" mwee jamaniii. Siku ukimiliki jet si ndo hata humu Ukipewa like utahisi"ashasikia nina jet, ananishobokea" hahahah .....

Part 1
Copied & pasted
a04beb121a85fe6d0064a3470a889a7b.jpg
 
Duh, kwa hiyo mleta mada hutaki pesa, nyumba wala gari siyo?

Watu wa aina yako mmebakia wachache kwenye hii SAYARI
 
Unaweza kunipa hivyo vyote ila nisiwe na furaha, pesa ,nyumba na magari si kila kitu
Furaha ni kitu kingine, immaterial thing huwezi kupima!

Let's stick to material things ambayo ndio msingi wa Thread yako
 
Furaha ni kitu kingine, immaterial thing huwezi kupima!

Let's stick to material things ambayo ndio msingi wa Thread yako
Soma vizuriiii jinsi nilivyorelate matumizi ya material things,kwa sasa naona umechagua cha kuelewa mengine umeyaacha hivyo hupati ninachokimaanisha
 
Unaweza kunipa hivyo vyote ila nisiwe na furaha, pesa ,nyumba na magari si kila kitu
Aise Mungu akujalie uwe na moyo huo besti
upate na mume mzuri
hao wanaotanguliza nyumba pesa na magari basi ndoa zao zitaendeshwa na magari na pesa
umuhimu wa pesa unajulikana lakini isiwe mbadala wa thamani ya mtu ama mbadala wa upendo...
 
Eti pesa...
Kina ruge wamebwagwa huko na mipesa yao atakua nani mwingine ambae atajifanya ana vihela vya kuhonga
 
mwanaume muoaji sio muoaji tu . ukiona mwanamme yupo 35-45 hajawai kuoa jipeleke kwa kunyata sana maana utaumizwa hadi maini .bora udate mzee aliefiwa na mke wa miaka 60-100
Hahaha unachosema ni kweli kabisa
 
Mwanamke umwambie mimi sina kitu unadhani utaambulia nini?
Inategemea ni mwanamke kwa ajili ya nini, kama ni wa kuoa alafu umdanganye hio ndoa haitodumu
Ila kama ni wa kumpitia tu ni sawa we danganya tu wapo wengi utawapata
 
Hahaha unachosema ni kweli kabisa
kwanza hawajui kupenda? yaani ni ngumu sana hata ufanye nini kuwin moyo wake .maana huna chochoter cha kumpa ana uwezo wa kupata chochote.kama ni sex anaweza hata kununua, umri huo uchumi nao unakuwa umestabilize hela anayo yaani ni ngumu sana kumuingia mwanaume wa miaka 35-45
 
Aise Mungu akujalie uwe na moyo huo besti
upate na mume mzuri
hao wanaotanguliza nyumba pesa na magari basi ndoa zao zitaendeshwa na magari na pesa
umuhimu wa pesa unajulikana lakini isiwe mbadala wa thamani ya mtu ama mbadala wa upendo...
Na siku hizo pesa zikiisha ndoa nazo zinaisha,kwakweli kwa sasa mambo yamekuwa magumu kwakweli
 
Soma vizuriiii jinsi nilivyorelate matumizi ya material things,kwa sasa naona umechagua cha kuelewa mengine umeyaacha hivyo hupati ninachokimaanisha
Panga mtiririko wa uzi ueleweke, naona hujafaham nini hasa umelenga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom