Sipandi ndege inayoendeshwa na Mweusi-NJONJO. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sipandi ndege inayoendeshwa na Mweusi-NJONJO.

Discussion in 'International Forum' started by PakaJimmy, Jan 10, 2010.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Charles Njonjo ni Mmoja kati ya waliopata kuwa wanasiasa mashuhuri wa Kenya miaka ya 1960-1980, ambaye pia alipata kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya, akiwa na digrii ya sheria aliyoipata Afrika Kusini.

  Bwana huyu pia alipata kuwa Mbunge na Waziri wa Sheria na katiba katika serikali ya Kenya, na hadi sasa yuko juu sana kwenye list ya Matajiri wanaoongoza Kenya.

  [​IMG]

  Miaka ya 1983 alilazimishwa kujiuzulu akidaiwa kutaka kuipindua serikali halali ya BABA MOI.

  Lakini, mbali ya kuwa kichocheo kikubwa sana cha uvunjifu wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika Mashariki ya mwanzo, kali zaidi inaaminika kuwa huyu ndugu alipata kutoa kauli nyingi sana tata na za dharau kama ifuatavyo:

  "Naona aibu sana kuwa Mkikuyu"

  "Siwezi kabisa kushikana mkono na kusalimiana na mtu wa kabila la Luo"

  "Nahisi kukosa amani na usalama nikipanda ndege inayoendeshwa na Mwafrika"

  Sasa huu sijui ni ulimbikeni au ndo mambo ya akina Nge**leja!

  CHANZO:[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Charles_Njonjo[/ame]
   
 2. M

  Mtuwamungu Senior Member

  #2
  Jan 10, 2010
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "Miaka ya 1983 alilazimishwa kujiuzulu akidaiwa kutaka kuipindua serikali halali ya Mwai Kibaki."

  Usipotoshe wana JF, Kibaki hakuwa rais wa Kenya wakati huo. Rais allikuwa Moi kama chanzo cha habari ulichokiweka mwenyewe kinavyoshuhudia. Kwa hiyo Njonjo alituhumiwa kutaka kumpiku Moi na siyo Kibaki.
   
 3. B

  Big Dady Member

  #3
  Jan 10, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Miaka hiyo Serikali iliyokuwa madarakani ni ya Mzee Moi na sio Kibaki. Baba Moi aliyeimbia wimbo Nakei Nairobi na mwanamziki Mbilia Bel.
   
 4. m

  matambo JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  i think huyu jamaa alikuwa na ile kasumba iwatafunayo wakenya wengi kujihisi wao ni wazungu weusi ilhali ni watumwa wa fikra
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Jamaa alikuwa kibri kwelikweli.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Jan 10, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  No negro dialect
   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 4,016
  Trophy Points: 280
  Kuna uwezekano ikawa lilisema hivyo, sishangai maana ni jinga flani, juzi aliulizwa kuhusu EAC akasema haoni kama inaweza fanya kazi! Alipoulizwa kampuni zake ambazo yeye ni stakeholder (yaani in Insurance and finance) zime-invest in EA, akashindwa kujibu!
   
 8. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sishangai wakikuyu!Wako proud sana,hawaamini kuwa kabila lolota haliwezi kutawala Kenya.Baada ya Uhuru,wakawa kama playground for Brits!Kumbuka Kenyata na huyu Njonjo wakapewa wanawake wazungu!

  Kabila ambalo ni bright Kenya ni Wajaluo!hawana majivuno,watu straight wanapenda shule.tulioenda JKT tuliiimba :Na Tom Mboya wa Kenya huo,ni kiongozi mzuri.....
  Baada ya uhuru Kenyata alijitahidi kuwaianua wakikuyu wenzake ku pata ardhi huko Rift valley kwa akina Moi.

  Mpaka leo haijulikani nani aliwaua Dr Robert Ouko na Tom Mboya wote wajaluo.
  Wakikuyu wana wivu sana kwa wajaluo.Huwezi kuamini rafiki yangu mkikuyu alikuwa hataki Obama awe rais,maana mkikuyu hataki kusikia mjaluo amesucced.
   
 9. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Talking about mtu mweusi kuendesha ndege, mimi nilirudi nyumbani kwa sherehe za Krismasi, nilirudi huku kwenye nchi za baridi mwanzo wa mwaka, ndio theluji inaanza kupamba moto, kwa kutumia ndege ya Kenya Airways. Rubani na wafanyakazi wote ndani ya ndege ni waKenya weusi. Sasa, kufika Amsterdam, watu wote (wazungu kibao) walikuwa roho mkononi kuhofia jinsi ndege itakavyotua uwanjani.

  Kusema kweli, rubani yule alikuwa "professional" sana, akiwataka watu wasitie shaka na akatua ndege salama salmini. Abiria wote walipiga makofi na kushangilia sana, ingekuwa inaruhusiwa kusimama nadhani angepata "standing ovation"...nilisisimka mwili kwa kweli

  Sasa huyu mjinga mwingine anadharau watu wa aina/kabila yake mwenyewe? Kweli utumwa wa fikra
   
 10. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kosa la kifundi hili mzee, (error) usikomae sana!


  Huyu jaama ni wale weusi wenye kasumba ya kutukuza uzungu kuliko asili yao. Wapo wengi sana kama hawa viongozi wetu ambao kila kukicha wapo Marekani na Ulaya. Anakubali kwenda kutalii Jamaica kuliko Serengeti.

  [​IMG]

  President Jakaya Kikwete and his wife, Salma Kikwete and Minister for Tourism in Jamaica, Mr Edmund Bartlett (right) and Chairman of the Mystic mountains conservation, Mr Horace Clarke, touring the hills facing the tourist attractions in St. Ann region, in Jamaica.
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  I am graceful to the Almighty to have lived long enough to see some of the STUPIDIEST AFRICANS, Charles Njonjo is one.
  Tatizo, hawezi kuhamia Uingereza maana bado ana ngozi nyeusi na anatambua fika kuwa atabaguliwa kama najavyojibagua!!
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Error!..u KNOW WHAT, i think faster than i can write..BE RATIONAL FRIEND..We ni mtu wa Mungu eeh?
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  kazi kwelikweli
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Chales njonjo alikuwa ni mwanasheria mkuu na waziri wa sheria kipindi cha Kenyatta na baadae Mzee Daniel Arap Moi.Wakati Mzee Jomo kenyatta anafariki Moi alikuwa ni makamu wa rais lakini hakuwa na nguvu kama Bwana charles njonjo.

  Bwana C Njonjo kwa wadhifa wake wa uanasheria mkuu alihakikisha Moi anapata urais Kenya.Kuna story niliwahi kuhadithia kwamba baba yake Njonjo aliwahi kumuuliza mwanae [C Njonjo] ni kwanini alimsaidia sana Moi kuupata urais badala ya yeye kuwa rais,akamjibu baba yake kamweka Moi kwasababu ni dhaifu sana ili baadae akiutaka urais wa Kenya asiwe na kazi ngumu.Baba yake Njonjo akamwambie mwanae akate kipande cha nyama amtupie paka Njonjo akafanya kama alivyoagizwa na baba yake,baba akamwambie ampokonye paka nyama aliyompa yeye mwenyewe Charles alipomsogelea paka akanguruma na kuidhibiti nyama.Baba yake Njonjo akamwambia mwanae siku akitaka kumwondoa Moi madarakani atakuwa mkali kama paka alivyokuwa mkali bila kujali ni wewe uliyemsaidia/ mpatia madaraka.Bwana Njonjo akatahayari kwa ujinga alioufanya na baadae kweli alipojaribu kumwondoa Mzee Moi aliishiwa kupokonywa vyeo vyote vya kisiasa.
   
 15. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  he was right kwa miaka hiyo south africa ulitarajia aseme nini?hata yeye kupata nafasi ya kwend kusoma huko lazma aponde weusi ndo akubalike!
   
 16. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  You got it twisted son. Its very wrong of you to come here and think you can categorize and stereotype Kikuyus and Luos (Kenyan tribes) of which you know nothing about except what you read and hear from people. just from the name you use in this forum, it easily shows that you are a tribalistic person, how can you gauge the morallity of a person from the tribe he comes from? To me its impossible, there are always exceptions everywhere, and there are always people who try and tarnish the good names of others. Mwambie Pakajimmy akupe sourse ya hiyo upuzi ametuletea hapa, acheni mchezo wakati mwingine.
   
 17. H

  Haruna JM Sauko Member

  #17
  Jan 12, 2010
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 24
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu bwana na miongoni mwa waafrika wenye nyodo kuna wakati nilisoma na kuona picha moja katika gazeti la wakati ule mfanyakazi amevaa suti yenye herufi CN na chini ya picha kulikuwa na maneno yalosema kuwa ilikuwa ikimaanisha Charles Njonjo. hivi sasa anashughulika nini huyu bwana?
  mwenye habari aweke jamvini si vibaya kuwajua viongozi wetu nchi za afrika mashariki
   
 18. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kenya kuna tatizo kubwa sana,yaani jamaa wameathiriwa sana na wamagharibi kifikra.
   
 19. Jammu Africa

  Jammu Africa JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Charles Mugane Njonjo, son of a the late chief Njonjo during colonial times,

  grew up in a very wealthy environment and went to the best schools
  and later got married to a british woman.

  Njonjo and Mwai Kibaki were instrumental to Moi ascending to power
  though he had another hidden agenda of letting Moi go up and then
  overthrow him constitutionally.

  Moi was not as weak as he (Njonjo) thought and saw all his plans.
  He was charged with treason but Moi forgave him later, remembering
  how Njonjo helped him during the change the constitution wave,
  where the Katiba would have been changed and so put a stop on the
  then vice president (Moi) asiwe rais wa mpito mpaka uchanguzi in
  case of the death of the then Mzee Kenyatta.

  Njonjo have had that kind of illusions of being very special and that can
  be the reason why he did not go far politically.

  Over ambitious and misculating all the time.
   
 20. Jammu Africa

  Jammu Africa JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni kweli Njonjo alikua akivaa suti nyeusi yenye
  misitari kama ilivyokua nawenye nguvu hizo siku.

  Lakini katika suti zake, misitari ilikua CN.

  Kama si kiburi na kujisikia kua special, angekua
  mtu mwenye nguvu nana kuheshika hapa Kenya.

  Lakini kiburi kilimtangulia.

  Haya ni masomo kila mtu anafaa kusoma kwamba
  hata kama umefanikiwa, usidharao wenzako.
   
Loading...