Sioni umuhimu wa daraja la Aga Khan - Coco beach kwa sasa

Nakuunga mkopo, una mawazo mazuri sana, kuna maeneo ya muhimu sana yanayohitaji madaraja na sio hilo daraja la Coco Beach, ni white elephant project, na kupoteza pesa za wahisani na walipa kodi!!
 
Mpwa nakafahamu kale ka njia, ule ni uchochoro, hautapunguza foleni popote pale

Basi kale ka uchochoro kana kismat. Kwa sasa kanasaidia sana lucha ya kutokuwepo daraja la coco beach.
 
Kwa macho ya kawaida unaweza kufikiri lengo la daraja hili ni kupunguza foleni ya Salender Bridge na kuwaondolea wananchi wa Dar kero ya foleni. La hasha daraja hili linalojengwa kwa gharama kubwa halitapunguza foleni kwa sababu watakaotumia daraja hili ni watu wachache sana, (under utilised bridge).

Ukiangalia kwa jicho la tatu, lengo hasa ni kuwasaidia viongozi, mabalozi na wazungu wachache wanaoishi maeneo ya Osterbay na Masaki ambao hawazidi hata 200, labda wasikae kwenye foleni kwa muda mrefu wakichanganyika na walalahoi wa maeneo ya Mwenge, Kawe, Kunduchi, Tegeta, Boko na Bunju.

USHAURI: Kama lengo ni kupunguza foleni ya Salender Bridge ingefaa zaidi lijengwe daraja kubwa la nchi kavu kutokea maeneo ya Hananasifu au Magomeni hadi Muhimbili au Fire kuvuka bonde la Jangwani linalojaa maji kipindi cha mvua.

Daraja hili la Hananasifu - Muhimbili/Fire, lingehudumia watu wengi hasa wafanyabiashara na wafanyakazi wa kada mbalimbali ambao ndio walio wengi ukilinganisha na wakazi wa Masaki, tofauti na daraja la Aga Khan - Coco beach ambalo litahudumia watu wachache na pengine kubaki 'idle' kwa kipindi kirefu.

Daraja kubwa la Jangwani si tu lingepunguza adha ya foleni ya Magomeni-Kariakoo/Posta bali pia lingesaidia kupunguza magari yanayopita Salender Bridge.

Anyways kupanga ni kuchagua, tumechagua daraja la Coco beach kwa wadosi tukawaacha wa Mbagala wahangaike na foleni yao.

Ni ushauri na mawazo huru ya MwanaJF mzoefu Quinine.
Mkuu hili daraja la magomeni_fire_mhimbili ni daraja muhimu sana kuliko hata flyover za ubungo..
 
Mkuu kipaumbele chetu kwa sasa ni kuwafanya mabalozi wasikae foleni kwa muda mrefu, daraja la jangwani linalotumiwa na walalahoi likifurika wao wanauwezo wa kusubiri hata wiki maji yapungue ndipo wapite hawana haraka kama mabalozi.
 
Mimi pia nina maoni sawa na mleta mada. Ngoja nipitie hoja za wana jukwaa naweza juzwa nisiyoyajua
 
Kwel ila kuna tofaut ya mpiga kula na msaini mikataba ya watu wa ulaya aspo fannya hivo wanamdai chao ,subili saanne utasikiaa wametusaidia kujenga kumbe wametukopesha halafu mashart jiwe hadi kufa maiti inadaiwa deni la taifa walo sain wakina juhaaaa Mawazo
 
Kwa macho ya kawaida unaweza kufikiri lengo la daraja hili ni kupunguza foleni ya Salender Bridge na kuwaondolea wananchi wa Dar kero ya foleni. La hasha daraja hili linalojengwa kwa gharama kubwa halitapunguza foleni kwa sababu watakaotumia daraja hili ni watu wachache sana, (under utilised bridge).

Ukiangalia kwa jicho la tatu, lengo hasa ni kuwasaidia viongozi, mabalozi na wazungu wachache wanaoishi maeneo ya Osterbay na Masaki ambao hawazidi hata 200, labda wasikae kwenye foleni kwa muda mrefu wakichanganyika na walalahoi wa maeneo ya Mwenge, Kawe, Kunduchi, Tegeta, Boko na Bunju.

USHAURI: Kama lengo ni kupunguza foleni ya Salender Bridge ingefaa zaidi lijengwe daraja kubwa la nchi kavu kutokea maeneo ya Hananasifu au Magomeni hadi Muhimbili au Fire kuvuka bonde la Jangwani linalojaa maji kipindi cha mvua.

Daraja hili la Hananasifu - Muhimbili/Fire, lingehudumia watu wengi hasa wafanyabiashara na wafanyakazi wa kada mbalimbali ambao ndio walio wengi ukilinganisha na wakazi wa Masaki, tofauti na daraja la Aga Khan - Coco beach ambalo litahudumia watu wachache na pengine kubaki 'idle' kwa kipindi kirefu.

Daraja kubwa la Jangwani si tu lingepunguza adha ya foleni ya Magomeni-Kariakoo/Posta bali pia lingesaidia kupunguza magari yanayopita Salender Bridge.

Anyways kupanga ni kuchagua, tumechagua daraja la Coco beach kwa wadosi tukawaacha wa Mbagala wahangaike na foleni yao.

Ni ushauri na mawazo huru ya MwanaJF mzoefu Quinine.
Wazee wa kupinga.
 
Very true..
 
Inapendeza sana mtu anapopinga jambo, akatoa sababu kisha akaleta mapendekezo mbafala, Quinine hongera kwa hilo.

Tukirudi kwenye hoja. Kwa mtazamo wangu, hilo daraja litadaidia kupunguza foleni kwa wakazi wa Mwenge, Kawe, Mbezi, Kunduchi na maeneo yote ya huo ukanda.

Kumbuka kuna barabara imetengenezea kwa kiwango kizuri sana kuanzia pale Mikocheni Tanesco, inakuja kutokezea Msasani, hapo watumiaji wengi watapita cocobeach kuja kutokezea mjini posta.

Lakini kinachonitatiza, bado nasikia wanataka kuipanua barabara ya AlHassan Mwinyi tena, ikiwa ni hivyo, wangeobgeza tu upana wa daraja la zamani magari mengi yapite hapo kwa sababu msongamano unaanzia hapo kwenye daraja.
Kweli daraja litapunguza sana foleni kwa wakazi wa maeneo tajwa. Ingawa naunga mkono kujengwa kwa daraja hilo ila kuna kiukakasi hapo kidogo, je cost ya kujenga daraja hilo ina justify kiasi cha foleni litalopunguza?

Lakini pia, nadhani kuna agenda nyingine ya mandhari ya jiji. Itabadilisha mtazamo wa jiji na kuitambulisha jiji. Maana meli yoyote itakayokuja Dar lazima walione.

Kama ilivyo daraja la Golden Gate la San Francisco. Yaani ukiutaja tu huo mji lazima na hilo daraja lionekane.
images.jpg
 
Umeongea ukweli mtupu ilo daraja litasaidia wakazi zaidi wa masaki,oysterbay ambao sio watz na hata kama watz basi mawaziri na viongozi wakubwa wa serikali.

Hilo daraja ni moja ya "WHITE ELEPHANT" Project za vigogo wa serikalini,wewe unadhani wakubwa wanapata wapi utajiri? Wanaanzisha miradi hewa kibao ya ufisadi na ndani ya hiyo miradi waneweka cha juu cha kufa mtu,imagine bei halisi ya Drimulaina ni usd 100m lakini sie tumenunua kwa 228m USD ina maanisha kuna watu wamepiga zaidi ya 118m usd wameweka mfukoni.

Kupunguza foleni dsm wajenge njia nyingi mbadala,sio ukitaka kwenda mwenge kwenda posta mbananane ali hassan,wajenge njia za Juu kutoka mkwajuni hadi Mwenge,wajenge njia ya juu kutoka Mikocheni viwanda ikatue mbezi beach,wajenge njia ya juu kutoka Magomeni Mtaaa mapipa ikatue Uhasibu,hapo watasaidia wakazi wengi.

Pia waharakishe Mwendo kasi kuijenga,posta to mbagala,posta to Gongo la mboto,Morocco to Mwenge to Bunju....Ilitakiwa waanze na Mwendokasi waachane kwanza na Salenda maana hilo daraja ni Pambo na 50% tu za wakubwa.
 
Hongera sana rais Dr.Magufuli kwa ujenzi wa daraja hilo, tunaomba na Busisi lijengwe daraja ili kutupunguzia maswaibu tunayoyapata sisi wapiga kura wako wenye kura zisizokuwa na mashaka hata kidogo.
 
Kweli daraja litapunguza sana foleni kwa wakazi wa maeneo tajwa. Ingawa naunga mkono kujengwa kwa daraja hilo ila kuna kiukakasi hapo kidogo, je cost ya kujenga daraja hilo ina justify kiasi cha foleni litalopunguza?

Lakini pia, nadhani kuna agenda nyingine ya mandhari ya jiji. Itabadilisha mtazamo wa jiji na kuitambulisha jiji. Maana meli yoyote itakayokuja Dar lazima walione.

Kama ilivyo daraja la Golden Gate la San Francisco. Yaani ukiutaja tu huo mji lazima na hilo daraja lionekane.
View attachment 816320
Mkuu nadhani lengo kuu la kujenga daraja huwa siyo kubadilisha mandhari bali kurahisisha mawasiliano.
 
Umuhimu mnao uona hapo ufipa ni wa biashara ya mwenyekiti wenu tu ( Madawa)
Kuzaliwa tu nchi moja na mwenye akili mdogo kama huyu no laana kubwa. Kweli wazo alilotoa mdau na mapendekezo hapo juu Kwako ukaona hiIo ndio la maana?? Huenda kweli mikesha ya mwenge imeleta kizazi cha hovyo kisichojielewa kama huyu.
 
Back
Top Bottom