Sioni tija yoyote ya matengenezo yanayoendelea barabara ya bagamoyo (Mbezi hadi Tegeta) kufanyika sasa.
Kinachofanyika sasa nakifananisha na uharibifu au fursa ya upigaji!
Kwanza hakuna mpango kazi mzuri kwasababu wanakwangua barabara na kuiacha barabara katika hali mbaya zaidi kwa mda mrefu pasipo kufanya matengenezo.
Pili matengenezo kama hayo ya kukwangua barabara kama yanazidi 1km ni bora wangefumua barabara nzima kuliko kujaza vilaka ambavyo havina msaada!
Nilitegemea katika kipindi hiki cha mpito ambacho nchi inakumbwa na majanga mbalimbali tungejikita kufanya miradi mhimu ya kimkakati kuliko kuja kumwaga pesa sehemu kama ile ambayo hata ingeweza kusubiri kwanza majanga yapungue na pesa tukazielekeza sehemu za lazima.
Bajeti ya kubadilisha lami iliyokuwepo ili kuweka lami mpya si tu ni matumizi mabaya ya rasilimali Bali pia ni matumizi mabaya ya taaluma ya uhandisi!
Tatizo la lami kuwa na mabonde huwezi kulimaliza kwa kubadilisha lami juu juu nakuacha kushughulikia msingi mzima wa barabara kuanzia chini (road base)
Ikumbukwe sehemu ya juu ya lami huwa haibebi mzigo Bali hurahisisha mseleleko, hivyo kama lami mpya itawekwa mahala ambako chini kuna unyevu au hapakushindiliwa vizuri inamaana hata ukiweka mpya itabonyea vilevile!
Kwahiyo kuweka lami au overlaying yoyote kwenye barabara hiyo ni bora zaidi kuiacha ilivyokuwa na pesa zake zikaelekezwa sehemu nyingine korofi zenye mahitaji ya lazima!
Kama kulikuwa na ulazima sana kutumika katika barabara hiyo ni Mara mia wangetanua barabara za pembeni (service road) pale mbuyuni na tegeta
Lakini kwa hiki kinachoendelea kwenye hii barabara kuanzia mbezi hadi tegeta hakina tija kufanyika kwa sasa hususani kipindi ambacho kunatarajiwa kutafanyika tena jenzi/upanuzi wa barabara ya magari ya mwendo kasi katika awamu ijayo!
Kuna haja kubwa sana Tanroad wakajitafakari kwenye barabara hii!