Sioni tija ya ukarabati unaoendelea Barabara ya Bagamoyo (Mbezi - Tegeta)

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Sioni tija yoyote ya matengenezo yanayoendelea barabara ya bagamoyo (Mbezi hadi Tegeta) kufanyika sasa.

Kinachofanyika sasa nakifananisha na uharibifu au fursa ya upigaji!

Kwanza hakuna mpango kazi mzuri kwasababu wanakwangua barabara na kuiacha barabara katika hali mbaya zaidi kwa mda mrefu pasipo kufanya matengenezo.

Pili matengenezo kama hayo ya kukwangua barabara kama yanazidi 1km ni bora wangefumua barabara nzima kuliko kujaza vilaka ambavyo havina msaada!

Nilitegemea katika kipindi hiki cha mpito ambacho nchi inakumbwa na majanga mbalimbali tungejikita kufanya miradi mhimu ya kimkakati kuliko kuja kumwaga pesa sehemu kama ile ambayo hata ingeweza kusubiri kwanza majanga yapungue na pesa tukazielekeza sehemu za lazima.

Bajeti ya kubadilisha lami iliyokuwepo ili kuweka lami mpya si tu ni matumizi mabaya ya rasilimali Bali pia ni matumizi mabaya ya taaluma ya uhandisi!

Tatizo la lami kuwa na mabonde huwezi kulimaliza kwa kubadilisha lami juu juu nakuacha kushughulikia msingi mzima wa barabara kuanzia chini (road base)

Ikumbukwe sehemu ya juu ya lami huwa haibebi mzigo Bali hurahisisha mseleleko, hivyo kama lami mpya itawekwa mahala ambako chini kuna unyevu au hapakushindiliwa vizuri inamaana hata ukiweka mpya itabonyea vilevile!

Kwahiyo kuweka lami au overlaying yoyote kwenye barabara hiyo ni bora zaidi kuiacha ilivyokuwa na pesa zake zikaelekezwa sehemu nyingine korofi zenye mahitaji ya lazima!

Kama kulikuwa na ulazima sana kutumika katika barabara hiyo ni Mara mia wangetanua barabara za pembeni (service road) pale mbuyuni na tegeta

Lakini kwa hiki kinachoendelea kwenye hii barabara kuanzia mbezi hadi tegeta hakina tija kufanyika kwa sasa hususani kipindi ambacho kunatarajiwa kutafanyika tena jenzi/upanuzi wa barabara ya magari ya mwendo kasi katika awamu ijayo!

Kuna haja kubwa sana Tanroad wakajitafakari kwenye barabara hii!
 
Yale mamashine yao yalikaa sana chini bila kazi, sasa awamu imefika ya UREFU WA KAMBA, kuna $1bn inakuja.

Wakiwa na pesa wanajichubua, zikiisha wanarudia rangi yao, lakini iliyoharibika tayari.
 
Ile barabara ifumuliwe yote ndo tabia zao wanachimba wanaacha.

Sema ndo vichaka vya wapiga dili acha wajipimie
 
Ikiachwa bila kukarabatiwa inaharibika zaidi na hapo ndipo itabidi ijengwe upya.

Waafrika hasa watanzania uwa tuna hulka ya kujenga lakini matengenezo uwa haba na ndio maana uwa kila mara tunatudia kufanya jambo lile lile badala ya kuongeza mengine.

Tunafail kwenye kupanga mipango tukiwa na vision ya miaka 50 mbele. Ndio maana unaona kila siku barabara kuu zinarudiwa kujengwa kwasababu wanaopanga wanaona urefu wa pua zao hajiulizi hii barabra baada ya mika 20 ni mizigo na magari kiasi gani yatakayopita.
 
Mwendo kasi ukija tunavunja tena
 
Mwendo kasi ukija tunavunja tena
Kabisa mara nlisikia eti upande mmoja zitapita mwendo kasi upande mwingine gari za kawaida. Sasa si kurudisha foleni. Yanj mipango yetu hatuwazi mbali. Kila siku tunarudia kutengeneza vitu vile vile ndio maa mji haujapangwa. Iwapo dodoma itakua ikawa kama dar aisee kwa ile miundombinu wataanza bomoa bomoa
 
Ishu ipo hivi, kuna jamaa wana hilo limashine lao la kukwangua lami ambalo limekaa bila kazi kwa muda mrefu, na benki nao wanadai pesa, hivyo likaundwantatizo ambalo wala halikuwepo ili mashine ipate kazi, ni upigaji tu.
 
Sema kweli mkuu! Tumepigwa
 
Sasa mkuu kama fungu la fedha limetengwa kwa hiyo barabara isijengwe?
Sio lazima fungu likitengwa litumike!! Ni fedha kama hizi ndizo serikali inatakiwa kuzifanyia reallocation na kuzipeleka kwenye emergency fund ya kudhiniti mfumuko wa bei! Ukifanya hivyo nchi nzima utapata fedha za kutosha!
 
Back
Top Bottom