Nimekuwa nikibishana na watu waliokuwa wakiunganisha Mbowe na ukaribu wake na Familia ya Mtei kuliko uwezo wake binafsi.Mtei alifanya maamuzi ya kama mfanya biashara.Unapoanza biashara unahitaji dedicated people,smart na wasio na njaa za kugombea mafanikio kidogo yanayopatikana njiani.Mbowe wanamjua wapiga Kura wake wa Hai.Huwa ni mtu mwenye msimamo, anaheshimu watu sana, ni jasiri hakuna kipimo.Huwa ni mtu apendaye akitoa msaada ufanye kazi husika.Waliowahi kwepesha wanamjua , naona hata wapenda longo longo wanatamani sana aitwe dictator.
Mbowe amepata majaribu mengi ila hajapoteza integrity yake.Chagangamoto nyingi kama za kuvamiwa na polisi, ulinzi wa Kura etc. Kuna mazingira unaona kabisa angewekwa "mzee wa Liwalo na Liwe".Nadhani tungekuwa sasa hivi kama Syria.Kuna maeneo unaweza ona kabisa kuwa CCM wanapoteza akili na ku push to the limit vurugu zianze,tena vurugu ambazo zikianza kuzimika ni utawala kuondoka.Ila mbowe anameza uamuzi mgumu wa kukabiliana na wanachama wanaotaka atoe ruhusa tuu.
Ukitaka jua Mbowe na timu nzima ya CDM ni wachapa kazi ,angalia uchaguzi uliopita,hawa jamaa walikuwa wakipigana majimbo kadhaa kwa muda huo kuhakikisha kura haziibwi.Jimbo lake la Hai, Arusha,Moshi majimbo kadhaa, wakiwa na Mzee Ndesa.