kupelwa
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 1,087
- 450
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.
Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.
Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa CDM kwa sasa ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka.Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C
Source: Tanzania Daima
aminia kamanda,ni kweli muda huu ni wa kupiga kisomo mpaka kieleweke, chama makini huwafikia wanachama wake na kupata mawasiliano nao kwa kuwaelemisha, kuwasikiliza na kuwaada ili wapokee mabadiliko.CDM ki mstakabali nivyema ikafanya jitihada mbadala za ccm kuwafikia watanzania walio wengi na kuwaada ili wawe mtaji wa kisiasa wakati wa uchaguzi kupata majimbo mengi na hivyo kuleta madailiko bungeni na kuwekez
a kwenye sera nzuri za kuwakomboa watanzania.hoja ya mavyeo madaraka ni ufinyu wa fikra, tunataka mabadiliko na si magenge ya uraisi ambayo ni fikra dhaifu