Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,920
- 870,915
Na pia nimeieleza World Bank jinsi serikali ya awamu ya Tano ilivyodhamiria kuua upinzani kwa nguvu zake zote,kwa hiyo si ajabu hizo pesa zitatumika ktk operesheni Tokomeza upinzani.[emoji117][emoji117][emoji117] [emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
Jr[emoji769]
Mnapoteza muda wenu bure kumwandama Zitto eti kaiandikia World Bank isitishe mkopo wake kwa Tanzania.
Hata sisi pia na mimi nikiwemo na wenzangu wengine wengi pia tumeileza World Bank juu ya uozo wa serikali ya awamu ya Tano juu ya haki za Binadamu, Demokrasia na hali ya kisiasa kwa ujumla Tanzania.
Binafsi nimetuma clip za Video kwa World Bank na kuwataka pia ku prove hizo clip You Tube juu ya matamshi ya Rais kwa Wapinzani, ambayo amekuwa akiyatoa hadharani.
Kwanini serikali inahitaji hiyo pesa karibia na uchaguzi mkuu na siyo baada ya uchaguzi mkuu au kabla?
Jibu li wazi kwamba hiyo pesa inalengwa kutumika kwenye Kampeni.
Nimewaandikia Benk ya Dunia na kuwaeleza wazi kwamba kwa sasa kila kiongozi ana tension na uchaguzi mkuu hasa Rais na Wabunge hasa wa CCM ambako ndo kuna mawaziri.
Nimeikumbusha World Bank juu ya mizengwe ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana jinsi wapinzani walivyonyanyaswa hadi kujitoa kwenye uchaguzi.
Nimeieleza World Bank kuwa Tanzania imeshapata mikopo mingi mno ya Elimu tangu Tupate Uhuru na Rais pekee aliyekuwa akitumia mikopo hiyo vizuri ni Nyerere pekee yake ndo maana ktk utawala wake Elimu ilikuwa bure kweli kweli na siyo bure ya mdomoni Kama tunavyoaminishwa sasa hivi.
Nimeieleza World Bank jinsi watoto wadogo wanavyotembea km zaidi ya 10 kwa siku kwenda shule na bado wakifika darasani hakuna madawati, vitabu na uhaba wa walimu,na kwamba kipaumbele cha serikali ya awamu ya Tano siyo Elimu bali ni ununuzi wa ndege na miradi mikubwa ambayo inazidi uwezo wa nchi kiuchumi.
Na pia nimeieleza World Bank jinsi serikali ya awamu ya Tano ilivyodhamiria kuua upinzani kwa nguvu zake zote,kwa hiyo si ajabu hizo pesa zitatumika ktk operesheni Tokomeza upinzani.
Jr[emoji769]