Sio Zitto pekee yake, hata sisi tumeandika

Sio Zitto pekee yake, hata sisi tumeandika

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,930
Reaction score
13,335
Mnapoteza muda wenu bure kumwandama Zitto eti kaiandikia World Bank isitishe mkopo wake kwa Tanzania.

Hata sisi pia na mimi nikiwemo na wenzangu wengine wengi pia tumeileza World Bank juu ya uozo wa serikali ya awamu ya Tano juu ya haki za Binadamu, Demokrasia na hali ya kisiasa kwa ujumla Tanzania.

Binafsi nimetuma clip za Video kwa World Bank na kuwataka pia ku prove hizo clip You Tube juu ya matamshi ya Rais kwa Wapinzani, ambayo amekuwa akiyatoa hadharani.

Kwanini serikali inahitaji hiyo pesa karibia na uchaguzi mkuu na siyo baada ya uchaguzi mkuu au kabla?

Jibu li wazi kwamba hiyo pesa inalengwa kutumika kwenye Kampeni.

Nimewaandikia Benk ya Dunia na kuwaeleza wazi kwamba kwa sasa kila kiongozi ana tension na uchaguzi mkuu hasa Rais na Wabunge hasa wa CCM ambako ndo kuna mawaziri.

Nimeikumbusha World Bank juu ya mizengwe ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana jinsi wapinzani walivyonyanyaswa hadi kujitoa kwenye uchaguzi.

Nimeieleza World Bank kuwa Tanzania imeshapata mikopo mingi mno ya Elimu tangu Tupate Uhuru na Rais pekee aliyekuwa akitumia mikopo hiyo vizuri ni Nyerere pekee yake ndo maana ktk utawala wake Elimu ilikuwa bure kweli kweli na siyo bure ya mdomoni Kama tunavyoaminishwa sasa hivi.

Nimeieleza World Bank jinsi watoto wadogo wanavyotembea km zaidi ya 10 kwa siku kwenda shule na bado wakifika darasani hakuna madawati, vitabu na uhaba wa walimu,na kwamba kipaumbele cha serikali ya awamu ya Tano siyo Elimu bali ni ununuzi wa ndege na miradi mikubwa ambayo inazidi uwezo wa nchi kiuchumi.

Na pia nimeieleza World Bank jinsi serikali ya awamu ya Tano ilivyodhamiria kuua upinzani kwa nguvu zake zote,kwa hiyo si ajabu hizo pesa zitatumika ktk operesheni Tokomeza upinzani.
 
My Son drink water,
Who the hell do you thing you as a mere organism can write to WORLD BANK and get listened? Kosa la Zito ni kutumia kofia ya Ubunge na facilities za nembo za bunge la Tanzania kuaminisha World Benki kwa hicho alichokisema. Lakini muwe munajua usaliti wa nchi yako katika nchi yoyote hile ni kosa (na sijui lakini) linaweza kulinganishwa na "uhaini". Kuifitinisha nchi yako katika maslahi ya kiuchumi ni ngazi ya juu ya uhujumu uchumi na uhalifu ambao hauwezi kukuacha salama. Kafanye usaliti huo katika nchi za mashariki ya kati au china uone kama hutakatwa kichwa!
 
Kuwa mpole, tulia kwanza. Mbona World Bank ukianika facts with evidence wanakusikiliza vizuri sana? Kwani yale mashirika yanayokuwa funded na world bank kwenye miradi mbalimbali barua au proposals zao huwa zinakuwa nembo ya bunge?
 
Back
Top Bottom