Sio Wakenya tu wanaotuzidi Ujanja, hata Warundi, Waganda na Wanywaranda pia

Niliishi kasulu wakati nasota kutafuta life ,Nilioajiriwa nilitaman nirud tena huko target ni kilimo na ufugaji ila bahati mbaya kila nikiomba kuhama nafelishwa tu
Karibu sana mkuu kwa sasa kumenoga ingawa kuhusu kilimo kama ulikuwa ukitegemea pori au mashamba ya kagera nkanda kwa sasa yamezuiliwa na kuchukuliwa na shirika la hifadhi (TANAPA, ) so unaweza tumia mashamba yaliyoko karibu ila utatumia kilimo cha kisasa cha mbolea nyingi ili kupata mazao mengi kama utafanikiwa kurudi karibu sana,
asante
 
Migodini warundi hawacheki na kima wakipata chao, lakini unaona watz wakipata na ujamaa wao full kujipendekeza! Ni kweli dawa ni ku venture away from comfort zone, na uthubutu( kitu ambacho watz hatuna!)

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
Huo ujamaa utaondolewa baada ya sisi kutumia muda vizuri, wenzetu wamefundishwa thamani ya muda ndo maana wako hivyo, sisi tujitahidi kupinga mambo yanayotupotezea muda Kama kushinda kanisani siku nzima, bar usiku mzima, mikutano wakati wa kazi, msiba mwezi mzima watu hawaziki ni kula na soga peke yake, vikao vya harusi mwaka mzima, yaani mtu analazimishwa kutumia muda wake vibaya wakati wenzetu wanafanyakazi usiku na mchana na muda wa kupoteza hawana, hasa vijana tukiwa na nguvu tunatumia muda vibaya kwasababu ya ujamaa na mambo yanalazimisha tuchezee muda.
 
Huo ujamaa utaondolewa baada ya sisi kutumia muda vizuri, wenzetu wamefundishwa thamani ya muda ndo maana wako hivyo, sisi tujitahidi kupinga mambo yanayotupotezea muda Kama kushinda kanisani siku nzima, bar usiku mzima, mikutano wakati wa kazi, msiba mwezi mzima watu hawaziki ni kula na soga peke yake, vikao vya harusi mwaka mzima, yaani mtu analazimishwa kutumia muda wake vibaya wakati wenzetu wanafanyakazi usiku na mchana na muda wa kupoteza hawana, hasa vijana tukiwa na nguvu tunatumia muda vibaya kwasababu ya ujamaa na mambo yanalazimisha tuchezee muda.
Uswahili mwingi Tz
 
Mkuu umeongea point kubwa sana.

Lakini bongo Kuna changamoto sana halafu hatupendani sisi kwa sisi, nikupe mfano wangu Kuna shamba huku Sumbawanga ni la kanisa bhasi nikaomba Ekari 40 nilime alizeti Toka mwaka Jana mwezi wa9, mwezi wa 10 mwishoni ndio nilikuja kuonyeshwa shamba tena ni baada ya kuwasumbua sanaaa.

Bhasi msimu wa kulima alizeti huku ni mwezi February kwasababu mvua zinakua zimepungua kiasi, kipindi nasubiri msimu nashangaa huyo mzee kanifuata ananiambia shamba alilonipa amempa mtu mwingine, DAAH NILISIKITIKA SANA NIKASEMA POA HAINA SHIDA.

Kuna eneo niliomba nilime kiangazi kwasababu maji yapo karibu walinibania kunipa eti hapo Kuna mtu huwa analima Amekuja mkenya mmoja hivi wamempa eneo lilelile nililoomba... NIKAPIGA MOYO KONDE SITAKUJA KUOMBA TENA SHAMBA KWA HILO KANISA JAPOKUA NASALI HAPOHAPO KANISANI.

BONGO NYOSO SANAAAA, TUMEJAA HILA, WIVU NA HUSUDA NA HIZI TABIA HATA VIONGOZI WETU WAKUU WA KISERIKALI WANAZO, YAANI WAKIONA CHALIII UNATAKA KUFANYA VITU VIKUBWA UTAONA VIUZIBE VINGI SANAAAAA.
Shamba la kanisa, sadaka zinaenda italy
 
Na bado Wasukuma wanaichangamkia ardhi si mchezo.Kufikia mwaka 2090, 60% ya ardhi ya nchi hii nitakuwa ni mali yao.Nenda Kigoma,Katavi,Mbeya,Ruvuma,n.j uone wanavyonunua mashamba na kufyeka mapoli.

Na hawa ni Watanzania wenzetu wanaojua thamani ya ardhi.
 
Tozo zipi? Sawa Tozo Ok, ila vipi Wakenya wanakuja hadi kulimia huku kwetu vipi hilo?
Ni kweli wakenya wanakuja kwetu kulima, lakini mjue kuna watanzania wengi tuu wanalima kenya wengine wamefungua hadi biashara zingine nje ya kilimo, hivyo ni issue ya kuangalia ni wapi panakufaa. Mimi kuna jamaa ni jirani yangu yuko vzr tu, analima na ameajiri vijana wengi toka kijijini, Na sio kenya tu wako watanzania wako South Africa na zambia kwa uchache tu nimetaja
 
Back
Top Bottom