Sio Wakenya tu wanaotuzidi Ujanja, hata Warundi, Waganda na Wanywaranda pia

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Kuna Mjadala sana siku kadhaa kuhusu Wakenya na ishunzima ya wakenya kuwa wengi sana Tanzania kwa uwekezaji ilihali sisi tukiwa na kampuni kama 30.

Niliwahi enda Kigoma na nilikaa kaa sana kule na katika kakaa yangu nilikutana na Waganda, Warundi, Wanywarwanda yaani wale wana faidi sana Kigoma nazani kuliko sisi.

Nilicho choka kabisa ni baada ya kuambia kwamba Rwanda ikichukua ule muhogo wana uprocess na wana pelekea Gaboni west Africa kwa kipitia Kongo nazani.

Uganda nao wanachukua ule muhogo wana u process na kwenda kuuza Sudani kusini, Uganda pia wanalima sana Muhogo ila nazani hautoshi kwa wao ku Export then wanakuja kuchukua Kigoma.

Burundi pekee ndo wanao chukua ule muhogo na kuutumia wenyewe.

Ukienda kule Mang'ola Karatu Wakenya wana lima sana vitunguu wamekamata mashamba ya kutosha, wako kule Moshi wanalima nyanya sana, Wako Arusha wanalima nyanya pia.

Watanzania wengi Kigoma tunaichukulia kama sehemu ya hovyo, mbali, kubaha, polini lakini Warwanda, Waganda wanapiga Dolla kupitia muhogo wa Kigoma na wananunuakwa bei ndogo sana.

Mentality zetu ni za kipekee sana aiseee, bado mentality za Ujamaa zinatusumbua sana.
 
Ukiijua historia ya Mwamwindi ndio utasikitika, hasa pale Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati huo, Kleruu alipoenda Isimani akakuta Mwamwindi Yuko shambani kwake siku ya Xmas, akamzingua eti kwanini hufànyi kazi kwenye shamba la ujamaa uko shambani kwako?
Mwamwindi akajibu leo ni sikukuu, hata kwenye shamba la Kijiji hamna mtu wako kilabuni, akazabwa kibao, ndipo akampiga risasi
I hate it kwakweli
 
Braza ulichosema ni sahih kbsa wabongo sijui tumelogwa na vtu gan...mimi nipo kgoma apa lkn warundi,wanyarwanda,waganda wanakuja kuchukua vtu vingi xn bongo sio tu muhogo ata tangawiz wanabeba..kw mfano rwanda Wana kiwanda cha kuprocess tangawz ikisindikwa inatembea mbele uko ulaya...lakn huku wananunua mzgo bei ndgo xn wabongo wanalaliwa kwa kua hawana sehm yakuplka
 
Na hivyo ndo vtu vnavyotuchelewesha wabongo...ukitaka kuexport mzgo dah humo njian utaimba haleluya utakaguliwa had boxer mashariti ni mengi sana...hatujifunzi kw wakenya juzi kat uhuru kenyata karuhus wat wafanye biashara bila mashariti yyte... Km una mzgo peleka tu
 
Sisi tunaweza tena sana tuu, shida ni upashanaji hbr tuu baasi ... Tulikuwa wajamaa hivi tuko na advantage ya kufanya vzr kuliko hao majirani, sbb ya ujamaa upashanaji hbr ulio chanya uanzie juu kushuka chini tutaweza !
 
Upashanaji habari upi Dunia hii? Ni habari gani kwa sasa utaikosa? Wakenya wako kule Mang'ola wanalima vitunguu nani kawapeleka kule?
 
Na hivyo ndo vtu vnavyotuchelewesha wabongo...ukitaka kuexport mzgo dah humo njian utaimba haleluya utakaguliwa had boxer mashariti ni mengi sana...hatujifunzi kw wakenya juzi kat uhuru kenyata karuhus wat wafanye biashara bila mashariti yyte... Km una mzgo peleka tu
Ku export ukisha kamilisha vigezo mbona una Export? Wao hao Waganga wana vuka vipi nayo Boda? Wakenya wanavuka vipi na Vitunguu yao pale boda ya Namanga au Tarakea au Holili?
 
Ukiijua historia ya Mwamwindi ndio utasikitika, hasa pale Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati huo, Kleruu alipoenda Isimani akakuta Mwamwindi Yuko shambani kwake siku ya Xmas, akamzingua eti kwanini hufànyi kazi kwenye shamba la ujamaa uko shambani kwako?
Mwamwindi akajibu leo ni sikukuu, hata kwenye shamba la Kijiji hamna mtu wako kilabuni, akazabwa kibao, ndipo akampiga risasi
Aisee
 
Hatukatai wa kuja always huwa wanakuja na idea nyingi na fursa za kibiashara kwa sababu wanaona hizo fursa na kuzichukua

Ila na sisi tumezidi uzembe ingawa ni wachache sana wanaoiga na kufanya nao

Kwanza biashara haina siri ukiifatilia
Kuna nchi ukitembelea watu wanafanya biashara nchi nyingi za Africa na kuchukua biadhaa zao au zetu

Watu wanaridhika na kuuza hapo hapo biashara ndogo na haoni faida ya exporters kabisa
 
Back
Top Bottom