wagagagigi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2014
- 890
- 986
Hapa kwa kweli umetusemea wengi mkuu!Kuna zimwi kubwa sana gizani linalowatisha vijana nuruni... Mwisho wa siku
Uthubutu unakufa
Utayari unapotea
Ndoto zinafifia
Kauli ya yule katibu mkuu ilinisikitisha sana na iliwakatisha tamaa vijana wengi.. I have a family to feed not the public to impress...!
Just imagine mtazamo kama huu kwamba tunafanya siasa ili kuifurahisha hadhira... [emoji848][emoji124][emoji124][emoji144][emoji144][emoji144]that one was too low...
Jr[emoji769]
Watu ambao tuliwategemea kuwa mstari wa mbele kusimamia ukweli na kuwa upande wa haki wanakata tamaa ovyo!
mifano ni mingi mno; Wa kina Mtatiro, Lipumba, Slaa na wengi wengineo ni matunda ya kukata tamaa!
Kutokana na kukata kwao tamaa wakaamua ni bora kupata kitu kuliko kukosa kila kitu!
Humu JF mwenzetu Paskali kama ukisoma nyuzi zake na ukatafakari kwa umakini, utagundua kwamba na yeye ama kaingia katika waliokata tamaa au anaelekea huko! Baya zaidi huyu ndugu yetu Paskali anajaribu kutupa somo kpitia nyuzi zake hizo la kutukatisha tamaa!
Hebu tujiulize hivi lengo la kutukatisha tamaa ni lipi?
Je... sote tukiwa na mtizamo kama wake /wao tutakuwa salama?
Kwamba nchi itaendelea na kila mtu atakuwa na uhakika wa usalama wake na haki zake zitalindwa?
KWa nini hawaandiki au hawayapi umuhimu yanayopaswa kuandikwa?
Bunge linasigina katiba mbona akina Mwankijiji na Paskali hamuandiki kuhusu haya?
Watanzania tuache unafiki na ubinafsi... ili tutoke hapa lazima kwa umoja wetu tujali zaidi maslahi ya taifa kuliko vyama!
Tafadhalini tuache 'Uzombe'.