Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Mshana , kwanza nikubaliane nawe kuwa, Tanzania tunahitaji vyama vya upinzani makini na vyenye nguvu. Upinzani ndio unaojenga siasa nzuri za kidemokrasi.

Kuhusu kifo cha Chadema, mimi sidhani hicho chama kinaweza kufa kwa kuuliwa na CCM, bali kinaweza kufa kwa KUJINYONGA chenyewe, chadema wasitafute mchawi wao njee ya Chadema.

Ni wakati muafaka wanachama wa chadema mkafanya utafiti wa matatizo yenu, na jee inawezekanaje mkapata mapigo mengi na hali mna kitengo cha security. Enzi ya Dr.Slaa chadema ndicho kilikuwa kinatupa mapigo mengi kwa ccm, tena kitego chao cha security kilikuwa imara sana, nini kimetokea, palikuwa hakuna hamahama, siasa zao zilikuwa zina ubora kuliko sasa, waliweza fukua madudu mengi, waliweza faulu kulazimisha mabadiliko ya serekali mara kadha.

Siku hizi kitu mnachokimudu sana ni matusi mitandaoni, na mpiganaji wenu mkubwa ni KIGOGO ambaye ni mtu wa pesa, ACT wakimlipa vizuri anapaidha bendera yao, naona miezi hii pay check yake inatoka chadema.

Rudini mezani, mkajipange upya, mnahitaji mabadiliko ya uongozi. Cha ajabu kuwa hata Lissu naona ama kanyamazishwa na viongozi wake au kaona mambo sio mazuri ndani ya chama, kaamua kuka kimya na kupunguza mashambulizi.

CHADEMA KINAJINYONGA CHENYEWE, WASIMLAUMU MTU YOYOTE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiachana na kile kitengo cha propaganda cha CCM na ile praise team. Wengine wote hatupaswi kuwa na muono kimo cha mbilikimo. Ni lazima tuwaze zaidi ya mwisho wa uono wa macho yetu.

Nimemuona P kwenye mada za CHADEMA. Utabiri wa mabaya. P ulituasa tuepuke prophecy of doom. Tusiwaase wengine huku sisi tunatenda.

Natambua mgongano wa mawazo na hoja. Natambua tofauti za kimtazamo kati yetu lakini haya yasitufanye tukafika mahali tukawa na mitazamo finyu. Tunaihitaji CHADEMA kama taasisi imara ili CCM isijisahau sana. Miaka ile ya 1995-2005. Wakati huo NCCR kikiwa chama chenye nguvu na ushawishi, kuna mengi yaliyotokea lakini pengine hayakumbukwi sana.

Alitokea Augustine Mrema, waziri machachari wa CCM aliyebwaga manyanga na kujiunga na NCCR Mageuzi. Wengi bado tunakumbuka kilichotokea pale, kukawa na vichwa hasa.

Baadae NCCR ikafitinishwa na kumgeuka. Kukawa na NCCR mbili. Huo ndio ukawa mwisho wa kile chama. Kuna mtu pale NCCR mmojawapo wa viongozi mahiri akiitwa Prince Bangeda. Mpaka leo sijui alitofautiana nini na Mrema. Alimuandika vibaya na kumchambua Mrema kwenye safu yake ndani ya gazeti la Rai kila Jumatano kwa makala ndefu ndefu kwa miezi kadhaa. Nadhani hakuna mwanasiasa alichambuliwa na kuandikwa vibaya mpaka leo hii kama alivyofanya Bangeda kwa Mrema.

Leo hii Bangeda yuko wapi na Mrema yuko wapi? Unapotumika angalia unatumikaje. Usipojiongeza, wanaweza kukufanya kama toilet paper.

CHADEMA inapigwa vita sana kwakuwa ni mwiba mchungu kwa CCM. Project za kukiangamiza hiki chama ni nyingi mno. Watu wanaotumika ni wengi mno. Pesa iliyokwisha tumika ni nyingi mno. Hakuna chama cha siasa kimepitia mapigo mengi kama CHADEMA, lakini mpaka leo kipo hai na kinadunda. Kukiombea kife ni:

Kupoteza matumaini ya vijana wasomi wengi
Ni kupoteza viongozi wazuri wa kesho
Ni kupoteza matumaini na furaha wa wapiga kura milioni 7
Ni kupoteza matumaini na furaha ya wapenzi, washabiki na wafurukutwa zaidi ya milioni kumi

Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.

Viongozi walioko CHADEMA ni binadamu kama wewe na mimi wana mapungufu yao, lakini kwenye mizania ya haki wana mengi mazuri ya kukumbukwa vizazi na vizazi. Wanahitaji tuwatie moyo, tuwasaidie na kuwapa faraja kwenye kila hatua wanayopitia. Tusiwakatishe tamaa. CCM iliyokuwa na upendo wa kweli kwa Watanzania ni ile ya Mwalimu Nyerere tu. Baada ya hapo ni vurugu mechi kwa kwenda mbele.

Makala nyingi za kuiponda CHADEMA na kukiombea mabaya hata kama sio sehemu ya zile project zina ukakasi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Je, kuna personal issues nje ya politik?

Jr[emoji769]
Ni kweli kuwa na chama imara cha upinzani ni muhimu sana kwa afya ya Taifa letu, kiwe chama chochote kile chadema, nccr mageuzi, cuf au act n.k lakini kwa mtazamo wangu chadema walishajimaliza wenyewe tangu 2015 na kuanzia hapo wamepoteza kabisa muelekeo wanapambana kupinga kila kitu hata chenye faida na maana kwa nchi.
 
Big umeandika kwa hisia sana. Na ndivyo inavyotakiwa kuwa.

Chama la wana halifi leo wala kesho hilo.

StaySafe with CHADEMA.[emoji111][emoji111][emoji111][emoji111]
[emoji120][emoji120][emoji120]

Jr[emoji769]
 
Mtu akiniambia CHADEMA ni chama bora, nashindwa kuelewa ubora uko wapi. Ikiwa miaka yote hii kimeshindwa kuwaandaa vijana wasomi kuchukuwa nafasi za uwongozi, sijui huo ubora unatoka wapi? Kijana anachukuliwa chuo kikuu, akiingia CHADEMA anafundisha kupinga kila kitu na kukimbizana na dola. You can't create tomorrow's leader by disobeying the rule of law.

Ukiwa CHADEMA lazima uwe tayari kutafuna pesa ya umma bila woga wala ukakasi, mikutano kwenye mahoteli makubwa, safari za nje zisizo za lazima, magari ya kifahari hata mmiliki hajulikani ni nani kusema hicho ndio chama cha mfano, sio kwa mfumo uliopo.

Hata itikadi, CHADEMA imeshindwa kuwa hata na kachuo kadogo kutowa somo la itikadi kwa viongozi watarajiwa ili kuwe na muongozo hawa wajuwe CHADEMA inasimamia kitu gani. Halafu watu wanashangaa kuona wanachama wanakihama chama, ni kwasababu wanafikiri CHADEMA na CCM wote wako sawa lakini ni vyama vyenye misimamo tofauti.
People are not disobeying the rule of rather they are opposing and challenging oppressive laws. Kumbuka ata Apartheid ilikua sheria halali,hut tax,kipande policy an the like.
 
Mshana , kwanza nikubaliane nawe kuwa, Tanzania tunahitaji vyama vya upinzani makini na vyenye nguvu. Upinzani ndio unaojenga siasa nzuri za kidemokrasi.

Kuhusu kifo cha Chadema, mimi sidhani hicho chama kinaweza kufa kwa kuuliwa na CCM, bali kinaweza kufa kwa KUJINYONGA chenyewe, chadema wasitafute mchawi wao njee ya Chadema.

Ni wakati muafaka wanachama wa chadema mkafanya utafiti wa matatizo yenu, na jee inawezekanaje mkapata mapigo mengi na hali mna kitengo cha security. Enzi ya Dr.Slaa chadema ndicho kilikuwa kinatupa mapigo mengi kwa ccm, tena kitego chao cha security kilikuwa imara sana, nini kimetokea, palikuwa hakuna hamahama, siasa zao zilikuwa zina ubora kuliko sasa, waliweza fukua madudu mengi, waliweza faulu kulazimisha mabadiliko ya serekali mara kadha.

Siku hizi kitu mnachokimudu sana ni matusi mitandaoni, na mpiganaji wenu mkubwa ni KIGOGO ambaye ni mtu wa pesa, ACT wakimlipa vizuri anapaidha bendera yao, naona miezi hii pay check yake inatoka chadema.

Rudini mezani, mkajipange upya, mnahitaji mabadiliko ya uongozi. Cha ajabu kuwa hata Lissu naona ama kanyamazishwa na viongozi wake au kaona mambo sio mazuri ndani ya chama, kaamua kuka kimya na kupunguza mashambulizi.

CHADEMA KINAJINYONGA CHENYEWE, WASIMLAUMU MTU YOYOTE

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkirindi Inaonyesha wazi ulikuwa na Mahaba na Dr.wa Kushindia Mihogo(Dr.Slaa)ndiyo maana unajitahidi sana kumsafisha na nina uhakika utashindwa tu maana Dr.wa kushindia Mihogo alikimbia mapambano katikati ya vita na kuhamia upande wa pili kuwaunga mkono lakini pamoja na hayo Chadema ilijinyakulia wabunge lukuki kinyume na matarajio ya Dr. wa kushundia Mihogo Dr.Slaa.Ni kweli kabisa Chadema inakabiliwa na magumi mengi sana ikiwa na pamoja na yafuatayo-
1.Wameondokewa na wabunge waliorubuniwa na ccm kisha zikafanywa chaguzi ndogo ccm wakalindwa na vyombo,vya usalama,Tume na watendaji ambao ni makada wa ccm Chadema haikufa
2.Madiwani wakajivua kwa makundu makundi na kuunga mkono juhudi hewa Chadema haikufa.
3.Wakawashambbulia na kuwaua viongozi na wengine kuwajeruhi kwa risasi Chadema haikufa
4.Wamekuwa wakiwafukuza na kuwafungia Bungeni wasishiriki vikao vingi Chadema haikufa
5.Wamekuwa wakiwazulia kesi mbalimbali mahakamani kuanzia Ugaidi hadi Uchochezi Chadema haikufa
6.Wabunge wa chadema wamekuwa wakihudhuria mahakamani karibu na zaidi ya miaka miwili mfurululizo ili tu kuwanyima mwanya wa kuwawakilisha watu wao kisha kuwahukumu kulipazaidi ya M380 cha ajabu hakuna hata senti moja ya chama ilitumika kuwakomboa bali NGUVU YA UMMA ilisimama kati na kumaliza mchongo huo kwa siku chache tu.Hivyo namalizia kusema ni ngumu sana kuiua Chadema maana chama hicho kiko mioyoni mwa wananchi.Pamoja na kwamba ccm inapanga kutumia polisi,Tume na Watendaji ili kuweza kuzima ndoto za wananchi najua hata hivyo hawataweza kuiua Chadema.Sababu ni moja tu Chadema imo mioyoni mwa wananchi wa Tanzania.
 
Hapo ndio unakosea unahusisha maisha na mwenendo wa mtu binafsi na mfumo wa kisiasa. Ujamaa ni mfumo wa kuongoza nchi kuliko imani ya mtu moja moja, ukitoa mifano ya Nyerere na Paul Sozigwa walikuwa ni watu wa aina fulani haimaanishi na nchi lazima iwe kama wao. Ni sawa na kusema ikiwa Mbowe ni mfanyabiashara na ametoka kwenye familia ya kitajiri basi hana uwezo wa kumuongoza mtu masikini kwasababu hakuwa umasikini ni nini.

CCM ni chama cha kijamaa, na ujamaa sio mfumo wa kuwafanya watu wawe masikini na wala haikatazi mtu awe tajiri, ila ni mfumo ambao haumuachi mtu yoyote nyuma kwa kukosa fedha. Ndani ya mfumo wa ujamaa, mtoto wa masikini na mtoto wa tajiri wote wanatakiwa kupata huduma zote za msingi bila kubaguliwa. Ukija kwenye mfumo wa kibepari au kihafidhina kama wa CHADEMA (let the market decided), utakuta yule mtoto wa tajiri anapata huduma zote za msingi kutokana na uwezo wake wa kifedha, huku mtoto wa masikini aidha anapata huduma ya hali ya chini au hapati kabisaa kwa kukosa fedha.
Unaujua ujamaa wewe? Naona unapiga porojo wenzio wenye chumvi nyingi tumeuona na wengine waliuishi!

CCM ni wajamaa kiutawala na si kiitikadi, ujamaa Mwenyekiti ni Mungu ndio maana hapo awali kulikuwa na slogan kama "zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti"" si kwa makosa Bali ndivyo ujamaa ulivyo. Vitu viingi huvijui wewe na unabishana na magwiji.

Hata Nyerere mwenyewe hakuwa mjamaa ndio kisa cha kukosana na Kambona, maana Oscar alimuuliza mbona wewe si mjamaa kwanini unaiingiza nchi kwenye itikadi usiyoiamini Hata wewe? Na Mwalimu alijua ukitaka usipinduliwe eneza itikadi za kijamaa, maana utatisha watu na utakuwa mungu MTU, yote yalitokea baada ya mapinduzi 1964. Ulizia kama je Mwalimu alikuwa mjamaa kabla ya mapinduzi na nikwanini alikuwa na urafiki na JF Kennedy na west Germany? Wakati wa cold war!!

Hujui vingi wala usijitutumue, kiufupi CCM ni chama laghai cha kijamaa bila mjamaa
 
hizo ni baadhi ya weakness za chama! lakini bado ni watu wanaoweza kutengeneza hoja zenye kusimama, nikupe mfano mdogo, ukiangalia maono ya magufuli kipindi cha corona alafu ukiangalia na mono ya mbowe alafu ukija kuskiliza conclusion ya WHO ndo utajua nan akili zimo na nan kazi yake bendera fuata upepo,mm sjui huo ushindi mnauongeleea ni upi lakini mm binafsi siwezi kumwaga kura yangu kwa mtu yoyote wa cdm nlishafanya ivo kipindi mlivokua na hoja za kuibua madudu serikalini but not anymore, bila shaka watawapigia kura watu wengine but kwangu mm its a not, ingawa these few days nmeona progress ya siasa safi kutoka kwa NCCR MAGEUZI, ingawa bado chadema ina nafasi yake kubwa sana katika hii nchi
Nimekuambia umepofushwa na ukabila, naweza nikakujua pamoja uko mbali, unahisi kuhusu corona huyo kafanikiwa? Unaishi mji gani kwani? Kama dar utakuwa mwandawazimu! Kama huko mikoani hujui bado uliza utaelekezwa kwasiri!

Watu wanazikwa usiku, wewe unajua wanaharakati wanatania, kwanini Wizara imekataza kuzika usiku japo kisiri bado wanazika? Na kwanini wanazika usiku? Jiulize!

Corona ni ugonjwa ulifanyiwa tafiti ni science si wa kukurupuka na kujiongelea yako! Unajua kwanini majirani wanatunyanyasa sasa kuingia kwao? Tumekuwa wasafirishaji wazuri wa corona usisombwe na propaganda ukaonekana na wewe hamnazo!

Ukienda Congo huruhusiwi kuingia, Zambia wametufungia, Uganda tunanyanyasika na Leo Kenya wametufungia bado tuu huelewi?

Zambia ina waginjwa 300 lakini 100 wana connection na Tanzania, Malawi nusu wana connection na Tanzania bado hujui tatizo Tanzania?

Wakisema wapime kama wengine wanavyopima nahisi tutakuwa tunaelekeana na uingereza au Hata marekani kwasasa!
 
People are not disobeying the rule of rather they are opposing and challenging oppressive laws. Kumbuka ata Apartheid ilikua sheria halali,hut tax,kipande policy an the like.
Challenging injustice or operation can be done peaceful and end up with long lasting solution when all sides agree. Duniani kote fighting operations forceful hasn't brought a lasting solution, sio South Africa, sio Marekani wala sio Afghanistan. Chadema they like to use these type of tactics of forcing their way through because it suited few hardliners but majority of Tanzanian's wanaona ni ukorofi na hawapendi kuona malumbano. Mwisho wa siku mnapoteza wafuasi kuliko kuongeza.
 
Mkirindi Inaonyesha wazi ulikuwa na Mahaba na Dr.wa Kushindia Mihogo(Dr.Slaa)ndiyo maana unajitahidi sana kumsafisha na nina uhakika utashindwa tu maana Dr.wa kushindia Mihogo alikimbia mapambano katikati ya vita na kuhamia upande wa pili kuwaunga mkono lakini pamoja na hayo Chadema ilijinyakulia wabunge lukuki kinyume na matarajio ya Dr. wa kushundia Mihogo Dr.Slaa.Ni kweli kabisa Chadema inakabiliwa na magumi mengi sana ikiwa na pamoja na yafuatayo-
1.Wameondokewa na wabunge waliorubuniwa na ccm kisha zikafanywa chaguzi ndogo ccm wakalindwa na vyombo,vya usalama,Tume na watendaji ambao ni makada wa ccm Chadema haikufa
2.Madiwani wakajivua kwa makundu makundi na kuunga mkono juhudi hewa Chadema haikufa.
3.Wakawashambbulia na kuwaua viongozi na wengine kuwajeruhi kwa risasi Chadema haikufa
4.Wamekuwa wakiwafukuza na kuwafungia Bungeni wasishiriki vikao vingi Chadema haikufa
5.Wamekuwa wakiwazulia kesi mbalimbali mahakamani kuanzia Ugaidi hadi Uchochezi Chadema haikufa
6.Wabunge wa chadema wamekuwa wakihudhuria mahakamani karibu na zaidi ya miaka miwili mfurululizo ili tu kuwanyima mwanya wa kuwawakilisha watu wao kisha kuwahukumu kulipazaidi ya M380 cha ajabu hakuna hata senti moja ya chama ilitumika kuwakomboa bali NGUVU YA UMMA ilisimama kati na kumaliza mchongo huo kwa siku chache tu.Hivyo namalizia kusema ni ngumu sana kuiua Chadema maana chama hicho kiko mioyoni mwa wananchi.Pamoja na kwamba ccm inapanga kutumia polisi,Tume na Watendaji ili kuweza kuzima ndoto za wananchi najua hata hivyo hawataweza kuiua Chadema.Sababu ni moja tu Chadema imo mioyoni mwa wananchi wa Tanzania.
Ndugu, sidhani kuna chama kimekufa na kufutika kabisa, hata CUF bado kiko jina, kadhalika vyama vingi. Tunachozungumzia ni kinachokiuwa chama ni vita ya ndani na sio ya kutoka njee. Msijidanganye mambo hayajakuwa shwari Chadema tokea Lowassa ahamie chadema hadi sasa.

Enzi za akina Slaa, Zitto mlikuwa macho sana, mliona kila kombora linalolengwa kwenu na kulipangua, lakini sasa makombora yanatua.

Ninacho sema Msiangalie vita mnayopigwa na serekali na CCM, angalieni matatizo yenu ya ndani ambayo ndiyo ya hatari sana kwa uhai wa chama, na mkiambiwa hivyo mnakurupuka na kujitetea bila hata plani, CHADEMA MNAJINYONGA WENYEWE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuambia umepofushwa na ukabila, naweza nikakujua pamoja uko mbali, unahisi kuhusu corona huyo kafanikiwa? Unaishi mji gani kwani? Kama dar utakuwa mwandawazimu! Kama huko mikoani hujui bado uliza utaelekezwa kwasiri!

Watu wanazikwa usiku, wewe unajua wanaharakati wanatania, kwanini Wizara imekataza kuzika usiku japo kisiri bado wanazika? Na kwanini wanazika usiku? Jiulize!

Corona ni ugonjwa ulifanyiwa tafiti ni science si wa kukurupuka na kujiongelea yako! Unajua kwanini majirani wanatunyanyasa sasa kuingia kwao? Tumekuwa wasafirishaji wazuri wa corona usisombwe na propaganda ukaonekana na wewe hamnazo!

Ukienda Congo huruhusiwi kuingia, Zambia wametufungia, Uganda tunanyanyasika na Leo Kenya wametufungia bado tuu huelewi?

Zambia ina waginjwa 300 lakini 100 wana connection na Tanzania, Malawi nusu wana connection na Tanzania bado hujui tatizo Tanzania?

Wakisema wapime kama wengine wanavyopima nahisi tutakuwa tunaelekeana na uingereza au Hata marekani kwasasa!

kwan wewe unakaa dunia gan si mshaambiwa hakuna budi zaidi ya watu kuishi nayo? ama hujaskia maelezo ya WHO, mbna hata ligi la spain limeanza leo na maisha yanatakiwa kuendelea kama kawa!

boda ya nakonde ishafunguliwa kitambo sana you seem very outdated and yes nakaa dar and maisha yanaendelea kama kawa, na tunasubiria ligi letu pia lianze nyie endeleeni kusubiria mbowe awape tamko
 
Nakonde imefunguliwa lini tena? Wiki iliyopita jtatu ndio ilifungwa! Ngosha usiandike tuu ilimradi unaandika! Kama umeenda shule itendee haki!

WHO wanaset baseline kilasiku ukiruka hatua umeharibu na sisi timeharibu.
 
1589644821999.png

yawezekana sio ata basi kwamba hauna izi taarifa labda ulikua unataman sana pasifunguliwe, yaani hili lichama lenu tushalichoka
 
Nakonde imefunguliwa lini tena? Wiki iliyopita jtatu ndio ilifungwa! Ngosha usiandike tuu ilimradi unaandika! Kama umeenda shule itendee haki!

WHO wanaset baseline kilasiku ukiruka hatua umeharibu na sisi timeharibu.

1589645009071.png

pole pole tunapata chama kipya kikuu cha upinzani, cdm mshapoteza dira kwanza ata hamkua na dira
 
Ukiachana na kile kitengo cha propaganda cha CCM na ile praise team. Wengine wote hatupaswi kuwa na muono kimo cha mbilikimo. Ni lazima tuwaze zaidi ya mwisho wa uono wa macho yetu.

Nimemuona P kwenye mada za CHADEMA. Utabiri wa mabaya. P ulituasa tuepuke prophecy of doom. Tusiwaase wengine huku sisi tunatenda.

Natambua mgongano wa mawazo na hoja. Natambua tofauti za kimtazamo kati yetu lakini haya yasitufanye tukafika mahali tukawa na mitazamo finyu. Tunaihitaji CHADEMA kama taasisi imara ili CCM isijisahau sana. Miaka ile ya 1995-2005. Wakati huo NCCR kikiwa chama chenye nguvu na ushawishi, kuna mengi yaliyotokea lakini pengine hayakumbukwi sana.

Alitokea Augustine Mrema, waziri machachari wa CCM aliyebwaga manyanga na kujiunga na NCCR Mageuzi. Wengi bado tunakumbuka kilichotokea pale, kukawa na vichwa hasa.

Baadae NCCR ikafitinishwa na kumgeuka. Kukawa na NCCR mbili. Huo ndio ukawa mwisho wa kile chama. Kuna mtu pale NCCR mmojawapo wa viongozi mahiri akiitwa Prince Bangeda. Mpaka leo sijui alitofautiana nini na Mrema. Alimuandika vibaya na kumchambua Mrema kwenye safu yake ndani ya gazeti la Rai kila Jumatano kwa makala ndefu ndefu kwa miezi kadhaa. Nadhani hakuna mwanasiasa alichambuliwa na kuandikwa vibaya mpaka leo hii kama alivyofanya Bangeda kwa Mrema.

Leo hii Bangeda yuko wapi na Mrema yuko wapi? Unapotumika angalia unatumikaje. Usipojiongeza, wanaweza kukufanya kama toilet paper.

CHADEMA inapigwa vita sana kwakuwa ni mwiba mchungu kwa CCM. Project za kukiangamiza hiki chama ni nyingi mno. Watu wanaotumika ni wengi mno. Pesa iliyokwisha tumika ni nyingi mno. Hakuna chama cha siasa kimepitia mapigo mengi kama CHADEMA, lakini mpaka leo kipo hai na kinadunda. Kukiombea kife ni:

Kupoteza matumaini ya vijana wasomi wengi
Ni kupoteza viongozi wazuri wa kesho
Ni kupoteza matumaini na furaha wa wapiga kura milioni 7
Ni kupoteza matumaini na furaha ya wapenzi, washabiki na wafurukutwa zaidi ya milioni kumi

Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.

Viongozi walioko CHADEMA ni binadamu kama wewe na mimi wana mapungufu yao, lakini kwenye mizania ya haki wana mengi mazuri ya kukumbukwa vizazi na vizazi. Wanahitaji tuwatie moyo, tuwasaidie na kuwapa faraja kwenye kila hatua wanayopitia. Tusiwakatishe tamaa. CCM iliyokuwa na upendo wa kweli kwa Watanzania ni ile ya Mwalimu Nyerere tu. Baada ya hapo ni vurugu mechi kwa kwenda mbele.

Makala nyingi za kuiponda CHADEMA na kukiombea mabaya hata kama sio sehemu ya zile project zina ukakasi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Je, kuna personal issues nje ya politik?

Jr[emoji769]
Q 2

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ngosha!

1589645455920.png

hizi sasa ndo siasa safi, apa tunajua ccm wakishindwa kutekeleza majukumu yake kuna chama kingine tunaweza kukiangalia sio chama kila saaa vurugu tu, hamna dira! yaani mmetumia hadi corona kama sera yenu, ivi mna katiba ya chama kwel?
 
Nakonde imefunguliwa lini tena? Wiki iliyopita jtatu ndio ilifungwa! Ngosha usiandike tuu ilimradi unaandika! Kama umeenda shule itendee haki!

WHO wanaset baseline kilasiku ukiruka hatua umeharibu na sisi timeharibu.

1589645642544.png

siasa safi, hata wananchama wenyewe wanafurahi kua kwenye chama
 
Stakehigh,

Nani kaleta vurugu au ndio umeongopewa na ukaongopeka? Watu mmewauwaa wamekaa wanawaangalia, mmewabimbika Kesi, mmewadhalilisha wangekuwa na vurugu si wangewapiga mabomu?
 
Back
Top Bottom