Sio tu uaminifu uwepo, bali uonekane kuwepo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio tu uaminifu uwepo, bali uonekane kuwepo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tuko, May 11, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Juzi kati nilijikuta napatanisha ugomvi fulani wa mtu na demu (sijui mchumba?) wake. Case ilikuwa mwanaume analalamika kuwa kila ikishafika usiku wa saa nne(hawaishi pamoja), sim ya demu inakuwa bize sana. Analalamika pia kuwa wakiwa pamoja mara zote, ama dem anazima simu au anaweka silent bila vibration, na sio simu zote zinapokelewa au msg zote zinajibiwa. Mara kadhaa jamaa anasema kuwa akiwa anachat na dem kwenye simu, sometimes anatumiwa wrong msgs kutoka kwa huyo dem wake ambazo akiziangalia maudhui yake yake zinaashiria wazi kuwa zilikuwa zinaenda kwa mwanaume mwingine na zina harufu ya mapenzi. Kikubwa zaidi ni kuwa jamaa anasema akimshtukiza dem wakakutana, dem hampi simu hadi adelete msg zote, na zipo namba nyingi kasev bila kuandika jina kwenye sim yake. Kutokana na ushahidi huo wa kimazingira, jamaa anaona kabisa uaminifu kwa dem wake haupo.

  Hata hivyo kwa upande wa dem yeye anadai kuwa ni kwel sim yake inakuwaga bize usiku kwani anamwazimaga dada yake aongee kama hana vocha. Anakubali pia kuwa anazimaga sim akiwa na jamaa yake kwa sababu hapendi usumbufu toka kwa mashosti na wafanyakazi wenzake. Kiufupi ni kuwa malalamiko yote ya jamaa dem anakubali lakini anayapangua kwa kutoa reasons fulani.

  Tulijadili mgogoro huo, na japo hakukuwa na ushahidi kuwa dem anamcheat jamaa, lakini nililazimika kumshauri dem kuwa sio tu lazima uaminifu uwepo, bali unatakiwa kuonekana upo. Asikubali kujenga mazingira tatanishi kwa kuwa tu ana kisingizio na haachi ushahidi.

  Yapo mambo ambayo tusipoyahandle vizuri hata kama sio kwa nia mbaya yanaweza kuleta matatizo katika ndoa/mahusiano.

  Kuchat na simu, Kupokea simu unapopigiwa, jinsi unavyoongea na simu, muda wa kurudi nyumbani, marafiki zako nk, ni mambo ambayo yanaweza kujenga mazingira ya kutokuaminiwa.

  Kwangu mi nasema, "ni bora usiwe mwaminifu ukaonekana mwaminifu, kuliko kuwa mwaminifu lakini huonekani mwaminifu"...

  Take care.... AIDS is there...
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Bora pekee ni kuonekana na kua mwaminifu!!
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mtu anaweza kuwa mwaminifu ila akawa na move zinazotia doa uaminifu wake.
  Personally nimewahi kukumbwa na tatizo hili miaka ya mwanzoni nilikuwa naona raha kuwazungusha bila kuwapa jibu kavu la SIKUPENDI,SIKUTAKI.......with time meseji zao kidogo ziniharibie.

  nakubaliana na mleta sred kuwa kuna haja ya kuonekana mwaminifu unapokuwa na uaminifu.
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kwa ufupi ni kua huyo dada (shemejio or whateva) hamfai huyo kaka, na relationship ambazo mwanamke ndo ana cheat na mwanaume katulia results zake si nzuri mwishoni mana guys wana mtindo wa kuchukua hatua mkononi.. Na hapo ni waz kua mkaka anajua kuna wengine - for matatizo ni makubwa na sababu zinazotolewa ni za kitoto. Sishangai kaka kusubiri maana majibu tuliyapata katika thread ya "tunavumilia ili iweje?"

  Yote 9, 10 ni statement yako hapo juu... labda kama sijaielewa, utatupa vipi ushari "Take care.... AIDS is there..." wenye uzito hivyo alafu what you believe in is contradictory???
   
 5. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hcho kimeo tu dem haiwezekan akiwa na jamaaa ful kupgiwa simu ful kuchat wap hyo mwizi mkubwa kwan jamaa kakosa madem wengine anajiweka matatani tu kiufupi dem anamabwana wengine we umemfcha ila ukwel unaujua the way alivyokuwa anaongea live utajua tu hapa there is something wrong
   
 6. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi naacha hata simu gani iingie napokea hapohapo, huyo dada atakuwa anamzingua jamaa tu watu gani wa ofisini wapige usiku namna hiyo? Aanze upya abadili simu awe mkweli kwa mtu wake
   
 7. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Achana na mapenzi mkuu, pale unaposumbuliwa ndio hapohapo unapaona panakufaa
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndo maana nikasema bora ni pale unapoonekana mwaminifu na unapokua mwaminifu pia!!!Mtu akishakua na wasiwasi na wewe hata kama umetulia haitasaidia!
   
Loading...