Sio tu tusichanganye Dini na Siasa, bali pia tusitumie maneno ya Mungu kwa hoja za kisiasa, shuhudia maajabu ya neno "MENE MENE TEKELI NA PERESI'!

Tena sana. Hapa kwetu jamaa mmoja alisema anaweza kunywa vipaketi 30 vya konyagi enzi za viroba. Watu wakaweka dau akaanza kunywa alipofikia cha 17 alipumua kwa nguvu roho ikakatoka lakini wakati wa mazishi ikasemwa KAZI YA MUNGU. Ndio maana ukasema ni upumbavu nami naunga mkono
Tena Upumbavu hasa ,na Sifa ya Mpumbavu hata umtwange kwenye Kinu hawezi kuisha Upumbavu wake.Umesomeka Mkuu.
 
Kuna watu, Watanzania wenzetu wanaamini leo neno hili "MENE MENE TEKELI NA PERESI'!, linaweza kutokea Tanzania!
Na tusubiri.... maana siku yenyewe ni leo.
P
 
Kuna wakati unapaswa kutii Mungu na sio mamlaka za kidunia. Ushahidi upo Kitabu chs Daniel ambao vijana watatu walikataa "amri halali" ya mfalme wa kusujudia sanamu. Walikubali kufa kuliko kutii amri ya mfalme ingawaje Mungu aliwaokoa na ghadhabu ya mfalme.
Hivyo, kwa sisi Wakristo tunaaswa kutii amri ile tu ambayo haiendi kinyume na maagizo ya Mungu.
Hao vijana watatu waliitwa Shadrack, Meshaki na Abidnego
P
 
Back
Top Bottom