Ujumbe Mahsusi Kwako Kiongozi Uliyesema Tusichanganye Siasa na Dini.

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,802
71,229
Ujumbe muhimu kuwafikia viongozi wa juu Wastaafu na walio madarakani juu ya dhana ya kuchanganya dini na siasa kama nilivyoukuta mtandaoni. Somo tosha;

*******

Kuna tofauti kubwa kati ya kuchanganya dini na siasa na kuchanganya imani za kidini na siasa. Yenye madhara ni kuchanganya imani za dini na siasa. Dini ni vyombo vinavyolea wanasiasa na kuwaandaa kuwa waadilifu, wenye kujali utu. Dini zinawaandaa wananchi kuishi kwa amani ni upendo. Katika matamko yaliyotamkwa ama nyaraka/waraka zilizotolewa sijaona wala kusikia mathalani viongozi wa dini wakisema ama kuhamasisha utii wa mambo yanayohusu misingi ya imani zao bali mambo yote ya msingi yahusuyo mustakabali mwema wa Taifa. Wanaosema tusichanganye dini na siasa wanasahau kwamba wao ndio wanaingiza imani zao kwenye siasa jambo ambalo si jema. Dini ni taasis zinazojumuisha watu wenye mamlaka tofauti ndani ya serikali, wakiwamo wanasiasa, kamwe haziwezi kukaa kimya pale viongozi wenye dini wanakiuka misingi ya utu, amani, utawala bora, ulinzi wa raia na raslimali za taifa. Kufanya hivyo kutakuwa hakuna maana ya uwepo wao. Hakuna mpaka wa utengano wa wajibu na uhusiano wa dini katika siasa. Wapotoshaji tu ndio wataamini kwamba kukemea maovu kunakofanywa na viongozi mbalimbali wa dini ni kuchanganya dini na siasa. Na hiyo ni ishara ya UBINAFSI na WOGA. Msituchanganye jibu hoja.

Msituhitilafishe wala kutufarakanisha kwa maslahi yenu binafsi. Kuna Heshima kubwa sana kwenye kukiri na kukubali kutenda makosa na kuomba msamaha. Wahenga walisema "Kiburi si maungwana" na mchelea mwana kulia hulia yeye" viongozi wa dini wametekeleza wajibu wao, kazi kwenu. Binafsi nimawaelewa viongozi wa dini. Na sasa ninaendelea kuwalewa vizuri watawala wetu.

Tunapoingia kwenye uchaguzi hasa wa Rais mara kadhaa hekima imesukuma kuangalia usawa wa mabadilishano ya utawala, kama sikosei uwino wa mbadilishano wa mamlaka kuu ya nchi huangalia dini, ingawa sio sheria bali ni msukumo wa hekima, ninataka kujiuliza Rais wa kwanza alikuwa Mkristo, wa Pili akawa Muisilam, wa tatu akawa mkristo wa nne akawa Muislam wa Tano akawa mkristo sasa sijui huyu wa sita ni dini gani? Sijui kama mnanielewa sawasawa? Niwasihi ndugu zangu wananchi Mwenyezi Mungu ameruhusu dini ziwepo ili apate kutuzwa, na waliomo katika dini hizo wanaitwa nankufanyika viongozi. Kuwa kiongozi wa kisiasa kamwe hakukufanyi upoteze imani yako? Na wala hakukufanyi usionywe na kusolewa na viongozi wa dini. Kuwa mtawala hakukupatii kinga ya kuelezwa makosa unayoyafanya, wala haiwazuii viongozi wa dini kukueleza ubatili unaoutenda. Viongozi wenye hekima hupokea laumu na makosoo kwa hekima na kuyatendea kazi kwa saburi.

Mungu awajaalie viongozi wetu wa kisiasa na wa dini kuwa na hekima, saburi na weledi wanapoingia katika changamoto. Awajalie weledi wa kutambua ni wakati gani wanajaa kiburi na kuomba neema ya kuwa wanyenyekevu. Maana katika unyenyekevu mwaketi hekima, saburi na uelewa.

Credit to; Gaspar Mwanalyela.
 
Jk atuachie taifa letu GSM,lake oil na.........hazikutoshi
 
Jk Alishamwambiaga Kuwa Tutume (yaani Yeye Na Wa Kwenye 50), Usipotutumia Basi,sasa Mama Kaingia King,kumbe Alikaribisha Nzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom