Sio mpenzi wangu lakini kaninunia sababu nimeshindwa kumkopesha pesa

Sensei Tai

Senior Member
May 26, 2022
126
359
Kuna binti mmoja nilipata kujuana nae baada ya kukutana kwenye kazi ya muda ambayo tuliifanya kwa muda wa miezi 6.

Baada ya ile kazi kuisha kila mtu aliendelea na harakati zake zingine lakini bado tulikuwa tutawasiliana mara mojamoja.

Kuna siku alinitumia link ya group la ajira lakini nikamwambia kwasasa mimi nimeshapata sehemu ya kujishikiza na nikamtajia jina la kampuni.

Kwakua nilitoka kwenye msoto madeni nayo yalikua mengi, sasa ile mwisho wa mwezi ulivyofika tu akanambia nimuazime Tsh 50,000.

Nikamwambia kiukweli bajeti yangu haipo vizuri mana nimepata mshahara lakini karibu asilimia 65 nimelipa madeni ya watu, akaitikia sawa "hamna shida", lakini kiunyonge flani akiamini ninayo ila nimemnyima makusudi.

Baada ya kama siku tatu nikasema ngoja nijaribu kumjulia hali nione reaction yake, bwana weeeee kaisoma tu sms yangu Whatssap na imeonyesha blue tick lakini wala hajahangaika kuijibu hadi leo.

Sasa nikajiuliza kwanini hawa wenzetu hawaamini kwamba na sisi kuna muda tunakosa pesa, tena ukizingatia sio mpenzi wangu na sijawahi hata siku moja kumtamkia kwamba namtaka kimapenzi?

Mtu kama huyu hata ni ningemuazima kweli si angeingia mitini na hela yangu, maana pia wataalamu wa haya mambo wanakwambia mwanamke hakopeshwi.

Je, wewe mdau wa JF ulishawahi kutana na mtu wa namna hii?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom