Alijisemea mchungaji wa kanisa flani maarufu la KKKT.... Watu wanadhani ukiambiwa usizini ni kwa sabbu ya magonjwa ya zinaa, sijui Ukimwi... Sio hayo tu. Uzinzi ni mlango mkubwa sana wa shetani kumshambulia mtu ama familia nzima. Hasa eneo la afya na uchumi.
Unaposex na asiye mke wako, kuna spiritual transaction inafanyika. A.k.a utabeba kila tatizo la huyo mwanamke ulielala nae kuanzia kizazi cha nne mpaka kufikia yeye. Yani kama babu yake alikua mwizi..umebeba roho ya wizi, kama mama yake hawakusoma kwao..au walikataa shule..unaibeba ile roho..unashangaa watoto wanadeteriorate kwenye elimu, kama baba yake alitapeli watu..kazi zako utafanya na hutaona faida...yani umejifanyia muamala wa matatizo na uchafu wote...
Ukibisha sitashangaa...lakin nikuulize..hujawahi ona mtu kaoa mwanamke afu anapata mafanikio...kwa sabbu huyo background iko njema na ukichunguza upande wa huyo mke wake yawezekana kuna aliyesimamaga katika imani kuvunja na kuharibu maroho yote ya kurithi na yawezekana huyo mwanamke pia ni mtu wa kusali ama kuswali.
Sasa wewe mwenzangu na mie hurogi, husali afu unat***a ovyo...kusudi la kuumbwa unaliacha unafata tamaa. Nakwambia ni lazima uharibikiwe tu. Nikitazama mifano michache ya baba zangu kadhaa..ambao walioa mke mmoja lakini wakaja kuchepuka...na kupata hata mtoto nje...walileta ukame kwenye familia sana. Tena ukame haswa. Maisha yalikua magumu, kula kwa tabu..shule tukasoma kibishi. Mpaka mama zetu walipoumia sana...wakaombana msamaha..wakaamua kutulia, na mama zetu kusali sana....ndo Mungu akaondoa utasa wa kiuchumi kwenye familia zetu..ndo atleast kuna ahueni.
Tukirudi kwa babu zetu...walioa wake wawili wengine watatu...lakini nikiangalia trend...wake wa pili na kuendelea....watoto zao...no direction. Wameish maisha ya kanyaga twende..bora liende...mbaya zaidi wakazaa nyumbani, na watoto wao wakazaa nyumbani...no blessings...ni wachache sana waliofanikiwa na hao waliamua kuutafuta Uso wa Mungu na kuomba toba ili Mungu asamehe ule uovu.
Kwahiyo am not saying itaapply kwa wote...lakini ni heri kutembea katika njia za Mungu kuliko kufatisha namna ya dunia hii....unless uwe mwanga...lakin wewe mwenzangu na mie pesa ya tabu bado unaenda kuichuma laana nyingine hasa kama mke wako kasimama katika haki, mmechuma nae mafanikio na alikua na wewe tangu mwanzo..afu unajitetea tamaa akati yeye katulia..huyo mama akidondosha chozi...sisemi kitu!! Pima haya maneno kama si yako wewe pita. Kama ni yako..jifunze kitu!!
#em nikanywe zangu supu#