Sinopharm inavyochochea uhusiano wa China na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1665537410497.png

Uhusiano kati ya China na mataifa ya Afrika una miaka zaidi ya 60 sasa, msingi wa uhusiano huo ni urafiki wa kindugu, na mara kadhaa China huitaja Afrika au waafrika kama marafiki wa kweli.


Unaweza kusema uhusiano ulianza miaka ya 1960, baada ya takribani nchi 10 za Kiafrika kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Umma wa China na nyingi zilikuwa ni zile zilizofuata siasa za mrengo wa kushoto zikiwemo Algeria, Misri na Guinea.

Katika miaka mitatu iliyopita baada ya mlipuko wa ugonjwa wa uviko-19 ambapo mahusiano ya China na Afrika yaliimarika zaidi katika nyanja ya matibabu, ulikuwa ni wakati mgumu kwa dunia nzima na mataifa yanayoendelea yalikuwa njiapanda.

Sinopharm ambayo ni wazalishaji wakubwa wa chanjo za Covid-19 ilitoa mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano huo. Mkuu wa Kampuni ya Sinopharm Bw, Zhu Jingjing amesema, "Wakati wa vita dhidi ya Covid-19, Sinopharm ilichukua jukumu kama njia kuu ya misaada ya nje na usafirishaji wa vifaa vya matibabu, ikitoa zaidi ya bidhaa bilioni 3.3 za vifaa vya kupambana na janga kwa nchi na maeneo 170."

Alisema kampuni hiyo inafanya sambamba na maono ya Rais wa China Xi Jinping ambaye mara zote amekuwa akisisitiza kutoa kipaumbele kwa maisha ya watu.

Wakati wa mkutano baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wangi Yi alisema hadi kufikia Agosti mwaka huu China ilikuwa imetoa msaada wa dozi milioni 189 kwa nchi 27 za Afrika na kushiriki katika ujenzi wa kituo cha kutengeneza chanjo ya ugonjwa huo chenye uwezo wa kuzalisha dozi milioni 400 kwa mwaka.

Hata hivyo Mkuu wa idara ya kimataifa wa Sinopharm Zhou Song alisema ushirikiano kati ya Sinopharm na Afrika hauko kwenye chanjo pekee, bali kampuni hiyo imekuwa ikiuza bidhaa katika mataifa mbalimbali pamoja na kunoa wataalamu wanaotoa huduma za afya, hata hivyo alisisitiza kuwa ushirikiano huo utaongezeka katika siku zijazo.

“Hatutoi chanjo tu, tunauza dawa nyingi na vifaa tiba kwa nchi za Afrika lakini pia tunashirikiana katika utaalamu, kuna watoa huduma wanaokuja huku kufanya kazi nasi, nasi tunatuma watu wetu kwenda kufanya kazi katika nchi zao ili kubadilishana ujuzi,” alisema Song wakati wa matembezi ya waandishi wa habari kutoka mataifa tofauti yakiwemo ya Afrika.
 
Africa tunapaswa kujifunza thamani ya unafiki kwa maslahi ya mataifa yetu ona wachina wanafuatilia kwa karibu matatizo yetu wanajitokeza kutupa misaada ya laki moja Kisha Wana chukua cashi ya milioni alfu moja
 
Back
Top Bottom