Singo nyingine ya TANESCO! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Singo nyingine ya TANESCO!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kipis, Sep 27, 2011.

 1. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimesikitishwa sana jana na kauli ya tanesco kuhusu huu mgao wa umeme usiojulikana kikomo chake.

  tanesco inawashangaa wananchi kwa kuwatupia wao lawama kuhusu mgao wa umeme,bila kujua nani anasitahili kutupiwa lawama hizo.

  kwa mujibu wa maelezo ya tanesco kwa wananchi,wanadai eti wao kwa hili hawapaswi kulaumiwa badala yake pan africa ndio wanaositahili kulaumiwa kwa hili.7bu eti pan africa ndio wasambazaji wakuu wa gesi hivyo kiwango cha usambazaji kimepungua hivyo kupelekea kupungua kwa uzalishaji wa megawati kwa songas hali inayopelekea mgao kuongezeka badala ya kupungua kama walivyokuwa wameahidi.

  hivyo wananchi tuache kuilaumu tanesco katika hili kwani wao hawahusiki. Habari hii ni kwa mujibu wa badra masoud.
   
 2. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Walio tuita wadanganyika walikuwa sahihi kabisaaa
   
 3. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nilimsikia huyo Badra jana akizungumza ktk kipindi cha jahazi clouds fm, eti PanAfrica linapotokea tatizo nao watoe matamko kwa linalo wahusu coz ati yeye amechoka kila siku kua ni m2 wa matamko tu na malawama!
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kwa serikali ya ccm ubabaishaji, wizi, ulaghai ni kama chumvi kwenye chakula. wametuhadaa kupitia bunge na kupitisha bajeti ya trilioni na ushe! halafu bado tupo gizani, malalamiko yetu halali yamewatia hasira ccm wameingia mikataba bomu, wamechota mapesa yetu, wanatupiga danadana kwa matamko.
   
 5. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mambo ya Wizara hii ukiyazikiliza au kuyawekea maanani unaweza kuishia MILEMBE, nataka niwaulize wahusika wakuu: Hivi hiyo GAS ya Mnazi si ilivumbuliwa na Wahindi kwenye mwishoni mwa miaka ya sabini na baada ya kuchimbwa sijuhi kulitokea nini hikalipuka na kuwaka miaka nenda rudi bila kuzimwa - sasa hawa wazungu walipata vya mtelemko hawakuangaika chochote kutafuta GAS walishajuwa pa kuipata, mimi ninacho jiuliza siku zote ni kwa nini TPDC haikupewa nyenzo na Serikali yetu hata kama ni kukopa hili waweze ku-exploit na kusambaza GAS wenyewe bila ya kuingiza hawa watu wanyonyaji wakubwa, leo utahambiwa GAS ina uchafu, kesho mitambo ya kusukuma hiko-down, keshokutwa -wanafanyia maintenance mitambo yaani hawana contigency plan yoyote ya kuhakikisha GAS inapatikana 24/7 je hii ni bahati mbaya? Jibu ni hapana inawezekana kabisa wakawa wanatuwekea mikwala tu kwa kuwa wana-monopolize nishati hii muhimu nchini, wizara yetu inawezaje kuwa-blind kwa kutogunduwa mapema kwamba kitu muhimu kama GAS haipashwi kupewa hiendeshwe na watu ambao hawana uchungu na nchi hii, wizara/serikali ilichotakiwa kufanya ni kuwambia wafunge mitambo ya kusukuma GAS alafu waondoke ZAO wawahachie TPDC, damn! unahambiwa eti tunawalipa sijuhi kiasi gani (wameweka tarrif kubwa kupindukia) kwa kutumia GAS ( our natural resource) as if wametoka nayo Ulaya/Merikani na sisi tunakubali tu kama watu walio run bankrupt of REASONING!

  Mambo ya nchi yetu yanavyo endeshwa wakati mwingine yanashangaza sana, wizara hiyo hiyo unasikia waziri anasema hili na naibu wake anasema kitu kingine na k/kuu yake mtu unashindwa kuelewa kwamba hapa kuna-collective leadership kweli! Je na hilo JK anapashwa kuingilia kweli? utakuta wanachangamkia sana maswala ya kuagiza mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme kwa kuwa kuna bila shaka vested interest wanaunguza fedha chungu nzima za walipa kodi na hawajali, JK aliwahi kuwashauri wabadilishe mitamba ya IPTL itumie GAS badala ya mafuta mazito, kwani kuna aliyemsikiliza - JK siyo mwana sayansi lakini huwa ana uwelewa mkubwa katika mambo haya nadhani aliwahi kusoma physics, ah lakini Economics ni kama sayansi tu. Kitu gani kiliwafanya kupuuzia ushauri wa JK na kutoa visingizio chungu mzima katika eti gharama ya ku-modify mitambo itumie GAS - siyo wakweli na jibu la kuweka mikwala unalo..

  Hizi hela zinazo tumika kununulia mafuta haya kila mwezi ni kiasi gani - je hapo wizarani kuna aliyewahi kufikilia kwenda DRC kuangalia Mitambo yao ya kuzalisha umeme ya INGA nasikia inazalisha umeme in terms of GIGAWATTS sisi tunabaki kulia lia na kutoa press release kuhusu a dismal 100MW genarator ambayo ni tone kwenye bahari ukilinganisha demand halisi ya umeme katika nchi hii - ukosefu wa ubunifu ni kitu kibaya SANA.

  Hhivi mkimuomba Kabira mkaunganisha Grid yao na ya kwetu kupitia a marine cable lake Tanganyika kuja Kigoma alafu ifungwe kwenye Grid ya Taifa, hivi gharama zake zinaweza kushinda gharama ambazo mtatumia kwa mwaka kuagiza mafuta mazito ya kufua umeme, nina uhakika kama mgetoa wazo kama hilo kwa wafadhili wangetoa msaada mara moja, lakini waswahili hilo hawataki wanachotaka ni kuhunguza fedha za kigeni kwenye mafuta mazito ya mitambo kwa kuwa kuna maslahi binafsi.
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,088
  Likes Received: 6,554
  Trophy Points: 280
  ni wahuni tu hawa wote
   
 7. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ...mimi nimechoka na hiyo ngo tanesco,kwangu nyaya zao naanikia nguo,sitakiiiiii kusikia habari zao...hii itanisaidi kusihi muda mrefu hata kama ni kwa giza
   
 8. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na tukidanganywa tunaridhika
   
 9. u

  utantambua JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aache kazi kama amechoka, alaaaaaaaa
   
 10. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #10
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanatangaza mgao lakini bado wanaleta mabill makubwa kweli kweli, SIPENDI HATA KUONA HILI JINA TAA NESKO
   
 11. M

  Mwana wa Kitaa Member

  #11
  Sep 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao Pan Africa kwanini nao wasiongee? au ndio kusema hawana msemaji?
   
 12. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tanesco bado wanawajibika kutoa taarifa kwetu kwakuwa sisi ndi wateja wao, sisi ndio tuna mkataba nao.

  Hao pan african energy hatuna mkataba nao, wao wana mkataba na tanesco kwahiyo hawawezi kutoa taarifa kwetu wanatoa kwa tanesco.

  Ila kiukweli siku ikitokea tanesco imekufa ama imebinafsishwa ama kupewa mshindani ndipo tutaweza kupata umeme wa uhakika lakini tukiendelea na tanesco hii na katika mazingira haya, wanazidi kutuchefua tu na kutuongezea machungu.
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  bora nipige kimya maana. . .
   
 14. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kwani wameajiriwa/mkataba wao wameingia na nani?? -kaa siyo taanesco
  na kama tanesco sio wasimamizi wakuu wa nishati tz waseme tuanze kulalamkia hao pa
  shenzi kabisa wanafki tuuuu ss tulisharidhika wao watangaze tuu ratiba ya kueleweka
   
 15. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Nimepewa likizo na daktari nisijadili maswala ya nchi hii. Nitaishi MIREMBE.
   
 16. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  nadhani hata wananchi tuna matatizo ya kisaikolojia ambayo aidha tumeyapanda wenyewe au yalipandwa kwenye mioyo yetu na wachache wetu ili watunyonye, haiwezekani na wala haiingiii akilini hata kidogo tunachezewa hivi kama vile mtu anacheza na nywele zake za kwapani, anazishika, anazinusa, anazivuta kidogo, anafikiria lini azinyoe au azipige maji kidogo ziache kunuka! Yaaani mtu kweli anathubutu kusimama kwenye hadhara na kutangaza upupu kama huo na tumemwangalia tuuu? yaani kweli mtu anaenda FB anaandika upupu na baadhi yetu tunasema ndio mzee umepatia kabisa? No, I call upon you brethren, tufanyeni namna fulani ya kuwakumbusha hata kwa kuwatekenya tu, naombeni mwongozo naona ule wa October 2 bado hautawaaamsha sana
   
 17. M

  Mocrana JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  eeeh jamani Tanzania nani amekuroga aaarhg
   
 18. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #18
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Waungwana,

  Mtaniwia radhi. Hivi kweli kama sisi ni watu makini, kwa nini tunajisumbua kulalamika kuhusu kushindwa kwa TANESCO kumaliza tatizo la mgao wa umeme? Kwani nani alisema kwamba TANESCO peke yao ndio wenye dhamana ya kuzalisha umeme? Kwani nani amekuzuia wewe kuweka mtambo wa wind power, au solar power, nyumbani kwako, ukaachana na huo mgao?

  Jamani, kama sisi ni watu makini, tutajua kwamba ni kazi bure kuilalamikia Serikali na TANESCO. Dawa ni (1) funga mtambo wako mwenyewe wa umeme nyumbani, kama ni wind, solar, bioga, etc., kisha (2) ng'oa kabisa service line ya TANESCO, ili uachane na dhana kwamna TANESCO ni kampuni ya kuzalisha na kusambaza umeme, kwani hilo si kweli.

  Hata kufikiria mambo madogo kama haya, tunaiachia Serikali? Ujinga huu!

  Samahani kwa kuwaambia ukweli lakini TANESCO SIO SOLUTION ya kumaliza mgao wa umeme, na hata Serikali pia, haina nia hiyo.
   
 19. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  PAN AFRICAN ENERGY is the one owning our gas and is the one with authority to accept who should buy (in large quantities) and who should do the gas biz. Above all IT'S THE ONE LIMITING ANY USEFUL DEVELOPMENT IN NATURURAL GAS USE.-Source; I went to them personally like 3yrs ago.
   
 20. m

  massai JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  janja yao hiyo yakitoto sana,hivi hile hela ya dharura imebaki kiasi gani???wanasubiri mvua zianze ndipo wapate sababu ya kujitetea.Mimi ninachotaka kujua ni zile hela za dharura zimetumika lini na wapi na kwa matumizi gani coz umeme hatuku uona mpaka leo......na watatudanganya kua zzilitumika.huyo badra ajiandae kutupa majibu y msingi.
   
Loading...