snowhite
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,422
- 25,338
Namkumbuka sana huyu mfanyakazi mwenzangu wakati huo.Ilikuwa ni mwaka 1998 wakati nilipokua nafanya kazi pamoja nae,na ni mwaka huohuo alipata matatizo kazini yaliyopelekea kuyavuruga maisha yake kwa muda
'
Wakati mimi nakwenda kwenye kampuni ile nilimkuta na ni mkubwa kwangu kiumri,jamaa yangu huyu alikuwa ni mpenda starehe na wanawake,lakini pia alikua na mtoto wa miaka minane na alikua ameoa,kitendo chake cha kupenda starehe na akina dada kilipelekea akala fedha za kampuni kitendo kilichosababisha asimamishwe kazi na baadae kufukuzwa kabisa
'
Kampuni iliamua kuchukua chochote alichokua anamiliki ikiwa ni pamoja na samani alizokua nazo alipokua amepanga.Maisha yakawa magumu sana
'
Mkewe alifariki kwa ajali ya kugongwa na gari kitendo kilichomchanganya sana jamaa yangu huyu akawa kama amerukwa na akili,chakula cha kula yeye na mwanae kikawa tabu kupatikana
'
Siku moja akiwa mwenye mawazo mengi huku machozi yakimtoka bila kujijua,mwanawe akawa amelala kwenye box ambalo ndicho kilichokuwa kitanda chao aliamka na kumwambia baba yake maneno yafuatayo;
'
"Baba mama ameniambia usingizini kuwa amekusamehe kwa uliyokuwa unayafanya,ameniambi nikuambie hayo na amesema pia ufanye kazi na kumuomba Mungu ili maisha yawe mazuri na zawadi pekee utakayompa ni kuyabadili maisha yako"
'
Jamaa alijikuta analia kwa sauti mbele ya mwanae wa kike kwa uchungu
'
Kwa nguvu aliyopata siku ile alijituma sana na amefanikiwa kujenga nyumba mbili na ni mfanya biashara ya vipuri vya magari,mwanae yupo mwaka wa pili SAUTI
'
Nimekupeni kwa ufupi sana uzoefu wa single parent huyo ili mjifunze anglau kidogo.Najua sio jambo dogo mzazi mwenzako akuache na familia,iwe kwa kifo au kukukimbia lakini fahamu kuwa UNAWEZA kuishi na ukayabadili maisha na kuwa mazuri zaidi
'
Usijilaumu au kujilaani kwa lolote,jifunze kupitia makosa,hakuna asiekosea,songa mbele
'
Kama mkeo/mumeo amekukimbia na amekuachia watoto,usiogope wanao watakua baraka kwako,songa mbele
shikamoo shemeji!nakuamkia tuu!MUULIZE Dark City kwanini!lol
Last edited by a moderator: