Single mums and dads come this way

Kuna kitu nlisikia siku moja. Dada mmoja alisema hawezi kwenda sehemu na mumewe, the guy is no presentable enough to go out with her. Niliwaza sana. Inawezekana mke/mume anaishi na mwenzake lakini hata kutoka nae kwenda kwa mangi kununua sukari hawezi.
 
Sijaona sababu ya wewe kukasirika...
Kulea mtoto hakukupi haki ya kuwa baba yake..

Baba atabaki kuwa baba...mjomba atabaki kuwa mjomba...

 

wengine wanaolewa kwa kulazimishwa ndo kama hivyo ndoa inakuwa ndoano
 

Kama hujajua nachojaribu kukueleza basi mama, sina maneno mazuri zaidi. hizo restrain orders kwa nchi ninayoishi mimi ya Kusadikika hazipo au hakuna mazingira wezeshi. Kwa hiyo kwa kuwa tunaishi kwenye jamii 2 tofauti tukubaliane kutokubaliana.
 
Ndo kama hujui huna cha kudai,asiyekuwepo na lake halipo!Madhali kama mtu amesimama na kusema anazuia mawasiliano na ana sababu za msingi inabidi tuheshimu maamuzi yake kwasababu hatujui lolote kuhusu mahusiano yao mpaka wakafikia hapo!Unafikiri yeye hajui kama mtoto wake anatakiwa awe na father figure?Nadhani si rahisi kwa muhusika vilevile kupitia hayo.Na mpaka amepata guts za kusema ujue ni pride aloisimamia!
 
wanaume mara nyingi ndo wanakana mimba na single dads wapo ila wachache sana

Kuna dada namfahamu, aliacha watoto wake wawili sehemu, mmoja akiws 3yrs na mwingine 1yr hadi watoto wakasahau kama Kuna mama. Hadi wapo 23 kwa 21 ndio amewaona. Na believe me...hawataki hata kusukia kuhusu mama Yao. Haya mambo hapo kwa jinsia zote.
 
Sasa nimekuelewa, kuna mahali uliwahi komenti nikabaki :wacko:!!! Sikupi pole kwa kulea wala, maana sioni umepungukiwa, labda kwa kuondokewa na mwenza.
Kongosho haya Bwana,kulea kazi jamani halafu wanangu wako 6,3 na 2yrs,nipe pole mwenzako.Ila maombi ni silaha
 
Mkuu wangu hii kitu nimeishuhudia kwa macho yangu.Kipindi nafanyakazi shirika moja la umma kijana mmoja umri kama miaka kumi na nne / kumi na tano wakati huo kaagiziwa na Mama yake (kilimanjaro) sehemu Baba yake anapofanyakazi bahati mbaya siku hiyo (Baba mtuhumiwa aliaga anakwenda bank) tuna share ofisi moja walinzi walipopiga simu nikapokea wakanieleza kuna kijana anataka kuonana na fulani nikawaambia wamruhusu aje amsubiri ofisini kijana akaingi kanisalimia vizuri nikamkarisha kiti nikamweleza anayemtafuta kaenda bank atarejea baada ya dk 10.Kweli after 10 minutes jamaa kaingia ofisini nikamweleza ana mgeni wake wakasalimiana Kijana bila kupoteza muda akaanza kutiririka sababu zilizomleta Arusha duh Baba mtu akamtolea nje na kumweleza Mama yake ni mwongo yeye hausiki kabisa na akamwomba kijana aondoke wala asirudie tena kumfuata futa.Sitakaa katika maisha yangu nisahau huo mkasa basi kijana akanyanyuka kwa unyonge akaomba nauli ya kurejea Moshi Baba wa hiyari akakataa kutoa nauli ikabidi niingilie kati nikampatia nauli kijana akatokomea zake.

Baada ya kama miaka 8 - 9 kupita tangu tukio hilo litokee (shirika la umma lilikuja kufa kila mtu akashika hamsini zake) siku moja nipo mitaa ya Arusha City Parks napata moja moto moja baridi nashangaa natelewa bia 5 kwa mpigo nikashtuka nikamuuliza muhudumu kulikoni akaniambaia kuna jamaa kaniambia nikuletee hizi bia nikajisemea huyu lazima atakuwa katoka Merereni ndio wenye tabia hizo basi nikamwambia muudumu mwambie asante.Wakati naendelea kupambana na bia akajitokeza kijana aliyeninunulia na kujitambulisha kwangu na kunielezea lile tukio na jinsi nilivyomwokoa kwa kumpatia nauli kwani hakuwa anamjua mtu yoyote Arusha kipindi hicho.Si kwamba nilifurahi tu bali machozi ya furaha yalinitoka kwasababu kwanza kijana maisha yamemyookea haswa ni IT manager wa organisation ya kimataifa.Nikimtazama anafanana na Baba yake kila kitu nikajiuliza hivi sisi wababa tuna laana gani unawezaje kumkataa mtoto wako kisa unataka kulinda ndoa yako au usionekanane zamani ulikuwa mwingi wa habari.Unajua wengi hapa jamvini mmeshindwa kumwelewa Kilaza lakini ni bora usitie neno kama hujui machungu aliyokumbana nayo.

 
Last edited by a moderator:
Wanaotupa watoto wachanga ama kukana mimba hawajui kama si sawa? Kwa nini wanafanya sasa? Kuna justification?


Pride yake si lazima iwe pride ya baba/mtoto.

 
Pole sana mumie,Mungu akupe nguvu za kulea wanao wawe watu wenye hekima na busara!Watu wengine hawaelewi kabisa ni uzito mkubwa kiasi gani alokuwa nao single parent.Wanachukulia rahisirahisi sana na inakera!
Ni kazi hasa,yaani ila ile kuwa watakua,hata mimi nilishawahi kuwa mtoto ndo huwa inanitia moyo sana
 

mkuu ngongo huyo dogo alishawai kukutana tena na huyo kiazi aliyemkana

hahaha nauhakika mzee sasa hivi kiroho kinamuuma
 
Last edited by a moderator:
Wanaotupa watoto wachanga ama kukana mimba hawajui kama si sawa? Kwa nini wanafanya sasa? Kuna justification?


Pride yake si lazima iwe pride ya baba/mtoto.
Dhiki ndo inawatuma kwani we unaonaje?maana sasa tutatoka nje ya mada!!!
 
Ha ha ha ha ha Baby class hakutaka kumwona, std 1 -I - VII hakutia pua,form I - IV hayupo V - VI bado hajaamua kama mtoto ni wake chuoni mwaka wa pili ndio anajitokeza na kujifanya kuulizia mahitaji ya mtoto ?.Nilimtukana sana Dada yangu kwa upumbavu wa kubabaikia wajinga wajinga.

Sijaona sababu ya wewe kukasirika...
Kulea mtoto hakukupi haki ya kuwa baba yake..

Baba atabaki kuwa baba...mjomba atabaki kuwa mjomba...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…