Wakuu kwema?
Huu uzi ninauandika huku nikiwa na maumivu makali ya nafsi yaliyosababishwa na (single mother) Miezi kama 7 iliyopita kuna (single mother) nilimpenda na nikajua sasa hapa nimefika mwisho wa safari yangu ya kusaka mke. Kiukweli mwanzoni hata yeye alikuwa haamini kama kweli nimempenda na nia ya kumuoa.
Alifurahi na kunionyesha upendo. Kama mwezi mmoja hivi umepita ndo kaanza kutia supu nazi. Mawasiliano yamekuwa shida na pia kanipa taarifa rasmi kwamba tuwe kwanza marafiki kabla ya kuoana maana hayupo sawa kisaikolojia kwa sasa. Nikashtuka na kujiuliza hii kuwa marafiki si ni sawa na kurudi mwanzo maana tulishafikia hatua ya kupanga tuoane lini?Kuna wazo linanijia kwamba labda jamaa aliyemzalisha karudisha majeshi. Nimemuuliza kakana na kudai ni mambo yake mengine tu.
Wakuu nionavyo mimi hawa (single mother) kuwa nao kimahusiano lolote laweza hasa kurudiana na jamaa yake wa mwanzo. Ukiwa na (single mother) jua suala la gia kubadilishwa angani sio geni.
Nishaurini huyu mwanamama nimvumilie hadi hapo atakapokuwa sawa kisaikolojia au nipite zangu hivi?