Single Mother Waheshimiwa. Tyler Perry kasema nusu ya changamoto zao

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
168
Reaction score
281

Huhitaji utajiri Wa pesa kuelewa maisha ya mwingine Bali upendo ndio daraja pekee la kuokoa maisha ya mwezako anayepitia nyakati Ngumu.

Nimetazama filamu ya Straw kutoka Tyler Perry nimeona picha ya ndani wanayopitia single mothers tuache kuwakebehi kwa lolote hasa pale ambapo huwezi kumpa msaada.

Nimejifunza, msongo Wa mawazo uliopitiliza ni hatari. Mwana mama mtoto wake Aria alishakwisha fariki lakini aliishi Kwenye ndoto za mchana Hali iliyomfanya kuchanganyikiwa. Hapa Cha kujifunza ni lazima mtu ujifunze kukubaliana na nyakati Ngumu ili kuepuka kuingia katika msongo Wa mawazo ambao ni hatari kuliko Hali yenyewe na mnaona kabisa fujo alizofanya mwishowe akiwa tayari amechanganyikiwa.

Pili, Kila jamnii watu wema wapo, mpelelezi Nicole na Meneja wameonyesha picha hii. So, ukiwa katika Hali Ngumu usidhani binadamu wote wabaya amini kwamba Kuna ambaye atakusikiliza na kukuelewa.

Niwaambie kuwa zawadi pekee unayoweza kumpa mtu mwenye maumivu ni kumsikiliza.

Tatu, tusiwadharau single mothers kwa malezi ya watoto wako aisee wanapitia magumu lakini wanajitahidi sana kuonyesha na kutoa upendo kwa watoto wao. Kama mwanaume unaweza kumsaidia bila kuhitaji chochote basi fanya hivyo.

Lakini mwanaume kama umemwacha mtoto na Bado upo hai hapa Dunia huku mama akiteseka aisee!! Rudi ukatubu na uwe Kwenye maisha ya mtoto wako.

Hapana Tanzania naona utani na dharau nyingi sana kwa single mothers kupitia mtandaoni. Wengine wakiwakashifu na hata kutoa Elimu ya kwamba hawafai kuoa na usijaribu.

Acheni jamani narudia acheni na kama huwezi kumpa upendo Wa dhati usimtukane Wala usimdharau kwani wanayopitia ni mateso tosha kiakili na kimwili.


Nahisi tatizo alilopitia Janiya na kazi alionyeesha Tyler Perry ikawa sehemu ndogo sana ya matatizo wanayopitia single mothers Kwenye jamnii zetu hasa Tanzania ambao uhuru Wa kuongea bila kujali maneno kama silaha hatari umepitiliza Wa kuendelea kuwaumiza wanawake.

Mwisho, single mothers wanahitaji upendo, kusikilizwa na kuheshimiwa ili waweze kukuza kizazi Bora na pia kuwa salama kiakili kwa ajili ya maisha Yao.

Pia, Serikali iongeze sheria Kali Kali katika malezi ya watoto kunusuru jamii ili wanaume wanaokimbia watoto wawajibishwe vikali.
 
NIpo nasoma uzi huku nasubiri jamaa wa Car wash amalizie kuosha mkokoteni wangu ili nianze pilika pilika za kusaka chapaa.
 
Pole Sana single mother
 
Nyuzi kama hizi uwezi mkuta Lucha
Lucha yupo kwenye uzi wa vita..

Na yeye ni furaha tuu mda wote anakwambia Israel inateketea moto 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

mfatilieni lucha wakuu mtagundua kitu
Kuna kenge mmoja Lwiva ni misogynist ,yeye stori zake ni kuchezea wanawake tu ,mwana haramu kabisa huyu kijana.
 
Movie tu iyo, waswahili sana hal tatizo
 
Kusema ule ukweli , familia inahitaji stability ya nguvu angalau wazazi wawe pamoja mpaka kifo ,kuna mazingira yanahitaji sapot ya pande mbili.

Uncle wangu anayo pesa ila ni single fathers wa watoto wanne ,kazi ni umalaya tu . Ikitokea kwake amekuja hata mama yake kumuuguza basi anatafuta mtu kutoka mbali huko ili aje kukaa pale ili kupika ,siku za sikukuu watoto wake anawapeleka kwa mama zao .Kiufupi, kupata watoto kwenye familia ni nzuri zaidi.
 
Inashangaza sana mwanamke kuwa single maza!
 
Nilishasema mwanamke akishakuwa single mother akili huwa sio ya kwake kabisa,sasa ukijichanganya kumuao ndio akili itakukaa vizuri.Kama mke wako wa ndoa baada ya kuzaa watoto hali huwa zinabadilika na kufikia hata kujaza sumu watoto wako mwenyewe ili wakuchukie,sembuse huyu aliezaa na mwanaume ambaye alimkataa,na akamuacha na mtoto peke yake,na anajua kabisa huyu mtoto sio wako.Ukisoma nyuzi humu ndani wengi wanazungumzia uhalisia wa maisha waliyokutana nayo baada ya kuishi nao,achana na wale wanaotoa tu kejeli kwasababu ya hisia au kusikia kutoka kwa watu wengine......
 

Niliacha mke wangu Nina miaka 50 na watoto wa 4, iliniuma sana maana sikutegemea, alinidharau mno baada ya ( yeye mke wangu ) kutoka nje ya ndoa, na Mimi kujua.

Kama single Mother na x wife ni mmoja wapo, waache tu wayapitie Magumu kwa maana nikiwa na miaka 50 nililazimishwa kuanza tafuta mke.

Miaka yangu yote ya ndo nilikuwa nawahangaikia yeye na watoto wake, sikujifikiria, mwanamke single aisee kama wakwangu, mwache tu aendelee kutaabika!
 
Nusu kwa nusu,Yawezekana kuna tatizo kwa wanaume ,Lakini pia wengine hao single mother hujitakia hasa akiwa na kipato,haambiliki!
Mmoja ana injini 5 na kila moja ina baba yake huyu yupo Bukoba
Nikakutana na mwingine ana injini 4 na kila moja ina baba yake huyu yupo Dar
Nikakutana na mwingine ana injini 3 na kila moja ina baba yake mkoa wa Pwani
Yule wa Musoma mwenye injini 2 kila mmoja na baba yake mtoto wa Mchungaji mmoja maarufu ndio nilichoka kabisa

Bad enough wote kichwani km kuna nati zimepungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…