Single mother bana, tabu tupu

T A J I R I

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,671
3,388
Samaleko...

Hiki nacho ni moja ya visa vyangu kwenye harakati zangu za kumpata mtoto wa mama mkwe.

Kuna ka binti nilikutana nako miezi kama mitatu iliyopita. Siku ya kwanza tu nakaona nilipokasalimia tu, kalinichangamkia sana. Kakaniambia "ni kama nakuonaga maeneo flan" na ni kweli ndio maeneo niyoushi. Nikamjibu itakua kweli maana naishi maeneo hayo. Kwenye stori stori kumbe hakai mbali na ninapoishi. Basi tukabadilishana namba kila mtu kwao.

Nikatulia kama wiki kadhaa nikamche, just kumpa salam. Nikamuuliza upo wap? Akanijibu, kumbe anapofanya kazi nami huwa napita kila siku nikitoka kwenye mishe zangu jion. Basi nikamwambia naomba nisubiri nitakupitia hapo, akaubali.

Basi nimefunga zangu mida ya saa3 usiku nikamuuliza umemaliza kazi akajibu ndio, nikamwambia nakupitia, akajibu sawa. Kweli nikampita, nikampitisha mahala kupata dinner then kila mtu kwao. Siku ikaisha.

Sasa kipindi hichi sasa nikaanza kukathaminisha kama kanaweza nifaa kwenye nia yangu. Kimuonekano kakawa kanaingia, kanatoka. Nikajiambia anyway, ngoja nitupe ndoano huwezi jua pengine roho yake na treatment zake zinaweza nifanya nizame mazima. Wakati huu bado sijui kama ni ka single mother maana kalikua hakana muonekano wa kamba kalisha zaa na hakana smartphone, so sikua hata naona status zake whatsapp. Maana njia nyingine ya mkujua mtu ni kupia status anazopost.

Basi nikaanza kukasaundisha. Kakaanza kuingia lain. Jinsi nilivyokua romantic hadi kuna siku kakaniambia "yaani wanaume wengine jaman, unaweza hata wabebea mimba". Mimi bichwa hilo.

Basi life likaendelea, muda huu wote sijui kama ni ka single mother. Siku moja, nikasema leo nataka nijiridhishe na maisha yake. Nikamwambia atafute siku atakua na muda nimtoe dinner. Kweli akaniambia siku flan. Siku ikafika tukatoka. Basi ni msosi na soft drinks tu (situmii alcohol).

Kwenye mastori nikamtega akajaa. Akaanza kufunguka kuwa yy anamtoto wa kike alizaa na jamaa wa bukoba. Mtoto anaishi na baba yake bukoba. Nikamtega zaidi akaendelea kufunguka. Akasema, kuwa anampigia sim mzazi mwenzie anampa sim mtoto anaongea nae. Nikajiambia, hawa bado wana bondi inayoishi kabisa. Kwa kifupi nika conclude kwamba siku hio iwe mwisho wa kumfuatilia. Basi baada ya muda nikarudisha kwao maana anakaa na mama yake.

Sasa wiki mbili zilizopita nilimuona maeneo flan mida ya saa3 asubuhi ila yy hakuniona. Ilipofika saa5 nikamtext, nimekuona maeneo flan sijui ulikua wewe. Akasema ndio ni mm. Nikamuuliza hujaenda kazini? Akajibu sijaenda, ninasafari ya bukoba leo naondoka na magari ya saa7 yanayotoka dar. Nikamwambia safari njema. In short nilihisi kabisa anenda kwa mzaz mwenzie. Sasa kipindi hichi kesha nunua smartphone.

Kweli alisafiki. Picha likaanza kwenye status. Mara ampost mzazi mwenzie na caption like "asante baba kwa kunitunzia mwanangu" yaani ni post za mzaz mwenzie like bado wana uhusiano. Muda huu mm nilishasitisha zoezi, so nothing to complain.

Ninachota kuwaambia, kuoa single mother ni kujitafutia stress tu. Hawaachanagi hawa. Kama uko fresh tafuta fresh mwenzio muanze kwa score ya 0-0. Vinginevyo jiandae kuja kutuomba ushauri hapa.
 
Ila status bana Kuna watu ukiona tu unajua maisha yake yalivo ila Kuna wengine utasugua bench kumjua kwa kutumia status
Asilimia 90 ya wanawake wanaeleza Emotions na feelings zao kupitia status...!! Kama mdangaji utajua tu kama KAGOMBANA NA BEIB WAKE status itakwambia :D :D :D ila kwa wanaume ni wachache sana yani asilimia 2 unaweza jua maisha yake kwa social media
 
Back
Top Bottom