Mkuu umeeleza vizuri sana lakini nipende tu kuongezea hapo kwamba ni vigumu sana kumtambua mwanaume muoaji,wengi sana wana act but hakuna uhalisia. Nikupe mfano huu,kuna jamaa mmoja alipata bint tena bint mtulivu kabisa,wakaanzisha mahusiano naye,bint alikuwa hajaguswa na yyte,Hadi jamaa alikuwa anatuambia amebahatidhs kupata mke,walidumu kwenye mahusiano na wakapata watoto,wakatambulishana kwa wazazi na process za ndoa kafanyika.
Baada ya muda kidogo jamaa akaanza kubadilika gafla tu kumbe wakati wako kwenye mahusiano na bint alipata mchepuko akauzalisha huko,then baada ya mkewe mtarajiwa kugundua kila kitu kikaharibika na bint akabaki kuwa single mother.
So unaweza kuona ni jinsi gani kukosa maadili kwa vijana wote wa kike ma wakiume kunaweza kuleta madhsra,japo wanawake ndo wanaoathirika zaidi.
Umetoa SoMo zuri sana kuwatahadharisha wanawake kuacha kuzalia nyumbani,Hilo nakuunga mkono kwa 100% lakini pia na Imani zetu pia ziwe kama mwongozo wa kutupa wenzi walio sahihi.