Mi nafikiri kila mmoja ashinde mechi zake,anayetaka kuoa single mother muacheni aoe,maana amemchagua yeye mwenyewe,kuoa single mother sio dhambi,ila tu tahadhari ni muhimu.
Lakini pia vijana punguzeni tamaa na uongo sio kila single mother alitaka kuwa hivyo,kuna wengine wamekuwa hivyo kwa kuwaamini vijana wa hovyo ambao walikuja kwa nia ya kutaka kuoa mwisho wa siku wakaingia mitini.
Mwisho kabisa mahusiano hayana formula,kama ingekuwepo kila mtu angeifwata,hivyo vijana wote wa kike kwa wakiume ukitaka kuingia kwenye mahusiano mshurikishe Mungu naye atakupa Alie sahihi,tofauti na hapo vilio havitaisha humu.
Mkuu upo sahihi, lakini haupo sahihi kabisa.
Unaweza usinielewe nilichosema hapo, lakini ngoja nikueleweshe ili uelewe.
Mwanamke ni Maua ambayo yanapendeza na yanayotuvutia wanaume. Unakubali au unakataa?
Kama jibu lako ni ndio, basi kitu chochote mfano wa maua yanavyovutia siku zote huwa kinapiganiwa na wengi kwasababu ya uzuri wake.
Kwenye hao wanaokuja kumtaka mwanamke kuna wanaume wema na wabaya, sio rahisi kumgundua yupi ni mwema au mbaya ila Muumba katuwekea misingi ya kumgundua Mwanaume mwema, na always anajulikana kwasababu ya NDOA na sio vyenginevyo.
Mkuu, wanawake wanapewa Elimu ya kujitunza na Wazazi/Walezi a hata mashuleni tangia wakiwa wadogo. Kama unabisha waulize watakwambia wenyewe (Wanawake)
Elimu wanayopewa ni Elimu ya kuwalinda na madhara yasisi wanaume wenye tamaa. Swali langu ni kwanini hawawasikilizi wazazi wao kuhusu kujitunza?
Mpaka hapo naamini ushaona shida ipo wapi.
Wanawake inapaswa wajitambue na wajue kuwa Unalokatazwa lina madhara hata kama utajifanya mjanja kiasi gani (Especially kwenye uzazi kuzaa nje).
Kuhusu wanaume kuoa single mothers hakuna aliowakataza, ila tunawapa elimu mapema kuhusu matatizo ya hao watu wenye mapenzi nusu nusu (Single mothers).
MWANAMKE MWENYE MAMBO MENGI HAWEZI KUWA MKE, NA PIA HAWEZI KUTULIA MAANA AKILI YAKE HAINA UTULIVU.