Hiii tujazane ujinga au ndiyo uhalisia uliopo? Nimekwambia tunashuhudia ndoa nyingi ambazo wanawake wana tabia hizo na ndoa zinadumu vizuri tu hii dunia imeshaharibika yaani
Hivyo msidhani hizi pumba mnazoongea humu eti watu wote kabisa wanazifanyia kazi hakuna kitu kama hicho wanaume waovu na wanawake waovu walikuwepo wapo na wataendelea kuwepo hadi mwisho wa dunia
Hiyo dunia mnayoitaka ninyi eti wanaume muwe mashetani mfanye tu maovu mnavyojisikia ila wanawake wawe malaika watulie tu wawe wapole haijawahi kuwepo haipo na haitakuja kuwepo
Na huo ndiyo ukweli mchungu wewe wanawake wasioolewa wanakuuma nini tafuta mmoja mwenye tabia nzuri oa tulia kama unaona hawapo endelea kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha ukifa utaenda kujuana na Mungu vizuri huko!