1. Hayo ni maigizo yaliyoasisiwa na mafisadi wa CCM, hivi ukame wote ulioko Ihanja watu hawana chakula ili waishi then unawaambia wachangie maendeleo wakati wakinunua mafuta ya taa,kiberiti,kanga,mswaki na vitu vyote wanachangia VAT,wanachangia mwenge,wanachangia Elimu,maji n.k,
2. leo unawaabia hawa maskini wachangie maendeleo wakati mtoto wa mshua anamiliki petrol station kama 100 hiv na wajombaze wametajwa katika mabilioni ya Uswisi.
3. Hata mm mwajiriwa nalipia VAT katika umeme,maji,mshahara nao nalipia kodi,nikinywa bia nalipia VAT,na wakati huo huo natakiwa nichangie eti maendeleo!!!!!!!!!!!.Hizo kodi zote zinztumikaje????????????.
4. Wananchi wamefumbuliwa macho sasa wamebaini kuwa nchi ya Tanganyika yenye umri wa miaka 51 tangu uhuru ni nchi yenye asali,maziwa,dhahabu,gesi,tanzanite,twiga wengi mpaka wengine wanapanda ndege.
5. Watanganyika 85% wanaishi katika matembe,vichuguu,mbavu za mbwa,misonge,nk then unawaambia wachangie maendeleo huu ni upuuzi na utombo wa kuku.
6. Watanganyika wengine waliohoji matumizi ya serikali waliambiwa,wale nyasi ili ndege ya mjomba inunuliwe,wengine waliambiwa wapige mbizi,wengine waliambiwa wana wivu wa kike,mabinti waliopata mimba shuleni waliambiwa wanaviherehere,wengine wakaambiwa waende motoni,kuzimu (go to hell).