Singida: Diwani wa kata ya Iseke ajiuzuru

Singida: Diwani wa kata ya Iseke ajiuzuru

JUMATANO, JANUARI 02, 2013 05:18 NA NATHANIEL LIMU, SINGIDA

SERA ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), ya kukataza wananchi kuchangia maendeleo yao, imesababisha diwani wa chama hicho Kata ya Iseka, Amos Rubein Mughenyi, jimbo la Singida magharibi, kujiuzulu.

Akitangaza uamuzi huo, kwa waandishi wa habari, Amosi alisema amejiuzulu nafasi ya udiwani huo kuanzia Desemba 21, mwaka jana.

Alisema uamuzi wake, haujatokana na kushawishiwa wala kulazimishwa na mtu au chama chochote cha siasa, bali umetokana na CHADEMA kumzuia kushirikiana na viongozi wa Serikali ngazi ya wilaya na mkoa kusimamia shughuli za maendeleo.

Alisema amekuwa akishinikizwa asikubaliane na changizo (michango) ya aina yoyote ya maendeleo ya kata yake, kwa madai kuwa jukumu la kuwaletea maendeleo wakazi wa kata ya Iseka, ni la Serikali pekee.

“Hivi sasa, Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Iseke (WDC), imeazimia kufanya harambee kwa ajili ya kutafuta fedha za ujenzi wa madarasa na maabara katika shule yetu ya sekondari. Tunapendekeza Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli awe mgeni rasmi katika harambee hiyo, CHADEMA wamenigomea,” alisema Amosi.

Alisema viongozi wa CHADEMA wilaya, wamemtaka akae pembeni asijihusishe na harambee hiyo na kama atalazimika kushiriki atajiondoa ndani ya chama.

“Nimeamua kwa ridhaa yangu mwenyewe kujiuzulu wadhifa huu, ili wananchi wangu wawe huru kujipangia shughuli zao za maendeleo, bila kuzuiwa na itikadi ya CHADEMA,” alisema Amosi.

Amewaomba viongozi wa Serikali na hasa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Manju Msambya, kuendelea kuwaunga mkono wananchi wa Iseke ili wafanikishe harambee hiyo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Illuminata Mwendwa, amekiri kupokea barua ya Amos kujiuzulu.

Tundu Lissu mara kwa mara, amekuwa akiwaeleza wananchi wake watakuwa likizo ya kutochangia maendeleo hadi ubunge wake utakapokoma.

 

Nilidhani WANANCHI wameshachangia MAENDELEO ya MAENEO yao kwa ULIPAJI wa KODI; Sasa kwanini Watoe MICHANGO MFUKONI MWAO na SIO ENEO TAJIRI NCHINI? AU ndio SEHEMU ya ULAJI kwa BAADHI ya VIONGOZI??

Inashangaza HII SABABU ya DIWANI...
 
Lissu amekuwa mbunge kwa miaka mitatu sasa. Huyo Diwani anaweza kusema kulikuwa na maendeleo gani Singida (kote) kabla ya Lissu hajawa mbunge na sasa? Walala hoi wachange, wachache wafiche hela Uswiss!
 
Sioni ubaya wowote kuchangia katika miradi ya maendeleo ili mradi michango hiyo ni ya HIYARI
 
Sioni ubaya wowote kuchangia katika miradi ya maendeleo ili mradi michango hiyo ni ya HIYARI

Mkuu, mtu anafugakuku wake au analima mtama wake then akiwapeleka sokoni kuwauza anasimamishwa barabarani anatakiwa kulipa ushuru wa uuzaji mifugo au mazao, huo ni unyang'anyi wa mchana kweupe kabisa.
 
Lissu amekuwa mbunge kwa miaka mitatu sasa. Huyo Diwani anaweza kusema kulikuwa na maendeleo gani Singida (kote) kabla ya Lissu hajawa mbunge na sasa? Walala hoi wachange, wachache wafiche hela Uswiss!

acheni nge, ivi chama chenu hakipati ruzuku ya serikali kupitia kodi za wananchi hadi mchangishe kwenye mikutano
 
acheni nge, ivi chama chenu hakipati ruzuku ya serikali kupitia kodi za wananchi hadi mchangishe kwenye mikutano

Na chenu hakipati ruzuku toka serikalini mpaka muibe BOT (EPA)?
 
Daima mtu akishindwa husingizia vijimambo.
 
Back
Top Bottom