Singida: Diwani wa kata ya Iseke ajiuzuru

Singida: Diwani wa kata ya Iseke ajiuzuru

Ngoma inogile,juzi ilikuwa mwanza na ilemela leo kwa tundu lissu
 
January inakaribia watoto wanahitaji ada na sare za shule, ni rahisi sana kwa watu dhaifu kuuza utu wao kwasababu ya njaa, ndivyo ilivyo kwa diwani huyu, CCM wana hela za kuhonga CDM wana Mungu.
 
Inafurahisha kusikia kuwa wananchi wa kata ya Ikungi wanalilia kuchangia maendeleo na kwamba ni Mbunge wao tu ndio anawazuia! Hakika hawa wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwani wako watanzania wengi wanakwepa hata kulipa kodi wakiwemo wafayabihashara, wanasiasa na hata wananchi wa kawaida. TRA wanapaswa kwenda kujifunza kwa hawa wananchi pengine itasaidia kuboresha mikakati ya kulipa kodi pasipo shuruti.
mkuu za kuambiwa changanya na za kwako! Hahaaaaaa.
 
Amos mughenyi aliekuwa diwani wa kata ya iseke kupitia chadema amejiuzulu kwa madai kuwa amechoshwa na sera mbovu za chama hicho za kuwakataza wananchi kuchangia maendeleo kitendo kilichosababisha kudumaa kwa huduma za kijamii kwenye kata yake iliyopo wilaya ya ikungi jimbo la tundu lissu.

Mkuu unyakhae,

Naona unafurahia chama chako kupoteza Diwani Mmoja. Wewe haufai kabisa. Umeishabikia hii post na hata uaanzisha post yako separately ikaletwa kuchanganywa na hii hapa.

Umewasikia Makamanda wanaoenda Kanda ya Ziwa na Mwingine anaenda Songea?

CHADEMA, KANYAGA TWENDE..!

Tunasubiria Uchaguzi Makuyuni, Ifakara (RIP Marehemu Wote), Arusha kwa Mawazo na kwa akina Bayo, Ikungi n.k.
 
Last edited by a moderator:
Kutegemea kupangiwa na kuletewa maendeleo na government ni sera iliyopitwa na wakati
 
Naam,huyu anaingia... huyu anatoka..... CHADEMA inaongozwa na watu wanaoguswa na matatizo ya watanzania na si wawindaji wa fursa binafsi...Inawezekana kabisa aliona gwanda akahisi kuna ulaji huko.Hana hoja ya msingi ya kuhama chama ila maslahi binafsi tu maana kama ni kuboresha huduma za jamii angeisimamia halmashauri,mamlaka za serikali pamoja na mfuko wa maendeleo ya jimbo.Wananchi wa kijijini wangechangia nini kama si kuwapora hata kile kidogo wanachopata,wengi wao wanaishi chini ya dola.Huyu hana hata huruma na watoto wanashindwa kusoma kwa kukosa pesa ya dawati na michango mingine... Mama wajawazito wanaokufa kwa kukosa pesa ya matibabu je? Acheni hizo bwana....
 
Tundu lissu ana hali mbaya jimboni kwake, umaarufu nje ya jimbo lakini nyumbani kunateketea

Unajifurahisha. Tumetoka jimboni kwa lissu hata wiki haijaisha. Lissu ni maarufu sasa kuliko wakati wowote huko jimboni kwake. Ccm hawawezi hata kufanya mikutano jimboni kwa lissu.

BTW: huyu diwani hakuwa jimbo la lissu. Alikuwa wa singida magharibi wakati jimbo la lissu ni la mashariki.
 
kabla hajajiuzulu angetuambia vijana wa wilaya ya ikungi watapata wapi pesa za kuchangia miradi ya maendeleo wakati kazi hakuna? Huyo diwani kashanunuliwa ''njau''

ha ha ha mtaongea kila neno mwaka huu...hadi 2015 kazi ipo...
 
unajifurahisha. Tumetoka jimboni kwa lissu hata wiki haijaisha. Lissu ni maarufu sasa kuliko wakati wowote huko jimboni kwake. Ccm hawawezi hata kufanya mikutano jimboni kwa lissu.

Btw: Huyu diwani hakuwa jimbo la lissu. Alikuwa wa singida magharibi wakati jimbo la lissu ni la mashariki.
maarufu kwa lipi hasa????mana hakuna ambacho kafanya utasema anapita mbele kuongea kafanya na wananchi wamkubali
 
Tundu lissu ana hali mbaya jimboni kwake, umaarufu nje ya jimbo lakini nyumbani kunateketea

Well.,cjui unayoyaongea yanahusianaje na uzi ulioletwa. Tundu Augustino Mughwai Lissu ni mbunge wa Singida Mashariki.,Iseke ni kata iliyopo Singida Magharibi, jimbo lnaloongozwa na Missanga(CCM).. Kama unataka tuje na hoja za kuonesha maendeleo ambayo Lissu analeta Jimboni kwake,hebu anzisha uzi mwingine tafadhali...
 
January inakaribia watoto wanahitaji ada na sare za shule, ni rahisi sana kwa watu dhaifu kuuza utu wao kwasababu ya njaa, ndivyo ilivyo kwa diwani huyu, CCM wana hela za kuhonga CDM wana Mungu.

kwanini tunakimbilia kusema amenunuliwa na ccm? Kwanini hatuangalii matatizo yetu ya ndani? Huu ni ulimbukeni.
 
Jimbo la Singida Mashariki chini ya Tundu Lissu limeshuhudia kukua kwa haraka kwa huduma nyingi za msingi kuliko wakati mwingine wowote. Ndani ya muda mfupi,tayari wananchi wanajivunia kuwa naye. Ni mojawapo kati ya majimbo ambayo CCM wanayaogopa zaidi.,ni vigumu kwao hata kufanya mkutano wa siasa.. Wanaokuja na uongo kuwa Lissu hajafanya lolote wazingatie kwanza juhudi zake kuendeleza barabara, harakati za kuwatetea wananchi waliodhulumiwa ktk malipo ya mradi wa umeme., huduma za maji, matumizi wazi ya mfuko wa jimbo, na majukumu makubwa ya kuyafikisha mawazo ya wananchi wake bungeni,jukumu ambalo ndilo hasa waliomchagua walimkabidhi..
 
Well.,cjui unayoyaongea yanahusianaje na uzi ulioletwa. Tundu Augustino Mughwai Lissu ni mbunge wa Singida Mashariki.,Iseke ni kata iliyopo Singida Magharibi, jimbo lnaloongozwa na Missanga(CCM).. Kama unataka tuje na hoja za kuonesha maendeleo ambayo Lissu analeta Jimboni kwake,hebu anzisha uzi mwingine tafadhali...

iseke ipo wilaya gani na sgd mashariki iko wilaya gani? na pili diwani alikuwa wa chama gani na lissu ni mbunge wa chama gani?jibu ni wilaya ya ikungi chama ni chadema.kwa mwenye kutafakari kwa kina na kwa mapana atakubali mapungufu na kuyafanyia kazi
 
Back
Top Bottom