Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,646
- 2,911
Wewe inawezekana una uelewa zaidi wa haya mambo LAKINI mimi ninachojua ni kuwa SINGAPORE ndiyo nchi inayoongoza kwa productivity Duniani. Mataifa makubwa kama Japan na Marekani huwapeleka watu wao kwenda kujifunza productivity Singapore.Kwa siku Meli 60???? Kwa siku Makontena 91,000??? Really??
Nadhani bandari zinazoheshimika kwa ufanisi kama Felixstowe, Barcelona na HIT zinapaswa kujifunza kutoka kwa hawa jamaa.
Bandari haiwezi hudumia meli 60 au kontena 91,000 kwa siku (nadhani ikimaanisha 91000TEUs) afu ikawa inachangia only 7% ya pato la taifa. Sijui lakini..... kuna maajabu mengi sana siku hizi duniani.
Kama inawezekana Singapore ijenge chuo hapa nchini ili kuwafundisha Watanzania productivity maana mpaka sasa ipo chini sana. Tena kama Singapore itawekeza nchini, serikali kwa kuanzia iruhusu makampuni hayo ya Singapore yawalete wafanyakazi wengi toka Singapore ambao watapunguzwa taratibu, lengo ni kuwafanya watanzania wajifunze jinsi kazi zinavyoweza kufanyika kwa speed na accuracy. Watanzania accuracy yetu ni ndogo, speed ndogo, kuthamini muda ni zero, kulalamika na majungu 90%, matumizi -na kutanua 100%.
Note: Productivity = Tija= speed + accuracy