Singapore kuboresha Bandari ya Dar

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
WAZIRI wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dk Koh Poh Koon amesema wamepanga kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuwa kiunganishi cha biashara kati ya nchi hiyo na mataifa mengine ya Afrika Mashariki (EAC).

Dk Koon aliyasema hayo jana wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma, na kwamba Singapore ipo tayari kutoa fursa kwa wataalamu wa Tanzania kwenda kufanya kazi katika Bandari ya Singapore ili kupata uzoefu utakaosaidia uendeshaji wa bandari za Tanzania.

Dk Koon ambaye ameambatana na wafanyabiashara wakubwa wapatao 40, alimweleza Waziri Mkuu kwamba Kampuni ya Hyflux ya Singapore, imeanza kuwekeza nchini kwa kujenga eneo maalumu la uchumi mkoani Morogoro, ambako ndani ya kipindi cha miaka mitano wanatarajia kujenga miundombinu wezeshi ya kuweka viwanda vya kati, maeneo ya biashara na nyumba za makazi zipatazo 37,000.

“Jiwe la msingi la mradi huo litawekwa tarehe 29 Aprili 2016 na Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage,” alisema waziri huyo wa Singapore.

Mbali na ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji, Dk Koon alimweleza Waziri Mkuu kwamba nchi yake itaisaidia Tanzania kujenga uwezo wa kiufundi katika maeneo mbalimbali ya menejimenti na uendeshaji wa bandari na ufundi katika sekta ya gesi na mafuta.

“Hadi sasa makampuni ya Singapore yaliyowekeza nchini ni pamoja na Pavillion Energy ambayo imewekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 katika sekta ya gesi na inatarajia kuwekeza zaidi dola za kimarekani bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa kinu cha kuchakata gesi (LNG plant) kitakachojengwa mikoa ya Kusini kwa ubia na makampuni ya gesi kutoka Ulaya na Marekani,” alifafanua.

Alisema Kampuni ya PIL ya Singapore inatarajia kuwekeza Dola za Marekani milioni 400 kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kutoa huduma kwa kampuni ya gesi. Alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo pamoja na kuweka mikakati ya kuinua uchumi na kupanua wigo wa biashara.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru Serikali ya Singapore kwa uwekezaji unaofanywa na kampuni zake nchini na kwa misaada ya kiufundi ambayo wameitoa kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Ili kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kukuza uchumi, Waziri Mkuu amezikaribisha kampuni nyingine za Singapore kuja nchini kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda, mahoteli, kilimo na nishati.

Alimuahidi Dk Koon kwamba Tanzania ipo tayari kukamilisha mazungumzo ya kusaini Mkataba wa Kuvutia na kulinda uwekezaji baina ya nchi mbili na Mkataba wa Kuepuka kutoza ushuru mara mbili ili kuvutia uwekezaji zaidi kutoka Singapore.

Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka Watanzania kutumia fursa ya ushirikiano kati ya Singapore na Tanzania, kuanzisha biashara mpya zitakazowanufaisha wote.

Alisema Singapore ina uwezo mkubwa kibiashara pamoja na uzoefu wa siku nyingi kwenye uendeshaji wa bandari hivyo Tanzania itapata nafasi ya kujifunza namna ya uendeshaji katika sekta hizo.

Alisema Tanzania imefungua milango ya uwekezaji kwa wafanyabiashara wa Singapore, kuja kuwekeza katika sekta za viwanda, usafiri wa anga na kwenye Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZ).

CHANZO: Habarileo
 
Kama tunataka ufanisi na faida kwenye bandari zetu lazima tujifunze kutoka The Port of Singapore Authority.

Hawa jamaa wanawezesha asilimia zaidi 7 za pato la taifa kupatikana kwa njia ya maritime industry. Wanashughulika kwa ufanisi na meli zaidi ya 60 kwa siku, makontena zaidi ya 91,000 kwa siku.
Wenzetu wanatumia one-stop-centre katika documentation za makontena na hakuna rushwa, uzembe na urasimu.

Sisi bandari zetu zinanuka uzembe, rushwa na ufisadi kuanzia wafagiaji mpaka top level management.
Ikumbukwe, Singapore ilikuwa ni nchi masikini sawa na Tanzania kwenye miaka ya 1970 lakini kwa sasa ni moja kati ya nchi tajiri duniani.

Where there is will there is a way!
 
Kama tunataka ufanisi na faida kwenye bandari zetu lazima tujifunze kutoka The Port of Singapore Authority.

Hawa jamaa wanawezesha asilimia zaidi 7 za pato la taifa kupatikana kwa njia ya maritime industry.

Wanashughulika kwa ufanisi na meli zaidi ya 60 kwa siku, makontena zaidi ya 91,000 kwa siku.

Wenzetu wanatumia one-stop-centre katika documentation za makontena na hakuna rushwa, uzembe na urasimu.

Sisi bandari zetu zinanuka uzembe, rushwa na ufisadi kuanzia wafagiaji mpaka top level management.

Ikumbukwe, Singapore ilikuwa ni nchi masikini sawa na Tanzania kwenye miaka ya 1970 lakini kwa sasa ni moja kati ya nchi tajiri duniani.

Where there is will there is a way!

Kwa siku Meli 60???? Kwa siku Makontena 91,000??? Really??

Nadhani bandari zinazoheshimika kwa ufanisi kama Felixstowe, Barcelona na HIT zinapaswa kujifunza kutoka kwa hawa jamaa.

Bandari haiwezi hudumia meli 60 au kontena 91,000 kwa siku (nadhani ikimaanisha 91000TEUs) afu ikawa inachangia only 7% ya pato la taifa. Sijui lakini..... kuna maajabu mengi sana siku hizi duniani.
 
Mkuu, unashangaa nini?

Wenzetu wanapiga mzigo na hawataki siasa kwenye kazi.
 
Hapana kiongozi..... Acha nishangae tu. Napenda kujua hii nchi ina bandari ngapi? Naamini kwa mzigo huo lazima iwe inahudumia nchi zaidi ya 10.
 
Nilisoma mwaka jana articles kuhusu ufanisi wa hawa jamaa na kwa kukusaidia ili uamini nipe muda nikutafutie moja ya article.
 
WAZIRI wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dk Koh Poh Koon amesema wamepanga kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuwa kiunganishi cha biashara kati ya nchi hiyo na mataifa mengine ya Afrika Mashariki (EAC).

Dk Koon aliyasema hayo jana wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma, na kwamba Singapore ipo tayari kutoa fursa kwa wataalamu wa Tanzania kwenda kufanya kazi katika Bandari ya Singapore ili kupata uzoefu utakaosaidia uendeshaji wa bandari za Tanzania.

Dk Koon ambaye ameambatana na wafanyabiashara wakubwa wapatao 40, alimweleza Waziri Mkuu kwamba Kampuni ya Hyflux ya Singapore, imeanza kuwekeza nchini kwa kujenga eneo maalumu la uchumi mkoani Morogoro, ambako ndani ya kipindi cha miaka mitano wanatarajia kujenga miundombinu wezeshi ya kuweka viwanda vya kati, maeneo ya biashara na nyumba za makazi zipatazo 37,000.

“Jiwe la msingi la mradi huo litawekwa tarehe 29 Aprili 2016 na Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage,” alisema waziri huyo wa Singapore.

Mbali na ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji, Dk Koon alimweleza Waziri Mkuu kwamba nchi yake itaisaidia Tanzania kujenga uwezo wa kiufundi katika maeneo mbalimbali ya menejimenti na uendeshaji wa bandari na ufundi katika sekta ya gesi na mafuta.

“Hadi sasa makampuni ya Singapore yaliyowekeza nchini ni pamoja na Pavillion Energy ambayo imewekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 katika sekta ya gesi na inatarajia kuwekeza zaidi dola za kimarekani bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa kinu cha kuchakata gesi (LNG plant) kitakachojengwa mikoa ya Kusini kwa ubia na makampuni ya gesi kutoka Ulaya na Marekani,” alifafanua.

Alisema Kampuni ya PIL ya Singapore inatarajia kuwekeza Dola za Marekani milioni 400 kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kutoa huduma kwa kampuni ya gesi. Alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo pamoja na kuweka mikakati ya kuinua uchumi na kupanua wigo wa biashara.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru Serikali ya Singapore kwa uwekezaji unaofanywa na kampuni zake nchini na kwa misaada ya kiufundi ambayo wameitoa kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Ili kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kukuza uchumi, Waziri Mkuu amezikaribisha kampuni nyingine za Singapore kuja nchini kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda, mahoteli, kilimo na nishati.

Alimuahidi Dk Koon kwamba Tanzania ipo tayari kukamilisha mazungumzo ya kusaini Mkataba wa Kuvutia na kulinda uwekezaji baina ya nchi mbili na Mkataba wa Kuepuka kutoza ushuru mara mbili ili kuvutia uwekezaji zaidi kutoka Singapore.

Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka Watanzania kutumia fursa ya ushirikiano kati ya Singapore na Tanzania, kuanzisha biashara mpya zitakazowanufaisha wote.

Alisema Singapore ina uwezo mkubwa kibiashara pamoja na uzoefu wa siku nyingi kwenye uendeshaji wa bandari hivyo Tanzania itapata nafasi ya kujifunza namna ya uendeshaji katika sekta hizo.

Alisema Tanzania imefungua milango ya uwekezaji kwa wafanyabiashara wa Singapore, kuja kuwekeza katika sekta za viwanda, usafiri wa anga na kwenye Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZ).
 
Sasa ni wakati muafaka pia kwa Tanzania kwenda kujenga Barabara za DRC, kuna soko kubwa ila Barabara ni mbovu mno
 
Tanzania mmeshajenga barabara ngapi hadi kufikiri kwenda kujenga DRC? Kuna kampuni ngapi za Kitanzania ambazo zina uwezo wa kujenga barabara zaidi ya 100 km?
 
Kwa siku Meli 60???? Kwa siku Makontena 91,000??? Really??

Nadhani bandari zinazoheshimika kwa ufanisi kama Felixstowe, Barcelona na HIT zinapaswa kujifunza kutoka kwa hawa jamaa.

Bandari haiwezi hudumia meli 60 au kontena 91,000 kwa siku (nadhani ikimaanisha 91000TEUs) afu ikawa inachangia only 7% ya pato la taifa. Sijui lakini..... kuna maajabu mengi sana siku hizi duniani.
Sina takwimu za Singapore lakini ni VERY VERY possible kv Bandari ya Singapore is more than ordinary port but transhipment port! Bandari ya Singapore ipo very busy na ni among the busiest port duniani! Na kv ni transhipment hub, suala la kuhudumia meli na kontena nyingi kwa cku ni kawaida sana!

In short, I love Singapore linapokuja suala la port business. Na hawa ndugu wapo more than efficient in Service sector.
 
At any time kuna meli 1000 au zaidi zinasubiri bahari kuu kuingia gatini Singapore, Unashangaa nini? Wengine wanachapa kazi sisi tunawaza na kunuka rushwa tu. Nimetembelea mwenyewe sio kusoma ama kuambiwa.
 
Sina takwimu za Singapore lakini ni VERY VERY possible kv Bandari ya Singapore is more than ordinary port but transhipment port! Bandari ya Singapore ipo very busy na ni among the busiest port duniani! Na kv ni transhipment hub, suala la kuhudumia meli na kontena nyingi kwa cku ni kawaida sana!

In short, I love Singapore linapokuja suala la port business. Na hawa ndugu wapo more than efficient in Service sector.
Thanks for the info. Natamani kujua ukubwa wa hii port. Au hii performance ni combination ya ports zote. Kwa port moja kufanya yote haya.... lazima itakuwa na eneo kubwa sana na equipment zisizohesabika
 
Nilisoma mwaka jana articles kuhusu ufanisi wa hawa jamaa na kwa kukusaidia ili uamini nipe muda nikutafutie moja ya article.
Ntashukuru kiongozi. Nimejitahidi ku google lakini sijafanikiwa kupata nlichokitaka
 
Hapana kiongozi..... Acha nishangae tu. Napenda kujua hii nchi ina bandari ngapi? Naamini kwa mzigo huo lazima iwe inahudumia nchi zaidi ya 10.

Transit zote/nyingi za kutoka Australia na nchi nyingine za Far East ikiwamo China na Japana kwenda kwingineko duniani hupita Singapore na nchi nyingne nyingi tu. Wana export hata ambacho hawazalishi, ikiwa ni pa,oja na mawese ya Malysia, karatasi nk.
 
Sina takwimu za Singapore lakini ni VERY VERY possible kv Bandari ya Singapore is more than ordinary port but transhipment port! Bandari ya Singapore ipo very busy na ni among the busiest port duniani! Na kv ni transhipment hub, suala la kuhudumia meli na kontena nyingi kwa cku ni kawaida sana!

In short, I love Singapore linapokuja suala la port business. Na hawa ndugu wapo more than efficient in Service sector.

Takwimu za wakatu huo mimi nimetembelea bandari hiyo ilikuwa ya 3 busiest duniani na 1 fastest in cargo handling duniani. Kumbuka ni mji tu kama Dar, msisikie nchi ya Singapore mkadhani ni kama Tanzania ambayo kwao sisi ni Bara zima!!!
 
Thanks for the info. Natamani kujua ukubwa wa hii port. Au hii performance ni combination ya ports zote. Kwa port moja kufanya yote haya.... lazima itakuwa na eneo kubwa sana na equipment zisizohesabika

Ni port moja mkuu maana Singapore ni city-state. Ni mji/mkoa kama wa Dar tu, kwa hiyo hamna nyingine ya Tanga na Mtwara huko.
 
Transit zote/nyingi za kutoka Australia na nchi nyingine za Far East ikiwamo China na Japana kwenda kwingineko duniani hupita Singapore na nchi nyingne nyingi tu. Wana export hata ambacho hawazalishi, ikiwa ni pa,oja na mawese ya Malysia, karatasi nk.
Sure itakuwa busy sana. Mi mshangao wangu ni huu wa kuhudumia meli 60 kwa siku. Hizi meli zitakuwa zinaingia kama ndege kwenye busiest aiport.... Meli 60?? Meli 60 zinapokuwa kwenye port moja lazuma kuna ports kadhaa zitakuwa hazina meli wallah.
 
Back
Top Bottom