Niliwahi kusema mungu wa jk ni Nyerere,kila alichokisema wakati wa kutafuta mgombea uraisi kimetimia!
Nukuu ya mameno ya Mwalimu kuhusu serikali corrupt.....
Serikali corrupt popote pale, haitozi kodi. Serikali corrupt inatumwa na wenye mali.
Inawafanyia kazi wenye mali. Serikali corrupt itamwambiaje mwenye mali, kwamba "utalipa, usipolipa utakiona!" Atacheka tu huyu.
Atakwambia"unaniambia hivyo wewe? kesho siji basi!"
Serikali corrupt haikusanyi kodi. Itabaki kufukuzana fukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani hivi basi.
Yametimia - maana hawa mafisadi wana uwezo wa hata kutuchagulia viongozi wetu ndani ya serikali.
kumbe amerudi nchini, nilisikia katoroka. kama yupo kwanini asikamatwe kusubiri upelelezi akakae ndani pale segerea? polisi wanamchelewesha nini? huyo anatakiwa kukamatwa haraka kabla hajakimbia nchi.
yeye anasema ni mtu wa iringa, hivi mtu wa iringa anaweza kuwa na class ya uwekezaji kama yake, na anataka kesi ikaamuliwe uingereza wakati yeye ni tz? yaani mtz aingie mkataba na serikali yake ya tz halafu aseme kesi ikaamuliwe uingereza?hahahaha, anamdanganya nani? mtz aje aishi hapa tz kwa permit ya muwekezaji? au aliukana utzNani amkamate huyu jamaa alishajipenyeza ndani ya jeshi la polisi kwa kifupi serikali haina kauli juu ya bwana huyu