CHEF
JF-Expert Member
- Nov 4, 2013
- 222
- 122
Ndugu wapendwa salaam, leo wakati nawaza nani wa kumpigia kura, pamoja na kuona TAL anaweza kuongoza nikiwa na maana ya kusimamia katiba na Sheria za nchi kuongoza kama Rais jambo ambalo ni udhaifu wa mgombea wa CCM JPM , wakati udhaifu wa TAL ni kwamba tusitegemee maendeleo makubwa ya kiuchumi kama anayoyafanya JPM tofauti na usawa katika sheria na katiba mpya jambo ambalo muhimu sana kwa kizazi hiki na kijacho.
Haya twende kwenye maada kuu ambayo jinsi katiba ya chadema inavyo kinzana kusimamia uchumi wa nchi,
Katiba ya Chadema inasema inaitikadi ya mrengo wa kati wakiwa na maana wao sio mabepari wala wajamaa.
Hivyo hivyo chadema wanasema wanaamini katika soko huru yaani FREE MARKET ECONOMY, kitu ambacho msingi wake ni ubepari (CAPITALIST), kwa hiyo CHADEMA wanataka kutupeleka kwenye ubepari?
Hili suala la ubepari limethibitishwa tena na TAL alipokuwa anasema serikali yake itabaki kuwa msimamizi tu wa masuala ya kiuchumi lakini uchumi wote utendeshwa na wananchi wenyewe, hapa akiwa na maana kutakuwa na free market economy ambayo itaendeshwa by demand and supply forces. Huu ni ubepari kabisa, hili suala kwa Tanzania yetu bado hatujafikia , yaani kama ndio CHADEMA wanategemea kuendesha uchumi hivi kutakuwa na athari zifuatazo:
1. Kutaongeza tofauti kubwa sana kati ya wasio nacho na wenye nacho (income gap)
2. Watanzania bado hawajaelimika vyakutosha kwa hiyo watauza ardhi kwa urahisi kwa wenye nacho na kubaki kuwa masikini daima
3. Maisha kubadilika kwa asiye ncho itakuwa ndoto
4. Kutokea kwa machafuko kama Afrika kusini maana wageni watashika uchumi wakati wenyeji wakiwa hohe hahe.
Kwa maelezo haya nafikiri CHADEMA wanatakiwa wakae na kuitafakari katiba yao , baada ya hapo waje waombe ridhaa ya kuongoza nchi.
CHADEMA bado hawajaijua nchi yao na aina ya wananchi wake, tafadhali , chonde, chonde chonde tunahitaji mabadiliko lakini sio kwa katiba hii ya chadema itatupeleka pabaya.